KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 36,569
- 89,213
Mtapiga fimbo, mtasema na kulaani lakini kama mtoto si muelewa hatawasikia mpaka mtamkinai wakati umemzaa mwenyewe. Ni furaha ilioje kuona mwanao ana hekima na busara. Hekima na busara hupatikana kwenye uelewa, mzazi anaejielewa humfundisha mwanae kujielewa.
Kujielewa kwa mtoto hujitambua yeye ni nani, afanye nini, anaenda wapi na ametoka wapi ila juhudi ya kumuelewesha mtoto yatoka kwa mzazi. Usisubiri mpaka jamii imueleweshe mtoto wakati kitabu cha uelewa kipo ubongoni mwako kujielewa kwa mtoto hupelekea kuwa makini, mvumilivu, msikivu, ujali, mwepesi kujifunza, mdadisi kwa kutaka kuelewa n.k
Hebu jiulize unamuandaaje mtu ajae kukutunza ukiwa hujiwezi, awe na famili, kazi, kujitegemea n.k. Bila shaka mtu huyo anatakiwa awe na hulka ya kujielewa. Kama mzazi nadhani utajisikia vyema ukiwa umeandaa mtoto mwenye kujielewa lkn ni pressure ya aina gani utakuwa nayo kwa mtoto asiejielewa bila shaka hata ukimuachia mali yako hutajisikia amani kwenye fikra zako.
Yangu ni hayo tu kwa leo 🙁