My lady! Is this a True' love...

Nikhil

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
361
Reaction score
120
Wakuu habari zenu!
Nimetupia thread hii kwenu as a 'GREAT THINKERS' mnisaidie kimawazo juu ya huyu Mpenzi wangu".
Mimi ni kijana wa miaka 19 nilikuwa na mpenzi wangu aitwaye Grace kiukweli nilimpenda sana na upendo wangu mi na yeye umeanzia tangia nikiwa kidato cha pili na kusababisha hata perfomamce yangu kimasomo kushuka juu ya upendo wangu kwake.
Tuliendelea na uhusiano wetu huku tukiwa tumejiwekea malengo kuwa one day tutakuja kufunga pingu za Maisha, nilikuwa mstari wa mbele kwa kumsadia kwa kila jambo kwa kipindi tulipo kuwa shuleni hii ikanifanya nijisahau kimasomo cha ajabu performance yake ikawa nzuri japokuwa na yeye alikuwa bize na mimi ' Marafiki zangu walinionya japokuwa sikuwaelewa huku nikiwatia moyo kuwa nitabadilika.
Mwisho wa yote tukafanya mtihani wetu wa kumaliza kidato cha nne " huku tukisubiri matokeo bado tulikuwa tunaendeleza uhusiano wetu kwa njia ya simu kwa kuwa yuko home kwao .
Matokeo yalivyo toka japokuwa yalikuwa si mazuri kwa darasa zima ila yeye alifaulu kwenda A- level ila kwa upande wangu mimi sikufanikiwa ila nilipata daraja la 4 point 26 .
Maskini mimi akajiona yeye ndo yeye nikimpigia simu hapokei ila sivunjiki moyo akipokea anadai niko bizze labda baadae .Baadae nikimtafuta hapatkani Nimechanganyikiwa sijioni kama mwanadamu wa kawaida kwani siku moja kanitumia meseji inasema " Achana na mimi niko bize nasoma sitaki unipotezee muda kwani ninamalengo yagu" jamani imeniuma sana kwa nini amekuwa hivi amenifanya hadi siioni thamani ya maisha yangu ! Wana jf kuna maswali najiuliza ambalo ni Nifanyeje ili kukikomesha hiki kiburi chake na pia hivi Malengo yangu juu yake ndo yayeyuka hivi hivi .
Wakuu nifanye nini juu yake im serious juu ya hili ?
 
He he he he, tatizo la kudate kipanga afu wewe kilaza.

Huko kishakutana na fomu faivu mwenzie wanafundishana kwa mahaba, ila na huyo fomu faiv akifeli kwenda chuo atapigwa chini.

Cha kukushauri, nenda karisiti mtihani au kasome setifiketi yeyote ili uje kupambana na soko la ajira la afrika mashariki.

Sasa wee miaka 19, kula kulala kwa baba, utamsaidia nini Grace? Na mtihani umefeli? Unzurura mitaani, mwenzio anafokus na maisha ya mbele huku akila raha na wanafunzi wenzie. Unataka ale wa mtaani? (wewe ushakuwa wa mtaani)
 
Amekutumia akakudump, women use men too!

Wanasema "kisichoweza kukuua, kinakufanya uwe strong", ila mapenzi huja kwa aso kata tamaa. Take it positevely mapenzi yalikupotezea focus, sasa kwa kukuacha amekusaidia nawe jipange kwa maisha you are still a teeneger remember.
 
baada ya kupata daraja la 4 point 26 focus ya maisha yako iko wapi!!!.
Take the time that you need to evaluate &re evaluate your life
Bcoz you have a long way to go!!!!!!!!!!!!!!

she's in your past now so move on, there's a reason she didn't make it to the future.
 
