Mzanzibari mtarajiwa kupewa pasi ya kusafiria chini ya miezi miine..!

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,610
1,250
Haya WaZanzibari wazidisha chachu ya maendeleo kuna habari kuwa kunatayarishwa muswaada wa lazima kwa kila Mzanzibari mtarajiwa atakezaliwa Zanzibar basi ihakikishwe baada ya miezi minne amefunguliwa file na kupewa hati ya kusafiria kwa maana nyingine pasipote na hakuna sababu ya kungojea mpaka atake kusafiri ilivyo kuwa pasi ni haki ya kila raia ,hivyo serikali iwajibike kuhakikisha watoto wate wanaozaliwa wawe wanapatiwa hati hiyo na rekodi yake kutunzwa katika mitambo maalum.
 
mathematics

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
3,327
2,000

hati ya kusafiria au kitambulisho mkazi??
zanzibar wameanza toa lini hati ya kusafiria??
 
chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,143

Kuna sehemu mbili tu katika Tanzania hii zinapotoka pass za kusafiria ya Tanzania ni Daresalam na zanzibar.

kumbukumbu(database) ya majina ya waliopewa kutambulisho cha kusafiria kutoka Zanzibar zinabaki Zanzibar kwa maana hiyo database ya kumbukumbu ya Zanzibar iko tafauti na kumbukumbu za Daresalam .........

Kumbuka kuwa mambo ya ndani ya zanzibar sio ya Tanzania sio ya mungano :)
 
passport sio suala la mambo ya wizara ya mambo ya ndani, passport ni suala la wizara ya mambo ya nje, ipo wizara ya mambo ya nje moja tu.
 
Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
2,000
passport sio suala la mambo ya wizara ya mambo ya ndani, passport ni suala la wizara ya mambo ya nje, ipo wizara ya mambo ya nje moja tu.

Mkuu acha masihara, ina maana ulipoomba pasi (kama unayo) ulienda mambo ya Nje? Pasi zangu zote nilizokuwa nazo, ya kwanza niliomba mwaka 1970, niliiombea Uhamiaji. Na mpaka muda huu ninahitaji Pasi nyingine ninahudumiwa huko huko Mambo ya Ndani! Mkuu, kubali ya kuwa hujui na yaishe...
 
chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,143
2,000
passport sio suala la mambo ya wizara ya mambo ya ndani, passport ni suala la wizara ya mambo ya nje, ipo wizara ya mambo ya nje moja tu.

Kaka unaweza kuzipangua wizara unavyotaka lakini hivyo ndio ilivyo kwa mfumo huu tulionao sasa,Binafsi sijui kama uhamiaji ni wizara ya mambo ya ndani au ya nje lakini sijawahi kuona pasi za kusafiria zinatolewa wizara ya mambo ya nje.

kwa taarifa yako Kama sio mzanzibari ofisi ya uhamiaji ya zanzibar haiwezi kukupa pasi ya kusafiria.... ,inabidi upeleke vielelezo vyote vya kuhakikisha kuwa wewe ni mzanzibari,kama huamini nenda kajaribu.. :)
 
manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,533
2,000
passport sio suala la mambo ya wizara ya mambo ya ndani, passport ni suala la wizara ya mambo ya nje, ipo wizara ya mambo ya nje moja tu.

Wewe umewahi kupata passport kweli !!?Passport hutolewa na uhamiaji na iko chini ya wizara ya mambo ya ndani. Kwa Dar zinatolewa wizara ya mambo ya ndani baada ya kumaliza taratibu uhamiaji kule Temeke.
 
Kibona

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
1,021
2,000
passport sio suala la mambo ya wizara ya mambo ya ndani, passport ni suala la wizara ya mambo ya nje, ipo wizara ya mambo ya nje moja tu.
Passport ni suala la wizara ya mambo ya ndani. Wewe una passport au huna?
 
Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,610
1,250
hati ya kusafiria au kitambulisho mkazi??
zanzibar wameanza toa lini hati ya kusafiria??
Hivi wewe ni wawapi ,yaani umekarabatiwa na serikali ya CCM hadi hujui kama Mzanzibari hati yake ya kusafiria anaichukulia Zanzibar na hata akioa huko Tanganyika basi ,kiilivyo WaTanganyika hawana ruhusa ya kumpa mtoto wake pasi ya kusafiria kutoka DSM ni lazima pasi itokee Zanzibar ,bado Uzanzibari unalindwa na kudhibitiwa kiaina,hii ya kuwapa watoto pasi ni mkakati wa kuhakikisha katika miaka kumi na tano ijayo hakutakuwa na mtoto anaenda kuombewa pasi ,suali litakuwa alikuwa wapi na kwa nini na ukumbuke na gharama zitabidi zilipwe zaidi ,kuliko akiwa bado hajatimiza miezi minne ambapo ni bure.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom