My Eyes On Presidential Race 2015: Charles Julius Kambarage Nyerere Vs Dk Wilbrod Slaa

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Binafsi mimi si shabiki wala Mwanachama Wa Chama Chochote cha kisiasa, lakini swala la siasa linanihusu kwa kuwa SIASA ni sehemu ya maisha yangu kama ilivyo kwa Mwananchi yoyote yule aliye raia wa Tanzania.Kwa kuwa katiba ya Jamhuri Ya Muungano Ya Tanzania 1977 inatoa fursa ya kila raia kushiriki katika harakati za uchaguzi wa viongozi wake, iwe ni kwa yeye kuchaguliwa kuongoza watanzania wenzie ngazi yoyote ile ama yeye kuchagua kiongozi wa kumuongoza yeye mchaguaji katika ngazi yoyote ile.

Katika hatua tuliyonayo sasa binafsi natamani kuona mbio za uchaguzi wa mwaka huu 2015 katika nafasi ya Urais iwe ni kati ya Mwanaccm Kwa Jina la Charles Julius Kambarage Nyerere [CJ] dhidi ya Mwanachadema ambae pia ni Mwanaukawa DK Wilbrod Slaa [WS] nafasi ya juu ya uongozi kwa Taifa zikiwa na sura ya wafuatao kama endapo watajitokeza kuomba na wao kupewa baraka na vyama vyao kuwa na dhamana ya kichama na kupewa kukimbiza mbio za vijiti vya URAIS WA TANZANIA toka kizazi kimoja kwenda kingine.

Ukiacha makando kando ya maswala binafsi watajwa wana sifa bora na toshelezi za kuongoza Taifa kwa kiwango chenye utoshelezi wa kusimamia maono [Vision] yao dhidi ya kile wanacho kiamini bila kuyumba.

Sifa nzuri ya Rais bora ni uwezo wa kusikiliza wengi na kuchambua mawazo mengi aliyosikia na kuibuka yeye binafsi na wazo bunifu toka kwenye shauri tolewa na kutoa jibu sahihi kwa wakati huo na kusonga mbele kwa hatua nyingine.

Ukibisha Waangalie Charles Na Slaa Nyuso Zao,kisha kumbuka wosia wa Baba wa Taifa kwamba tukikuangalia usoni tuseme huyu nae....akimaanisha kuwa kile unachokitetea na kukisema tunaweza kukisoma kwenye sura ya msemaji na wapokeaje wakaamini bila wasiwasi kuwa yasemwayo na msemaji wako pamoja nae kuyasema na kuyatete popote pale.

Charles na Slaa ni aina ya watu wenye HAIBA ya kuweza kusema hili ni Koleo na sio kuwa Koleo ni Kijiko Kikubwa.Taifa liko katika hatua [Stage] ambayo Watanzania wamepata mwamko kiasi wa Kidemokrasia na sasa wanapaswa kupata fursa ya mwamko na mafanikio ya Kiuchumi yanayoendana na ustawi wa maisha bora kwa kila Mwananchi mmoja mmoja na hatimae kwa Taifa.

Ukiacha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, viongozi wengine waliofuata baada yake walijenga uchumi wa kitanzania kutoka juu kuja chini.Hii ni sawa na kusema waliangalia uchumi wa uwekezaji wenye kuangalia multi nations companies na matajiri wawekezaji wa ndani kuja kuinvest Nchini na kutoa fursa ya wakubwa hao toka juu kuwa na hati milki ya uchumi.Kwa style hiyo uchumi mkubwa wa Taifa ukamea mikononi mwa aina fulani ya kundi la Wafanyabiashara wa ndani na wa nje, na baadhi yao wakishirikiana na Viongozi waliopata fursa kupitia siasa iliyo wawezesha kupata mitaji.

Kwa kuwa hapa tulipo ni majibu ya matokeo au mazao ya mambo makuu mawili makubwa kutokea kwa wakati mmoja yani Mageuzi ya Siasa [East & West Politics /Cold War] na Uchumi [The Comming of Globalization] Duniani. Hayo yakitokea Taifa kama Taifa halikuwa limejiandaa kwa mageuzi hayo. Yani Taifa linabadilisha utawala [Administration] kutoka kwa muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, huku akiwa na maono ambayo kwa nyakati hizo yalikuwa yanakinzana na baadhi ya siasa za kimataifa, siasa ambazo Muasisi wa Taifa akiamini katika siasa za UJAMAA WA KIAFRIKA, lakini changamoto zilizo mbele ya Rais mpokea kijiti ni siasa zinazosukuma Taifa na Mataifa mengi Duniani kuegemea siasa za Uchumi wa Soko huru [Tafsiri Ruksa] .

