Mzabuni aigaragaza halmashauri mahakamani

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpanda, mkoani Rukwa, imeamuru halmashauri ya Mji wa Mpanda kumlipa Simon Savery zaidi ya Sh69 milioni kutokana na halmashauri hiyo kumvunja mkataba wake na mzabuni huyo.Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Desdelius Magezi, kufuatia kesi ya madai namba 12 ya mwaka 2010 iliyofunguliwa na mzabuni huyo dhidi ya Halmashauri ya Mji wa Mpanda.

Awali, kwenye hati ya madai mahakamani hapo, mzabuni huyo alikuwa akidai kuwa halmashauri hiyo ilimkosesha mapato ya faida ya Sh69,993,000, baada ya kuvunja mkataba wa kuuza kokoto ambazo ni mali ya halmashauri hiyo.Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, Septemba 22 , mwaka jana halmashauri ya mji iliingia mkataba na mzabuni kuuza kokoto ambazo ni mali ya halmashauri.

Hati ya mkataba huo inaonyesha kuanza kutumika Octoba Mosi, mwaka jana, ulisainiwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya mji huo, Henry Haule, kwa niaba ya halmashauri hiyo.Mkurugenzi huyo amestaafu utumishi wa umma tangu Desemba 31, mwaka jana.Katika kesi hiyo mlalamikaji alikuwa akiwakilishwa na Mwanasheria wa Kujitegemea, Bartazar Chambi wa Sumbawanga mjini, huku halmashauri ikitetewa na Mwanasheria wake, Joshua Sanga.

Akisoma hukumu, Hakimu Magezi alisema baada ya kusikiliza kwa makini maelezo ya pande zote, ameridhika pasi na shaka kuwa Halamashauri ya Mji huo wa Mpanda, ilivunja mkataba kwa makosa.Hivyo Magezi aliamuru halmashauri hiyo kumlipa Savery Sh69,993,000, huku akiionya kutorudia makosa ya kufuta mikataba holela bila kuzingatia taratibu, kanuni na sheria.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom