Niongee lugha ya babu.
Nakubaliana na maoni yako Kwa 100% lakini nadhani tatizo linaanzia Bodi ya Ligi wakati wanatunga kanuni hawazingatii hili. Hili likiwekwa kwenye kanuni hutaliona tena. EPL wamelimudu sababu ya kanuni. Time wastage pale EPL unaona kabisa ilikuwa na sababu za Msingi. Mchezaji kaumia au kuna tukio lililo nje ya uwezo wa waamuzi. Waamuzi wa Tanzania wanaendekeza mno Wachezaji. Anaona kabisa huyu anachelewesha Muda makusudi lakini akilalamikiwa anaonyesha saa kwamba ataongeza dakika. Kichekesho ni dakika zitakazoongezwa.
Unaona mwamuzi kabla ya mechi kuanza anawaita makipa wa timu mbili na kuwaonya mapema kwamba hatavumilia ucheleweshaji Muda. Subiri Mechi ianze utaona maajabu.