Ni kwa siasa hizo ambazo Taifa kwa umri wake na msimamo wa mjenzi wa kwanza wa Msingi wa Taifa viliibua changamoto kubwa sana kisiasa na uchumi kiasi kuwa hata ulipofika muda kuwa Taifa liingie kwenye mfumo wa vyama vingi [Multi-Partism] asilimia karibia 80% walisema hapana Taifa lisiingie Kwenye vyama vingi.Lakini kwa maono ya muasisi wa Taifa alitoa ushauri kwa Taifa kuwasikiliza asilimia 20% na leo tuko hapa.

Changamoto zote tulizopita kama Taifa ambazo pia zilipelekea baadhi ya viongozi wetu kuhalalisha kutekeleza mageuzi ya Kisiasa na Uchumi [Polical & Economic Justification] kwa namna ambayo wao waamuaji waliona inafaa ama kuzingatia au kutozingatia maslahi ya Taifa kwa ujumla wake. Ni kwa baadhi ya maamuzi hayo ambayo mengine yalitendwa kwa kutozingatia misingi iiyowekwa na MUASISI [FOUNDER] basi Taifa limepita kwenye misukosuko ya Kisiasa na Kiuchumi ambayo walio wengi wana matamanio ya kuona Watanzania wote wakiwa wamepiga hatua kimaisha kama ambavyo walifundishwa wakiwa chini ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa kupitia juhudi zao kwa pamoja wapige vita maadui wakuu wa Taifa ili wajiletee maendeleo yao wenyewe.

Tulipofika kama Taifa kumepatikana maendele ya vitu [Material things] kutoka tulipo Taifa laitaji Kiongozi atakewekeza kwenye utawala utakao simamia na kutoa USTAWI wa Taifa [Standard of Living] toka ngazi ya mtu mmoja kwenda kwenda ngazi ya Taifa kwa ujumla wake.Hii ni kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, jamii, kikundi cha watu na kwa ujumla wake kama Taifa zima.Ni muda ambao Taifa linaitaji aina ya kiongozi atakae zingatia uchumi wa kutoka chini kwenda juu.Uchumi ambao unampa fursa raia wa kawaida Mtanzania kushiriki kwenye ujenzi wa Uchumi wa Taifa lake kwa kuzingatia vigezo vya HAKI na fursa zenye viwezesho na vinavyo kidhi vigezo stahiki na ufanisi wenye kuhesabika kwa kila mmoja.

Ustawi wa mtu mmoja mmoja [Standard of Livingi ] hauwezi kupatikana kama Taifa halina MISINGI YA HAKI NA MIIKO....ustawi wa Taifa kwa kukosa hayo upoteza UWAJIBIKAJI, RUSHWA NA UFISADI, USHAMILI, MAOVU USTAWI, MAADILI UPOTEA, UZALENDO UPATA NAJISI, CHUKI NA UONGO USTAWI, HUDUMA UGEUKA KUWA HISANI, UCHOYO NA UBINAFSI UPATA KIBALI NA KUSTAWI, HOFU YA MUNGU UTOWEKA, UZEMBE NA UVIVU UTAMALAKI, MALALAMIKO NA MIGOGOLO ISIYOKWISHA UPATA HIFADHI NDANI YA JAMII, USALAMA NA AMANI UGEUKA KUOMBWA BADALA YA KUWA NI TABIA MIOYONI MWA WANANCHI, HESHIMA NA UNDUGU WA KIAFRIKA UPOTEZA MWELEKO, KIBULI NA MAJIVUNO UJENGA MASKANI KWENYE OFISI NA MAJUMBANI,

Hayo na mengineyo tajwa yanaitaji mtu mwenye JICHO la ndani asiye na mawaa bali ukimuona USONI unakili moyoni kuwa huyu akisema RUSHWA HAIPENDI basi kweli Rushwa inatoweka haraka.

Kwa miongo mitatu 3 [3 decade] sisi kama Taifa tulifundishwa na watawala kuendesha maisha yetu kiuchumi tukiwa tumezingatia sana uchumi wa soko huru [Free Market] -chini ya kivuli cha uwekezaji. Sasa ni muda mwafaka na tosha sana kama Taifa kuachana na Uchumi wa majaribio na kujikita kwenye fursa ya uchumi inayozingatia namna gani Mtanzania atastawi yeye na familia yake kwa kupitia maliasili alizo nazo Mtanzania.Rais ajae awe ni Rais anae kerwa na mfumo wa maisha ya mlo wa Mtanzania, afya yake, Kazi zake, Elimu yake, Makazi yake, na kwa kero hizo awe na kiu ya kubolesha maisha yao kwa kiwango ambacho Mtanzania akilinganishwa na Mataifa mengine Afrika basi awe ni namba moja na Taifa la kuigwa kuwa Tumewezaje.Kinachostawisha maisha ya watu ni SERA [POLICY] huku sera hizo zikiwa na usimamizi thabiti toka juu mpaka ngazi ya chini ya uongozi.Usimamizi wa sera zisizo zaa madaraja wala dhuruma dhidi ya mwingine bali utoaji wa fursa zenye mazingira ya kumwinua Mtanzania ngazi yoyote ile toka Mkulima wa Kilosa Morogoro mpaka Mmachinga wa Kariakoo Dar es Salaam.

Kama kwa CCM Charles hatojitokeza basi wafuatao wanaweza kidogo kusimama nyuma yake..
1: Magufuri 2: Benard Membe 3: Steven Wasira

Kwa Ukawa Vs Chadema
1: Aikael P Mbowe 2: Ibrahim Lipumba -ingawa anamezwa na tulivyojingea watanzania.

Ni Mtizamo..Tu...Get Ready
 
Edga Lungu "EL" unabifu nae

Ukisema Edga Lungu unamaanisha nini na hapo ukasema EL ungetumia EL pekee ningejua unasema nini...Lakini ni sawa na kusema PANGA kisha ukusema kwa hakika nini?

Ungesema PANGA ukasema kifaa au tendo basi ingekuwa na maana njema...be specific na hiyo EL kama ni Tanzania au Zambia.Uliposemaa Edga Lungu umepoteza maana halisi ambayo ulitaka kuifikisha.
 
Ndugu waweza kuwa na hoja lakini hebu tufafanulie kiasi ili tuufahamu utumishi uliotukuka wa Ndugu Charles Makongoro Nyerere unaompa sifa za kuwa Rais wetu.

Mbali ya ule ubunge wa muda mfupi wa Arusha mjini 1995 ambapo tuelezwe aliacha legacy gani ya kukumbukwa huko Arusha....vilevile ubunge wake wa Afrika ya Mashariki amefanya nini kuitetea Tanzania zaidi ya ukimya usio na maana
Urais sio ufalme wala usultani kwamba watoto warithishwe kwa kuwa tu ana jina la Nyerere...tutamchagua iwapo ana sifa na sio kwa kuwa ni Nyerere...tukumbuke ule msemo wa Wazungu kwa kuwa baba yako ni Profesa haina maana ya kuwa na wewe ni Profesa ama waweza ondoa ujinga kichwani mwako
Au mnataka kuleta kama ya Moi 2002 huko Kenya aliemleta inexperienced Uhuru Kenyatta agombee urais kwa tiketi ya KANU just kwa kuwa alikuwa ni mtoto wa Kenyatta?

Poor analysis......
 
Magufuli hafai aligawa nyumba zetu hadi kwa hawara zake cio ufisadi huo? Membe fedha za Gadaf ziko wapi? Wasira toka awamu kwanza ni waziri ni impact at all.
 
Huyo Nyerere si ameshindwa hata uenyekiti wa ccm mkoa?
Labda ccm wasurrende na Slaa kupita bila kupingwa!
 
late dr mvungi aliwai sema nyerere alikuwa na akili sana ila matoto yake hovyo. alisema hakuna mtoto mwenye akili ya kufanya yale baba yao aliyofanya. over!
 
Ndugu waweza kuwa na hoja lakini hebu tufafanulie kiasi ili tuufahamu utumishi uliotukuka wa Ndugu Charles Makongoro Nyerere unaompa sifa za kuwa Rais wetu.

Mbali ya ule ubunge wa muda mfupi wa Arusha mjini 1995 ambapo tuelezwe aliacha legacy gani ya kukumbukwa huko Arusha....vilevile ubunge wake wa Afrika ya Mashariki amefanya nini kuitetea Tanzania zaidi ya ukimya usio na maana
Urais sio ufalme wala usultani kwamba watoto warithishwe kwa kuwa tu ana jina la Nyerere...tutamchagua iwapo ana sifa na sio kwa kuwa ni Nyerere...tukumbuke ule msemo wa Wazungu kwa kuwa baba yako ni Profesa haina maana ya kuwa na wewe ni Profesa ama waweza ondoa ujinga kichwani mwako
Au mnataka kuleta kama ya Moi 2002 huko Kenya aliemleta inexperienced Uhuru Kenyatta agombee urais kwa tiketi ya KANU just kwa kuwa alikuwa ni mtoto wa Kenyatta?

Poor analysis......
Aksante Its Poor Analysis nilitegemea usichangie thread kwa kuwa POOR na RICH avifungamani...Sasa nashangaa a RICH analyst anachangia kwenye Poor Analysis...tayari umenionyesha kuwa una yako uliyotegemea kuyakuta kwenye thread hii ulipo yakosa kwa hamaki ukachangia kwa msisimko wa mtu aliyeghafilika.Anyway kwa kuwa ni Mtanzania mwenzangu nitakujibu hoja yako nyepesi kama ifuatavyo.

Unaomba legacy.... natumia kamusi ya kingereza kukuonyesha kuwa Charles bado yuko safarini kwa kuwa ajafika safari yake ya kuwa Mkongwe [Legendary ] kiasi kuwa awekwe kwenye kundi la kuwa na kumbukumbu ya kumfuata nyuma yake kama ushuhuda wa utendaji wake uliotukuka kwenye sekta husika.[Legacy].

Hivyo utumiaji wako wa neno utumishi uliotukuka na legacy unaonyesha kuwa ujui hata matumizi yake yana maana gani?Naomba Kukupa kwanza maana za maneno yako hayo...Utumishi uliotukuka [Stateman] na Ulithi Wa Utumishi [legacy].

MAANA YA UTUMISHI ULIOTUKUKA.[STATEMAN].
Maana ya Utumishi uliotukuka [Stateman]
1: A is an important and experienced politician, especially one who is widely known and respected.

Mtu anapotajwa kuwa ana utumishi uliotukuka ni utumishi ambao mtu huyu ameitumikia jamii yaje kwenye sekta husika iwe ni Kisiasa ama Serikalini na hata sekta binafsi kwa muda mlefu na hivyo kuwa uzoefu wake wa miongo kadha wa kadha jamii imefaidika na utumishi wake kwenye eneo husika kwa kiasi kuwa hauna mashaka nae.Ndio kusema kwa utumishi huo ambao umepelekea Muhusika kuitwa Mtumishi aliyetukuka ni kiwango kikubwa cha maisha yake kuwa kimetumika na kughalimika kuitumikia Jamii yake kwenye nyanja moja au kadha kadha kama Mtumishi wa Umma unaomzunguka kwa muda mlefu sana na wakati mwingine maisha yake yote mpaka kufikia dalaja la kustaafu kwenye utumishi na pia uenda pia Mtumishi akaendelea kutumika akiwa nje ya utumishi [Serikalini na Kisiasa kwa jinsi tunavyo tafsiri kibongo] huo wa umma kwa muhusika kutumika akiwa sekta binafsi ama nje ya mfumo lasmi [Formal Sector].

Mfano wa baadhi ya watumishi waliotukuka ni kama
1: Judge Joseph Sinde Warioba.
2: Stateman Salim Ahmed Salim
3: Balozi Paulo Rupia
4: Stateman John Malechela

Na wengineo wengi kutajwa...uwezavyo...Hivyo kumuweka Charles kwenye kundi tajwa hapo juu ni kumuonea.Kama ataomba na kupewa kibali hicho, basi miongo atakayo tumika akiwa kwenye dhamana hiyo ndio atapata dhamana ya kuvaa cheo hicho cha heshima kwenye jamii.Na uenda siku za mbele kwa kiwango chake kahesabiwa kwenye kundi la kuacha ulithi wa utumishi [Legacy].

ULITHI WA UTUMISHI [LEGACY ]
Maana ya neno legacy kwa Tafisri ya Kingereza .
1: A an event or period of history is something which is a direct result of it and which continues to exist after it is over.
2: A is money or property which someone leaves to you when they die.

Ndio kusema ndugu Charles bado yuko hai hivyo kundi hili hayumo na kwa Tanzania watu walio kundi la kuacha Ulithi wa Utumishi ni kama kina
1: Mtemi Mirambo na Chifu Mkwawa
2: Father Of The Nation Julius Kambarage Nyerere
3: Dk John T Williamson [Sekta ya Madini Tanzania].
Na wengineo wengi kutajwa pia.

Nikiludi kwenye hoja yako ya swala la uzoefu sasa. Kukujibu nikizingatia [Assume] kuwa sikukupa ufahamu wa maneno tajwa hapo juu nikalejea utetezi wa vijiwe vya kahawa na si ufahamu wa kishule ni kama ifuatavyo...

A; KIMFUMO [SYSTEM]

Kuna Watanzania wameingia kwenye utumishi wa umma na jamii ya Watanzania hawakujua hata waliko tokea lakini leo hii wamefanya kazi kubwa na utumishi wao umekuwa bora kuliko wale walio lelewa na kukulia kwenye utendaji wa Serikalini na kwenye majukwa ya siasa.Mfano...

1: Wakati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anachukua Nchi ya Tanganyika [1961] hakuwa na uzoefu wowote wa kiungozi zaidi ya kuwa na uzoefu Elimu yake, Ualimu wake toka Pugu Sekondari na Uongozi wa Chama cha TAA, TANU ambao kwa leo hii DK Slaa na Mh Mbowe wana uzoefu Mkubwa sana sana kuzidi Mwalimu Nyerere, kujua na kujifunza kuongoza Nchi wakiwa na uzoefu nje ya mfumo rasmi wa Kiserikali.Ukienda kwa Lipumba yeye ndio ana maradufu kwa kuwa yeye alikwisha onja japo kuwa mtaalamu kushauri maswala ya uchumi Serikali hivyo kuwa na ufahamu wa mengi.

2: Wakati Ambassador & Stateman Salim Ahmed Salim anachaguliwa kuwa balozi kitu kama Nchi ya Misri [Akiwa na Umri wa miaka 21] alikuwa mdogo sana na hakuwa na uzoefu wowote wa kidplomasia kuweza kusema siwezi lakini leo ni Mtumishi wa Taifa na Kimataifa aliyetukuka.

2: Wakati Karume Junior anachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar sitegemei unambie alikuwa na uzoefu wowote wenye vigezo vilivyosababisha aonekane hana uzoefu wa kuongoza.Lakini aliiingia akatumika na leo hii ashatimiza yake.Na hata Karume Senior naye zaidi ya kuwa na uzoefu kama Baharia hakuwa na cha zaidi kusema amejifunza na hivyo kuwa na uzoefu bali uzoefu wake ni akili yake na ufahamu wake kuhusu kuongoza.

3: Wakati Mkapa anachaguliwa kuwa kushika madaraka mchezaji wa mpira Kenny Mkapa wa Timu Ya Yanga [Wazee Wa Jangwani-Kwa Jerry Muro] alikuwa ametukuka kuwatumikia Watanzania kwenye soka akiwa Nahodha wa Yanga kuliko Benjamini William Mkapa Rais mtalajiwa wa Tanzania leo hii Mkapa ni Rais Mstaafu....

4: Rais Wa Serikali Ya Mapinduzi Zanzibar DK Shein, wakati anachaguliwa kuwa Makamu wa Rais, baada ya jina lake kutajwa na Rais wakati huo Benjamini Mkapa mjini Dodoma, watu waliangaika kugoogle kwenye Mitandao kutafuta jina hilo kama linapatikana kwenye kwenye mtandao [Google] katika kuonyesha ni jinsi gani huyu Rais alikuwa alikuwa hana rekodi yoyote ile kwenye jamii.

5: Waziri Mkuu wakati wa kipindi cha Rais Benjamini Mkapa, Mh Sumaye yeye ndio kabisa from no where lakini aliwajibika kulitumikia Taifa lake na leo hii anashikilia rekodi ya kuwa Waziri Mkuu aliyekaa kwenye ofisi hiyo kwa muda mrefu sana kuliko Waziri Mkuu yoyote ile toka Tafa lipate Uhuru 1961.

Wako wengi sana kinachomfanya mtu kuwa kiongozi bora sio rekodi umefanya mangapi bali utafanya mangapi...

B: UZOEFU KIBAILOJIA.[GENES]
Wanasayansi wamefanya utafiti na kukubali kuwa binadamu anapozaliwa akili yake kwa asilimia 80% inatokana na kulithi na Asilimia 20% ni matokeo ya mazingira yaliyo mzunguka.Sijui lakini wazungu na kizungu chao walisema ''LIKE FATHER LIKE SON''. Waswahili tukasema ''MTOTO WA NYOKA NI NYOKA''Sikulazimishi kukubali angalia mfano wa huyo uliye mtaja Kenyatta.Kwa mara ya Kwanza toka vyama vingi Rais Wa Kenya, anapata kuhutubia Bunge la Taifa na kwa hotuba yake hiyo Bunge zima linasimama bila kujali tofauti zao za kisiasa kama vyama wanakubaliana na hotuba yake.

Akili ya Rais Wa Marekani Barack H. Obama sio yakubangaiza ni akili ya Obama Senior , yani baba yake Obama, alikuwa ni Mchumi ambae siasa za Ukabira Kenya ndio zilifuta matumaini yake kuitumikia Kenya lakini akiwa ni moja ya vijana wa asili ya waluo walio kuwa na upeo mkubwa sana kwenye elimu lakini mchango wako kama nasaba [GENES] leo hii unawatumikia Wazungu.

Kwa Charles kutoonekana kuwa anashabiana na baba yake [Baba Wa Taifa] si kusema hana vile vichocheo vya kinasaba alivyokuwa navyo Baba yake au Mama Yake, Cha msingi kibailojia ni Kutrigger, moja kwa moja vinasaba vle vitaonekana kwa kuwa kwa Wanasayansi wana namna ya kuhamsha [Push] na vichocheo hivyo ujiziilisha kwa wazi na kufanya maamuzi kwa mujibu wa vinasaba.

Ulishafanya utafiti wa watoto wa kota za polisi kwa kiwango kikubwa uwa wanaishia kuwa kina nani kama sio Polisi na kazi nyingine zozote zinazofanana na ushikaji wa siraha.Chukulia tukio la Westgate Kenya yule kijana wa kisomali aliyeonekana yuko mstari wa mbele kuokoa baadhi ya wahanga wa tukio lile, yuke kijana si Askari wala Afisa Usalama, wala Mwanajeshi wa Jeshi la Kenya.Shujaa yule wa sakata lile ni mtoto wa aliyekuwa IGP Mstaafu wa Jeshi la polisi la Kenya. Uwezo wake na ufahamu wake wa matumizi ya vyombo vya moto kama siraha na maamuzi ya kishujaa [Braveness] si vitu vya mara moja bali ni vitu viko kwenye damu yake na pia kupitia maisha yake ya kila siku na mzazi wake toka akiwa mtoto mpaka utu uzima wanashabiana kwa kulithi, kusikia na kuongea kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto.

Na hata Charles kupitia maisha yake na mzazi wake kuna vitu kavirithi ambavyo kwa macho ya kawaida si lahisi kuviona lakini katika maisha ya kawaida ya kila siku vitaonekana kwa vitendo na maamuzi yatakavyotegemea uzito wa jambo au mambo husika.Mfano leo hii Charles angeamua kuwa FISADI, yani kusema achume kwa faida zake binafsi na kuwa na mtaji wake ni nani angemzuia kuwa mpigaji na kujilimbikizia kinoma, jibu ni hakuna lakini kwa kuwa kwenye vinasaba vyake hakuna aina hiyo ya damu basi si lahisi kuibuka ovyo ovyo kuwa FISADI.

C: UZOEFU WA KIMAISHA.[LIFE EXPERIENCE]
Kupitia nafasi alizopita kama raia wa kawaida mwenye elimu yake, toka shule ya msingi mpaka chuo na kisha kupitia Jeshi la Wananchi Wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo La Arusha mjini alikotumika kwa Muda Mfupi,sasa Mbunge wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti Wa CCM-Mkoa Wa Mara kama ataamua kupigania kwangu naona ni vigezo tosha tena vikubwa sana.Manake kama Mh DOVUTWA yeye alitumia haki yake Kikatiba sembuse mtu aliyetumika Jeshini ambako ndio tunakoweza kusema ni Utumishi mzito kuwa mlinzi wa amani kwa gharama ya Uhai wake binafsi, mimi na wewe tunafurahia maisha na wake zetu usiku huku wao hawajui ni saa ngapi watalala kupumzisha akili dhidi ya adui wasie mjua atatokea wapi.

Wakristu wanasema kesheni kwa kuwa amjui saa wala siku.Utumishi gani unataka kuliko huo wa kijeshi ambao gharama yake ni uhai wa Mwanajeshi husika.Ebuu acha masiahara etii....mwenzio alitumikia Taifa eneo hilo.Wamarekani wanamheshimu sana mgombea yoyote wa chama chochote kile iwe DEMOCRATIC AU REPUBLICAN ambae alishapata kulitumikia jeshi la Marekani [US ARMY].Mwanasiasa yoyote yule toka kona hiyo [ANGLE] uwa anaheshima sana kuliko mwingine yoyote yule katika Race nzima .

Sema kingine brother....kama ni zoefu hoja hafifu sana tena sana.USILUDIE
 
DSN if you want to be a fanboy, get the name right at least.

The guy's name is Charles Makongoro Nyerere, not Charles Julius Kambarage Nyerere.

Makongoro Nyerere - Wikipedia, the free encyclopedia

Kilanga bhana Charles jina la nani................

Charles huyo unaemjua kwa jina gani jingine vile.....Baba yake jina lake Julius

Hivyo nikitaka kumtaja jina lake itabidi nisema jina lake
CHARLES JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
Manake
Binafsi Jina Charles Julius Kambarage Nyerere na Makongoro Julius Kambarage Nyerere nikitu kile kile, ebu nifundishe manake kwa mujibu wa ufahamu wa historia kama sijakosea nitashihishwa jina Makongoro ni jina la Rafiki wa damu wa babu ya Charles, maalufu kama BULITO.

Kwa urafiki huo ndio jina Makongo likaingia kwa familia hiyo na kupewa Charles....kitu ambacho familia nyingi sana za kiafrika tuna majina mawili mawili, hata mimi ninalo.Manake Charles ka uandishi huo ndio kusema Baba wa Charles ni Makongoro, ama unatumia majina yote mawili..
 
Kilanga bhana Charles jina la nani................

Charles huyo unaemjua kwa jina gani jingine vile.....Baba yake jina lake Julius

Hivyo nikitaka kumtaja jina lake itabidi nisema jina lake
CHARLES JULIUS KAMBARAGE NYERERE.
Manake
Binafsi Jina Charles Julius Kambarage Nyerere na Makongoro Julius Kambarage Nyerere nikitu kile kile, ebu nifundishe manake kwa mujibu wa ufahamu wa historia kama sijakosea nitashihishwa jina Makongoro ni jina la Rafiki wa damu wa babu ya Charles, maalufu kama BULITO.

Kwa urafiki huo ndio jina Makongo likaingia kwa familia hiyo na kupewa Charles....kitu ambacho familia nyingi sana za kiafrika tuna majina mawili mawili, hata mimi ninalo.

Kwa formula gani?

Kizanaki kabila lao halitumii formula hiyo, kila mtu anapewa middle name yake. Ndiyo maana hata baba yake ana middle name yake (ambayo si jina la baba yake). Middle name hiyo ni Kambarage.

Kikatoliki hakuna mtindo wa kufanya jina la baba kiwa muendelezo wa jina la mtoto.

Wewe unatumia formula gani?

Halafu kama hujui jina la babu yake ni Burito na si Bulito you are not qualified to be a fanboy.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Nchi hii watu wamepindua usultani kwa damu. Baba yake huyo Makongoro mwenyewe alikuwa mmoja wa strategist wa kuondoa huo usultani.

Kwa nini mnataka kurudisha usultani?

Cc Andrew Nyerere
 
Last edited by a moderator:
Kwa formula gani?

Kizanaki kabila lao halitumii formula hiyo, kila mtu anapewa middle name yake. Ndiyo maana hata baba yake ana middle name yake (ambayo si jina la baba yake). Middle name hiyo ni Kambarage.

Kikatoliki hakuna mtindo wa kufanya jina la baba kiwa muendelezo wa jina la mtoto.

Wewe unatumia formula gani?

Halafu kama hujui jina la babu yake ni Burito na si Bulito you are not qualified to be a fanboy.

Rudini kwenye hoja.
Je anafaa kuwa rais wa Tanzania?
 
  • Thanks
Reactions: DSN
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom