My ex is back

PesaNdogo

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
1,992
Reaction score
1,294
Habari zenu wanajamvi,
Nimekuwa na mahusiano na mtu mmoja kwa miaka mi5, hakuwa na ukaribu sana jambo lililofanya nihisi kuna mengi sijayajua.

Mwaka wa nne wa kuwa na mahusiano nae vilianza vibalaa kibao Mara wanawake wananipigia simu kuniambia yeye ni mpenzi wao Mara wamezaa nae na wengine wakidai kuna wenzao wanawajua nk ila mimi walikuwa hawanijui jina lakini wananiambia anawasevu watu kibao my love, sijui mke wangu nk. Nlipohoji sikupata majibu ya kuridhisha ikiwemo kuwa amepoteza simu labda huyo muokota simu ndo kasoma msg na mwasiliano mengine na kwa kuwa atakuwa Anamfaham anataka kutugombanisha. N
Nikabadili line kukwepa usumbufu, baada ya mwaka kikatokea kisa kama cha kwanza kwa kupigiwa simu na mwanamke fulani nisiyemfahamu naye akaongea kama yule na majina yanafanana kwenye visa lakini safari hii alinitaja kwa jina sijui alipata kwa mpesa au wapi na aliongea mambo yaliyoniumiza kweli. Sikumjibu vibaya, nilimwambia asante tu. Mhusika hakuwa na majibu ya kuaminika sana , eti hajui nani ila kuna watu wanataka kutugombanisha, hapo napopigiwa Mara zote tulikuwa sehemu tofauti. Ila kwa mazingira tuliyokuwa hakuwana tabia ya kujiweka karibu sana akiulizwa anadai shughuli zinambana .
Mara ya mwisho nlipokuwa naendelea kumhoji kuhusu haya mambo ndipo aliponipa majibu kwamba yeye mwanaume anaamua awe na wanawake wangapi, niangalie nafasi yangu kwake nk alianza majibu ya kikatili hasa baada ya kile kisa cha kwanza cha mawasiliano Mara zote ansema ananilaumu kwa kuendekeza mawasiliano na wa tu nisiowajua lkn ukweli ulibaki alikuwa Ana mambo yake tu kwan shida iko wapi kama hajafanya wanayosema . Mara siku nyingine aseme mi nampelekesha hapendi kupelekesihwa, Mara anakata mawasiliano tu na hatokei sehemu eti dharura.
Ni mtiririko mkubwa wa matukio, mara ya mwisho nikamwambia kama anaona amenichoka bora aniache. Baada ya mda nikampigia akakata simu, nikamuuliza vipi akajibu yeye habipiwi. Akaacha kuwasiliana nami nikatulia kimya ingawa yaliniumiza ila nliona nafuu tu aniache. Siku flan nilitafutwa na rafiki yake kama mdogo wake hivi akawa ananijulia hali nikashang!a ila sikusema kitu. Baadae nikamtumia msg huyo shemeji kwamba nataka niongee nae jambo, lengo langu nimwambie sipo na nduguye lkn sikumwambia nikasema moyoni aliyenitambulisha kwake ndo amwambie.
Tulikuwa na mwaka mzima wa kutengana na miezi mitatu ya kukata mawasiliano sasa amerudi kama hajui aliyofanya, anaomba msamaha kwamba yeye binadamu sio malaika nimsamehe yote yaliyopita anaamini mimi ni wake tu n.k na ananimiss nikaonane nae. alinitenga mwaka mzima. Sijui ananiona mjinga kiasi gani. watu walionisumbua walifikisha mpk kwa wazazi wangu maneno kwamba Nina mahusiano na bwana wao kupitia mmama mmoja mmbea hata nikaambiwa niache kuwatia aibu kwa kuwa na mwanaume Malaya. Upande mmoja unasema nimsikie atakachosema, maana nimekuwa muwazi kwake kuwa amenifanyia ubaya mwingi mno sio rahisi kufuta Mara moja kumbu kumbu . Lakini nakumbuka kichwani point hii once a cheater he will always cheat and play around so hana maana. Mnaonaje ndugu zanguni mi kama dada, mdogo,rafiki au binti yenu.
 
mnhh uwe unaandika kwa aya basi

halafu wewe huna uamuzi kabisa
vyoyote tutakavyo kushauri itakuwa bure..
 
Zimwi likujualo halikuli ukaisha.
Mwenza si malaika, mpe nafasi ya 2.
 
Sasa mpaka hapo wewe moyo wako unakuambia nn? au kipi chake kilichukuvutia sababu mapenzi ni maneno matamu
amabayo yeye hana,mapenzi ni Kuaminiana yeye sio muaminifu sujui ni kipi au michezo yake? kwani yuko peke yake..
 
Wewe unaonaje mamy,uko tayari kumsamehe na kusahau yaliyopita?
 
mnhh uwe unaandika kwa aya basi

halafu wewe huna uamuzi kabisa
vyoyote tutakavyo kushauri itakuwa bure..
Sawa Boss, nimeweka Aya. Naomba unipe mawazo yako tu ndo maana naomba ushauri
 
kuna wanaume bil 83.7 duniani............wewe tu......
 
Kimbia.. usiangalie nyuma kwa mtu kama huyo. lakini umsamehe ili isiwe inakuumiza na uachie. wakwako yupo huyo mwache aende, hajui thamani yako
 
jamani!!!! hivi wanaume nanyinyi huwa mnaumia kweli kama ambavyo huwa mnaumiza wapenzi wenu kweli, kweli!!! huwa natamani kuwalaani, lakini ndo hvo, dua la kuku halimpati mwewe! mi naona nyie huwa hamuumii vile!
 
Kuna kitufe kimeandikwa edit, kimehusika hapo. Usistuke, Nipe mawazo yako tu

Ni mpenzi sio MUME......kaenda huko katanga na njia sa ndo kaja kurealise umuhim wako

katika maisha...Wanaume bana

There are so many fish in the pond...Move on dia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…