Vannele
JF-Expert Member
- May 4, 2013
- 287
- 90
Wenzangu mzaha umeniletea balaa ndani ya ndoa... Jana tulikuwa tupo kwenye utani mwepesi si nikajifanya nimezira mwenzangu! Nikamwambia baba watoto leo hamna kitu tunalala mzungu wa nne... Si nikajifanya kugeukia upande mwengine kweli tukawa tumelala mzungu wa nne lakini lengo langu lilikuwa kumtania tu nizuge kama dk. 5 nirudi kama kawaida... Mwenzangu si nikapitiwa na usingizi! Kutahamaki nimestuka saa kumi na mbili... Hapa ndani pametibuka tifu la hatari anasema nilitoka kwa bwana ndo mana nimemfanyia hivyo na kazira ameoga ameondoka... Nifanyeje wenzangu amiamini kuwa ulikuwa mzaha tu sikuwa nimedhamiria.