Mzazi tengeneza mtoto muelewa

Mzazi tengeneza mtoto muelewa

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,569
Reaction score
89,214
Inafika kipindi wazazi mnatakiwa kubadili mfumo wa malezi maana watoto wa sasa wamekuwa wagumu, wabishi na akili za kuload kwa muda mrefu. Hii inaonesha kuna tatizo mahala fulani, hata walimu muda mwengine tunawalalamikia lakini sometimes tatizo ni malezi.

Heri ukamtambulisha mtu kitu kuliko kumkaririsha unataka mtoto ajielewe akiwa na miaka 28 tunatengeneza taifa gani? Unamwambia awe na hekima, hiyo hekima ataijuaje bila kumuelewesha matendo hayo ya hekima? Mfundishe kwa utaratibu, mueleweshe kwa uyakinifu, dadavua lipi baya lipi zuri.

Kujitambua na kujielewa kuna raha yake bhana, mweke huru wa kifikra kwenye ulimwengu kuwa na mikakati madhubuti na timilifu kwa mwanao.
Wazazi wengine mpaka kero, unafanya mabaya mbele ya mwanao unategemea nini? Kwake kuna kukopi na kupaste tambua hilo, labda awe anajitambua yeye binafsi atachekecha na kuchuja.

Huku kulalamika kwenu mitoto ya sikuhizi balaa mara imelaaniwa inaonyesha kuzidiwa kete hasa na nguvu ya utandawazi.

Hapa lazima mjue la kufanya.
 
Hao wazazi unaowazungumzia ni hawa wanaoshinda makazini na wakirudi nyumba wapo busy na tv, simu na magazeti!! Hawa watoto hawajabadilika ni wazazi wamebadilika, cha mno wazazi tutambue majukumu yetu kwa watoto wetu jamani, haya mambo ya utandawazi yametukuta wala sio ya kuendekeza. Mshika mawili moja humponyoka aheri utandawazi uponyoke kuliko mwanao, chagua moja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom