My Eyes On Presidential Race 2015: Charles Julius Kambarage Nyerere Vs Dk Wilbrod Slaa

Makongoro apewe kazi ya U DC kwanza tumpime tuanzie pale

Wakati Dk Shein aliyekuwa Makamu wa Rais Wa Serikali Ya Jamuhuri ya Muungano na Sasa Rais Wa Serikali Ya Shirikisho Ya Mapinduzi Ya Zanzibar alikuwa DC wa Wapi vile?
 
muanzisha thread ana fantasies nyiiingi kichwani kwi kwi kwi kwi hatuwezi kuwa na utawala wa kiimla nchi hii riziwani yeye anapita mikoani kumpigia chapuo baba yake mdogo membe

Sasa wewe Kifinga definition ya neno Fantasies ujui mpaka kufikia kulitumia kwenye mchango wako huu....ningejua kazi ya Baba yako ningekwambia nani atairidhi kwenye familia yenu...kama si wewe..
Kama ni mzaliwa wa Tanzania basi misemo hii unaijua''Kama Baba Kama Mtoto'' au ''Mtoto wa Nyoka ni Nyoka'' au ''Tabia Ya Mtu Haina Dawa'', Ukipanda Mchicha Uvuni Bange'' Ukipanda Uadlifu Usitegemea wanao kuwa Manyangau.....nk.
 
Wakati Dk Shein aliyekuwa Makamu wa Rais Wa Serikali Ya Jamuhuri ya Muungano na Sasa Rais Wa Serikali Ya Shirikisho Ya Mapinduzi Ya Zanzibar alikuwa DC wa Wapi vile?



Ww kweli umetolewa kafara....Shein ni KIONGOZI...!!?

Do you know the meaning of a LEADER...!!? Shein hata hafai kabisa, the same to Makongoro wa gongo...hatuwataki watu kama Shein or Makongoro...
tena Makongoro is useless of all...

CCM ina viongozi wazuri sana tu...1: LOWASSA 2: Magufuli 3: Mwigulu 4: Wassira....kwa top 4 hao ndio atleast wanafaa...!!!
 
Nakushuru sana mkuu DSN kwa ufafanuzi wako wenye afya na kistaarabu bila kutumia lugha za kashafa wala matusi. Kwa kifupi nimependa approach yako ya kujibu hoja kwa kutumia hoja.

Kwa sehemu kubwa nimekubaliana na hoja yako ya kumpata kiongozi mwenye upeo,makini,mchapakazi,mzalendo wa kweli,mwenye maono na mwenye sifa za kiongozi badala ya mtawala.pia nakubaliana na uchambuzi wako kuhusu mifumo mbalimabli ya utawala na uendeshaji.

Kama watanzania wanaoitakia mema,ustawi,maendeleo endelevu kwa kizazi cha sasa na vinavyokuja nchi yetu, tunahitaji kufikiria kwa mapana na kujiuliza wapi tumeteleza na wapi tunahitaji kujirekebisha.kwa mtazamo wangu tanzania tunafanya vibaya kwa sababu zifuatazo:

1.mfumo wa vyama/chama kushika hatamu na ku dictate nyanja zote za uchumi, maendeleo na kiuchumi.mambo mengi yanafanyika zaidi kwa kuzingatia mlengo wa kichama bila kujali weledi na ushauri wa wataalam. Watu wa chama ndio wanamiliki kuanzia rais, mikoa,wilaya,halmashauri,idara,taasisi na vitengo vyote muhimu hata mabenki nk.matokeo yake maamuzi,mipango na utekezaji unakua kwa mlengo wa kichama na namna gani chama kitaendelea kushika hatamu za kutawala kwa gharama yoyote mifano mizuri tuliona mchakato wa katiba pendekezwa ulivyoeenda na hata maamuzi mengi yanayotolewa na serikali.

2.kupuuzwa na kutokutumika kwa wataalam mbalimbali kama wachumi,watafiti,na wanazuoni wenye weledi mkubwa kutuletea mabadiliko.hata ukiona wamewekwa katika nyanja mbalimbali hawapewi uhuru na uwezo wa kuzitumia taaluma zao wako pate kusikilizwa matakwa ya wanasiasa na wakijifanya wabisha wanawekwa sawa hata kuondolewa kwa visingizio mbalimbali.

Hakuna mfumo wa kuwalinda. Matokeo wataalamu wetu wanabaki frustrated na wengi hata watumishi wengi wa umma wanabaki kuchukua mishahara bila kutoa michango yao kikamilifu kwa sababu ya chama kushika hatam. Na wengine wanakimbia nchi za nje.

3.ugumu wa kumpata kiongozi mwadilifu na mzalendo wa kweli kwa kutumia mifumo ya vyama vilivyochafuka.kumbuka utaratibu wa kuchagua ndani ya vyama na rafu za makundi zinavyofanyika. Matokeo yake tumpata mtu ambaye ni chaguo la chama na sio chaguo la watanzania,zaidi ya hapo hata ndani ya chama anakuwa ni mwakilishi wa kundi dogo tu hivyo anaweza kuwa sio hata chaguo la chama bali ni chaguo la kundi fulani ndani ya chama.kwa mtazamo wangu mgombea binafsi angefaa sana katika eneo hili.

Nikirudi kwenye hoja ya msingi ni kuwa,mkuu DSN pamoja na kuwa nakubaliana na goja zako za kuwa na kiongozi mwenye nguvu,utashi, na mzalendo wa kweli lakini pia tunahita mfumo huru utakao mweka mbali na mashinikizo ya makundi hasimu ndani ya chama chake ili atakapoanza kuchukua maamuzi magumu asitishiwe.

Pia mkuu DSN lazima tukumbuke kuwa viongozi ni binadamu anaweza kuanza vizuri na kuonekana mwadilifu na mzalendo mwanzoni badae akakengeuka tukaanza kushangaa,utakumbuka ya mkapa awamu ya kwanza na ya pili pia rais Clinton wa marekani na issue ya monica Lewinsky. Hivyo mtazamo wangu lazima kuwepo na mfumo wa kuwalinda na kuwapa uhuru viongozi wazalendo wanapotekeza majukumu yao bila kuingiliwa na makundi yenye nguvu ndani ya vyama vyao, pia mfumo wa kuwawekea wigo wasikengeuke na kama wakikengeuka kuwepo utaratibu wa kuwaadibisha badala ya mfumo wa sasa ambapo viongozi wa africa akichaguliwa anakuwa kama mungu mtu angalia nkurunziza na wengine.

Well Hakika Uyasemayo Nsinsi
 
Ww kweli umetolewa kafara....Shein ni KIONGOZI...!!?

Do you know the meaning of a LEADER...!!? Shein hata hafai kabisa, the same to Makongoro wa gongo...hatuwataki watu kama Shein or Makongoro...
tena Makongoro is useless of all...

CCM ina viongozi wazuri sana tu...1: LOWASSA 2: Magufuli 3: Mwigulu 4: Wassira....kwa top 4 hao ndio atleast wanafaa...!!!

Unatumia avatar yenye maana nzuri sana, lakini michango yako humu JF haiendani na avatar yako...wala ufahamu wa mtu aliyepaswa kuitwa Mr Prsident japo ata wa Kampuni ya Wasafi Wa Tandale Kwa Mfuga Mbwa.

Ehehe leo unae mnadi ndio umekumbuka shuka kumekucha baada ya kugundua shuka kumekucha kuwa umechangia kumwaribia kwa kustrategize kwenye kila thread hata isiyo muhusu muhusika. Leo unamtafutia substitute wake ungeanza mapema tungeona unamtakia mema chaguo lako na kumpa haki yake technically na wewe haki yako technically ya kuchaguliwa na kumchagua yoyote yule ili mradi sheria za Nchi na taasisi husika azivunjwi....Siwezi kusema uliowataja kweye tamko lako kuwa ni USELESS ... kwa kuwa hakuna Mwanadamu aliezaliwa Duniani na mwandamu is useless kwa kuwa kila mja Mungu anamakusidio nae hapa Duniani, sembuse mtu toka kizazi cha Baba Wa Taifa, tena aliyesoma na kutumikia Taifa ngazi mbali mbali....Inaonyesha ni jinsi gani ulivyo MUHUNI na USTAHIKI hata KUJIBIWA nimeamua kukujibu hivi li wenye ufahamu humu ndani watatambue PUMBA na MCHELE.

