My Impressions on JF Mods

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,280
Tahadhari: Hii thread si mahakama ya kuhukumu.Nia ya thread ni kuwatazama
na kuchambua watu muhimu kwenye huu mtandao wa JF.Wala thread haikaribishi
malalamiko juu ya utendaji wa mods wa jf.Hii thread ni mawazo yangu tu jinsi
ninavyowaona mods wa jf. Baada ya kusema hayo, tuanze.

Kwanza neno mod ni kifupi cha neno la kiingereza- moderator.
Kwenye forum zote za mitandaoni ni lazima kuwe na moderators.
Kazi za moderators kwenye forum ni nyingi ila za muhimu ni:
1. kuhakikisha wanaforum wanazingatia sera na kanuni/sheria za mtandao.
2.kuhakikisha michango/maandiko ya wanaforum inahusiana na mada/mjadala
uliowekwa mezani
3.kutoa msaada wa kiufundi pale wanaforum wanapokumbana na tatizo kwenye forum
kama vile kushindwa kuingia kwenye forum au kusahau nywila (password)
4. kuwashughulikia wote wanaoshindwa kukidhi namba 1 na 2 hapo juu.

Kwa hiyo mtindo wa kuweka mods si kitu kilichozuliwa na viongozi wa jf, ila ni
mahitaji muhimu.

Mods wa Jf.
Kwa harakaharaka mods wa jf ni hawa wafuatao:
Invisible
Moderator
Pruner
Innovator
Cookie
Fang
Paw
Mhariri
Majina ya mods
Labda kwa kupanga au kwa bahati tu, majina ya mods yanatoa
taswira fulani.
Invisible: mathlani ni neno la kiingereza lenye maana ya -siyeonekana.
Na kweli invisible avatar yake imejaa giza nene na macho yanayokonyeza
yanatoa taswira ya mnyama mkali anayejiandaa kukurukia gizani.

Moderator: kajitaja waziwazi yeye ni moderator.

Pruner: ni mnyambulisho (derivation) wa neno to prune.Maana yake kupunguza
matawi ya ziada ya mti au mmea wowote na pruner ni mtu anayepunguza
matawi ya ziada. Bila shaka analogy hii mpunguza matawi waweza kui-apply hapa jf

Innovator: ni mnyambulisho wa neno innovate lenye maana ya kubuni upya.Kwenye fani
ya teknolojia na ubunifu neno hili hutumika sana. Kwa hiyo innovator ni mtu anayebuni mapya.

Cookie: ni vile vitu vyenye asili ya unga ngano vinavyokaangwa au kuokwa.Simpati sana huyu
mod kwa kuchagua jina hili.

Fang: kwa kiingereza sahihi fang ina maana ya jino la nyoka mwenye sumu kali.
Kwa hiyo wanajf mjihadhari na huyu mod.
Paw: Hiki pia ni kiingereza chenye maana ya kiganja cha simba au chui.Wanyama hawa
hawa hutumia viganja vyao vyenye nguvu kubwa kuzaba wanyama wengine na kuwala.
Mwanajf, jihadhari na kiganja cha simba wa jf!

Mhariri: Huyu mod kajitangaza wazi; yeye ni mhariri wa jf.

Naomba thread hii isiwe uwanja wa kuwatolea maneno makali mods wa jf.
(naogopa sana ban wandugu) Thread ijayo ntatezama kazi za mamods mbalimbali.
(the way I see it)
Bye!
 
Hapo kwenye Cookie...umenifurahisha sana.

Cookie ni internet / web technical jargon. Inamaanisha data ambazo website au remote server inastore kwenye client's computer, more specifically the browser.

Data hizi zina matumizi mbalimbali kubwa ikiwa ni kumkumbuka user pale anapoaccess ile site hivo kuweza kubypass login procedures. Nadhani mnaona ile checkbox ya 'Keep me logged in'. Kuna matumizi mengine....lakini ni a form of memory about a user's activities on a website.
 
Asante mdau kwa kunifafanulia hilo. kwa hiyo alipochagua hilo jina alitaka watumiaji wa jf wamjue kwamba yeye si msahaulifu.
 
Ahaa... kumbe hawa ndo mods wa Jf. Hawa jamaa wanafuta uzi hata ikiwa nzuri. Ipo siku nitawalipa cash, na sio kwa instalment wasipojirekebisha mapema.
 
Ahaa... kumbe hawa ndo mods wa Jf. Hawa jamaa wanafuta uzi hata ikiwa nzuri. Ipo siku nitawalipa cash, na sio kwa instalment wasipojirekebisha mapema.
chifu77,thread ilitahadharisha tangu mwanzo juu ya mtazamo uliounesha kwenye bold.Uzi ukiwa mzuri ni mzuri kwa nani?
 
Last edited by a moderator:
chifu77,thread ilitahadharisha tangu mwanzo juu ya mtazamo uliounesha kwenye bold.Uzi ukiwa mzuri ni mzuri kwa nani?

Lahaula... kumbe cookie yupo karibu. Ila naskia huyu hana noma sana. Invisible ndo mnoko, hachelewi kupiga ban.
 
Last edited by a moderator:
halafu mimi huwa sielewi,kwani BAN ni nini ?
Tusaidiane kidogo wengine tunatumia Jf Mobile hivyo vingine hatuvioni.
 
halafu mimi huwa sielewi,kwani BAN ni nini ?
Tusaidiane kidogo wengine tunatumia Jf Mobile hivyo vingine hatuvioni.

Mkuu 'ban' ni rungu wanayotumia kukugongea endapo umekomenti kisicho kizuri kwao. Invisible usinipige ban, namwelewesha tu mwana Jf mwenzetu.
 
Mkuu 'ban' ni rungu wanayotumia kukugongea endapo umekomenti kisicho kizuri kwao. Invisible usinipige ban, namwelewesha tu mwana Jf mwenzetu.

sasa nitajuaje kama nishapigwa BAN kwenye comment yangu ?
 
Hivi hawa mod hakua mwenye jinsia tofauti na jinsia yangu?
cc Invisible
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…