Acha ujinga wewe tafuta njia mbadala ya kukusaidia maishani achana na huyo mtoto wa kike naye aconcetrate kwenye masomo yake!!! kama anakupenda atakutafuta tuu ukishanyoosha maisha yako!!! unachezea watoto wa kike wewe!! afterall she is right kukupiga chini maana utakuwa unampotezea muada wake wa masomo maana wewe sasa uko iddle mtaani so wewe unaishia kumuwaza na kumsumbua tuu!!! tia akili kumkichwa wewe
 
Bado wewe ni mtoto hayo mambo yamekuzidi umri hata nikikushauri bado hutaelewa kwa sababu wewe ni kilaza
 

ha ha ha makavu laivu!!!!!
 
Mdogo wangu nami nlikuwa na mawazo kama yako kpnd nkiwa fm4,kwamba huyu dada tutakuja oana baadae,ila kumbe haikuwa hvyo,maisha yanavyoendelea unajua meng zaid.Hebu fanya kitu fulani kwamba japokuwa nimefli ila ntamwonyesha kwamba i'm the best.Rudia,soma kwa nguvu zote had ufaulu,kama ni chuo kikuu ahad kwamba nawe utafka kama yeye anavyodai,Anza sasa achana na maumivu hasaidii ,songa mbele na elimu.
 
Badala ya kufikiria four yako ya point 26 itakupeleka wapi kimaisha na ukaanza kufikiria maisha yako zaidi bado unamuwaza Grace ambaye yuko shule sasa hivi anapambana kujiandalia maisha yake
Ningekuwa wewe muda huu ningekuwa nawaza niende wapi na hii four yangu nifanye nini kwa maisha yangu ya baadae sio kumuwaza Grace ambaye kwa sasa mambo yake yako super anaendelea na shule
Dogo wacha mambo ya ajabu bana hebu nenda kajiandalie maisha yako kwanza na huyo Grace atakuja kwako akisikia uko chuo fulani au unaendesha kampuni fulani hapo utawapata akina grace wengi
ila kwa sasa mkuu angalia life lako achana na mambo ya mapendi dogo
 

Nashkuru mkuu ngoja Nijipange kimasomo najua nutatoka tu!'
God help me
 

Mkuu nashkuru ila we ulirudia au chuo i'm confused nipe mbinu nzuri'
 
Nashkuru mkuu ngoja Nijipange kimasomo najua nutatoka tu!'
God help me


Hilo ndo la muhimu kufanya na achana na kumwazia mwanamke ambaye kwa sasa hana mpango na wewe
By the way wewe mdogo sana na wala huna ndoto za kuoa leo wala kesho ila la muhimu pambana na maisha yako jipange kujiendeleza au hata kurudia paper upate credit za kwenda chuo a level na au kujiendeleza chuo labla ya kufikiria na kujiumiza eti umeachwa na grace
 

Nashkuru mkuu nakiri kosa langu" ila Najipanga najua ntatoka tu
 

Samahani mi sio kilaza but ni mistakes tu so it might be happens even to u "!
naomba ushauri wako sio unaniponda hii siyo aim ya mimi kutupia hii thread!
kama huna (KEEP QUIT)
 
Mkuu nashkuru ila we ulirudia au chuo i'm confused nipe mbinu nzuri'

Hapana,mi ki uwezo wa shule nlikuwa nao,hvyo nlichana fm4 na six,hatimaye hadi shahada mkononi,wala cwaz tena kuhusu yule dada.Inawezekana mdogo wangu kaza buti.Amua leo kubadili msimamo na kuwa na hasira ya kitabu.Hasra ulionayo hamshia kwenye masomo sasa.
 

Nashkuru mkuu ngoja nipige kitabu
 

Shukrani kweli kutenda kosa sio kosa kosa ni kulirudia ! i believe i can make it ( i trust myself for now)
 
Hivi umri huo ulionao pamoja na elimu uliyonayo unaacha kabisa kufikiria maisha yatakuwaje mbeleni bila elimu, we unawazawa utaishije bila Grace.

Acha kabisa hayo mawazo, hebu anza kuitongoza elimu sasa, na umbwage Grace.. Ameshakutana na wa level yake huyo.
 

Thanks we mkali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…