Uliowataja wenyewe na mapungufu yao baadhi kamwe siwezi kuwaita USELESS kwa mwenye ufahamu hata kuliwazia neno useless alipo kichwani kwa kuwa aliwazalo mpumbavu ndio limtokealo.Naweza kuwa sishawishiki na baadhi ya Watanzania baadhi yao uliowataja lakini KIHAKI sipaswi kuwaona ni USELESS eti kwa kuwa nina chaguo langu ambalo kwa mtizamo wangu na si kuwa ni maono ya umma mzima wa Watanzania naona anafaha nilazimishe kuwa ANAFAHA kwa Watanzania wote.Ila kama n busara katika michango mbalimbali nichangia na kutetea kile ninachooamini kuwa ni sahihi na kuonyesha kwa hoja kwanini ni sahihi.

Sasa hizi habari za Shein HAFAI, Makongoro ni USELESS , uoni kuwa unamtukana na kuwatukana hao ambao kwa sasa UMEAMUA kuwaingiza kuwa SUBSTITUTE wa chaguo lako..The Real President Shein ni mmoja wa watu makini sana walipata kuserve TAIFA la TANZANIA kwa muda mlefu sana kuliko viongozi walio wengi sana Nchini.Siri yake nini?Kutoka asiko julikana na leo hii kawa kwenye majengo ya IKULU za Wananchi muda mrefu...ebu tafakari...na badilika umtendee chaguo lako HAKI na kumfanya aonekane nae ni Kiongozi Muungwana, manake kama wewe ni SUPPOTER na atitude yako ndio hii ndani ya JF basi ndio kusema ''SHOW ME YOUR FRIENDS AND I WILL TELL YOU WHO YOUR'' and ''BIRDS OF THE SAME FEATHER FLOCK TOGETHER''
 
Sasa wewe Kifinga definition ya neno Fantasies ujui mpaka kufikia kulitumia kwenye mchango wako huu....ningejua kazi ya Baba yako ningekwambia nani atairidhi kwenye familia yenu...kama si wewe..
Kama ni mzaliwa wa Tanzania basi misemo hii unaijua''Kama Baba Kama Mtoto'' au ''Mtoto wa Nyoka ni Nyoka'' au ''Tabia Ya Mtu Haina Dawa'', Ukipanda Mchicha Uvuni Bange'' Ukipanda Uadlifu Usitegemea wanao kuwa Manyangau.....nk.

baba yangu ni one of the senior members wa tanzania peoples defence forces lakini mimi nimesoma na nafanya kazi nyingine kabisa na sikutaka kuingia jeshi japokua hata leo hii nikitaka kuingia naingia kwani ni kimemo tu kikitumwa nakula shavu lakini nimeamua kuwaachia nafasi hiyo watu wengine mimi niko zangu uraiani
 
Neno Kuota Kwa Lugha ya wenzetu ndio uwa Dreams...basi kupitia msemo wao Dreams Comes True inatokea kweli!!![/QUOTE]
nnachotaka kukwambia huyo ndugu yako membe hatoboi membe hawezi kuwa raisi nchii hata siku moja mzee wangu yuko kwenye system huwa ananiambia membe anajisumbua tu
 
Binafsi mimi si shabiki wala Mwanachama Wa Chama Chochote cha kisiasa, lakini swala la siasa linanihusu kwa kuwa SIASA ni sehemu ya maisha yangu kama ilivyo kwa Mwananchi yoyote yule aliye raia wa Tanzania.Kwa kuwa katiba ya Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania 1977 inatoa fursa ya kila raia kushiriki katika harakati za uchaguzi wa viongozi wake, iwe ni kwa yeye kuchaguliwa kuongoza watanzania wenzie ngazi yoyote ile ama yeye kuchagua kiongozi wa kumuongoza yeye mchaguaji katika ngazi yoyote ile.

Katika hatua tuliyonayo sasa binafsi natamani kuona mbio za uchaguzi wa mwaka huu 2015 katika nafasi ya Urais iwe ni kati ya Mwanaccm Kwa Jina la Charles Julius Kambarage Nyerere [CJ] dhidi ya Mwanachadema ambae pia ni Mwanaukawa DK Wilbrod Slaa [WS] nafasi ya juu ya uongozi kwa Taifa zikiwa na sura ya wafuatao kama endapo watajitokeza kuomba na wao kupewa baraka na vyama vyao kuwa na dhamana ya kichama na kupewa kukimbiza mbio za vijiti vya URAIS WA TANZANIA toka kizazi kimoja kwenda kingine.

Ukiacha makando kando ya maswala binafsi watajwa wana sifa bora na toshelezi za kuongoza Taifa kwa kiwango chenye utoshelezi wa kusimamia maono [Vision] yao dhidi ya kile wanacho kiamini bila kuyumba.

Sifa nzuri ya Rais bora ni uwezo wa kusikiliza wengi na kuchambua mawazo mengi aliyosikia na kuibuka yeye binafsi na wazo bunifu toka kwenye shauri tolewa na kutoa jibu sahihi kwa wakati huo na kusonga mbele kwa hatua nyingine.

Ukibisha Waangalie Charles Na Slaa Nyuso Zao,kisha kumbuka wosia wa Baba wa Taifa kwamba tukikuangalia usoni tuseme huyu nae....akimaanisha kuwa kile unachokitetea na kukisema tunaweza kukisoma kwenye sura ya msemaji na wapokeaje wakaamini bila wasiwasi kuwa yasemwayo na msemaji wako pamoja nae kuyasema na kuyatete popote pale.

Charles na Slaa ni aina ya watu wenye HAIBA ya kuweza kusema hili ni Koleo na sio kuwa Koleo ni Kijiko Kikubwa.Taifa liko katika hatua [Stage] ambayo Watanzania wamepata mwamko kiasi wa Kidemokrasia na sasa wanapaswa kupata fursa ya mwamko na mafanikio ya Kiuchumi yanayoendana na ustawi wa maisha bora kwa kila Mwananchi mmoja mmoja na hatimae kwa Taifa.

Ukiacha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, viongozi wengine waliofuata baada yake walijenga uchumi wa kitanzania kutoka juu kuja chini.Hii ni sawa na kusema waliangalia uchumi wa uwekezaji wenye kuangalia multi nations companies na matajiri wawekezaji wa ndani kuja kuinvest Nchini na kutoa fursa ya wakubwa hao toka juu kuwa na hati milki ya uchumi.Kwa style hiyo uchumi mkubwa wa Taifa ukamea mikononi mwa aina fulani ya kundi la Wafanyabiashara wa ndani na wa nje, na baadhi yao wakishirikiana na Viongozi waliopata fursa kupitia siasa iliyo wawezesha kupata mitaji.

Kwa kuwa hapa tulipo ni majibu ya matokeo au mazao ya mambo makuu mawili makubwa kutokea kwa wakati mmoja yani Mageuzi ya Siasa [East & West Politics /Cold War] na Uchumi [The Comming of Globalization] Duniani. Hayo yakitokea Taifa kama Taifa halikuwa limejiandaa kwa mageuzi hayo. Yani Taifa linabadilisha utawala [Administration] kutoka kwa muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, huku akiwa na maono ambayo kwa nyakati hizo yalikuwa yanakinzana na baadhi ya siasa za kimataifa, siasa ambazo Muasisi wa Taifa akiamini katika siasa za UJAMAA WA KIAFRIKA, lakini changamoto zilizo mbele ya Rais mpokea kijiti ni siasa zinazosukuma Taifa na Mataifa mengi Duniani kuegemea siasa za Uchumi wa Soko huru [Tafsiri Ruksa] .

Ni kwa siasa hizo ambazo Taifa kwa umri wake na msimamo wa mjenzi wa kwanza wa Msingi wa Taifa viliibua changamoto kubwa sana kisiasa na uchumi kiasi kuwa hata ulipofika muda kuwa Taifa liingie kwenye mfumo wa vyama vingi [Multi-Partism] asilimia karibia 80% walisema hapana Taifa lisiingie Kwenye vyama vingi.Lakini kwa maono ya muasisi wa Taifa alitoa ushauri kwa Taifa kuwasikiliza asilimia 20% na leo tuko hapa.

Changamoto zote tulizopita kama Taifa ambazo pia zilipelekea baadhi ya viongozi wetu kuhalalisha kutekeleza mageuzi ya Kisiasa na Uchumi [Polical & Economic Justification] kwa namna ambayo wao waamuaji waliona inafaa ama kuzingatia au kutozingatia maslahi ya Taifa kwa ujumla wake. Ni kwa baadhi ya maamuzi hayo ambayo mengine yalitendwa kwa kutozingatia misingi iiyowekwa na MUASISI [FOUNDER] basi Taifa limepita kwenye misukosuko ya Kisiasa na Kiuchumi ambayo walio wengi wana matamanio ya kuona Watanzania wote wakiwa wamepiga hatua kimaisha kama ambavyo walifundishwa wakiwa chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa kupitia juhudi zao kwa pamoja wapige vita maadui wakuu wa Taifa ili wajiletee maendeleo yao wenyewe.

Tulipofika kama Taifa kumepatikana maendele ya vitu [Material things] kutoka tulipo Taifa laitaji Kiongozi atakewekeza kwenye utawala utakao simamia na kutoa USTAWI wa Taifa [Standard of Living] toka ngazi ya mtu mmoja kwenda kwenda ngazi ya Taifa kwa ujumla wake.Hii ni kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, jamii, kikundi cha watu na kwa ujumla wake kama Taifa zima.Ni muda ambao Taifa linaitaji aina ya kiongozi atakae zingatia uchumi wa kutoka chini kwenda juu.Uchumi ambao unampa fursa raia wa kawaida Mtanzania kushiriki kwenye ujenzi wa Uchumi wa Taifa lake kwa kuzingatia vigezo vya HAKI na fursa zenye viwezesho na vinavyo kidhi vigezo stahiki na ufanisi wenye kuhesabika kwa kila mmoja.

Ustawi wa mtu mmoja mmoja [Standard of Livingi ] hauwezi kupatikana kama Taifa halina MISINGI YA HAKI NA MIIKO....ustawi wa Taifa kwa kukosa hayo upoteza UWAJIBIKAJI, RUSHWA NA UFISADI, USHAMILI, MAOVU USTAWI, MAADILI UPOTEA, UZALENDO UPATA NAJISI, CHUKI NA UONGO USTAWI, HUDUMA UGEUKA KUWA HISANI, UCHOYO NA UBINAFSI UPATA KIBALI NA KUSTAWI, HOFU YA MUNGU UTOWEKA, UZEMBE NA UVIVU UTAMALAKI, MALALAMIKO NA MIGOGOLO ISIYOKWISHA UPATA HIFADHI NDANI YA JAMII, USALAMA NA AMANI UGEUKA KUOMBWA BADALA YA KUWA NI TABIA MIOYONI MWA WANANCHI, HESHIMA NA UNDUGU WA KIAFRIKA UPOTEZA MWELEKO, KIBULI NA MAJIVUNO UJENGA MASKANI KWENYE OFISI NA MAJUMBANI,

Hayo na mengineyo tajwa yanaitaji mtu mwenye JICHO la ndani asiye na mawaa bali ukimuona USONI unakili moyoni kuwa huyu akisema RUSHWA HAIPENDI basi kweli Rushwa inatoweka haraka.

Kwa miongo mitatu 3 [3 decade] sisi kama Taifa tulifundishwa na watawala kuendesha maisha yetu kiuchumi tukiwa tumezingatia sana uchumi wa soko huru [Free Market] -chini ya kivuli cha uwekezaji. Sasa ni muda mwafaka na tosha sana kama Taifa kuachana na Uchumi wa majaribio na kujikita kwenye fursa ya uchumi inayozingatia namna gani Mtanzania atastawi yeye na familia yake kwa kupitia maliasili alizo nazo Mtanzania.Rais ajae awe ni Rais anae kerwa na mfumo wa maisha ya mlo wa Mtanzania, afya yake, Kazi zake, Elimu yake, Makazi yake, na kwa kero hizo awe na kiu ya kubolesha maisha yao kwa kiwango ambacho Mtanzania akilinganishwa na Mataifa mengine Afrika basi awe ni namba moja na Taifa la kuigwa kuwa Tumewezaje.Kinachostawisha maisha ya watu ni SERA [POLICY] huku sera hizo zikiwa na usimamizi thabiti toka juu mpaka ngazi ya chini ya uongozi.Usimamizi wa sera zisizo zaa madaraja wala dhuruma dhidi ya mwingine bali utoaji wa fursa zenye mazingira ya kumwinua Mtanzania ngazi yoyote ile toka Mkulima wa Kilosa Morogoro mpaka Mmachinga wa Kariakoo Dar es Salaam.

Kama kwa CCM Charles hatojitokeza basi wafuatao wanaweza kidogo kusimama nyuma yake..
1: Magufuri 2: Benard Membe 3: Steven Wasira

Kwa Ukawa Vs Chadema
1: Aikael P Mbowe 2: Ibrahim Lipumba -ingawa anamezwa na tulivyojingea watanzania.

Ni Mtizamo..Tu...Get Ready
Wewe ni mwana mitazamo bora..hatimaye mtazamo wako ukatimia na mmoja hapo ni Rais wa nyumbani kwao sasa!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom