My big no to GMO!

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
69
252
Sayansi na teknolojia ni maendeleo ya mwanaadamu ambayo yanaelekea kuiharibu Dunia yetu nzuri tuliyozawadiwa na Mungu.

Hii ndo kusema akili za mwanaadamu sasa zimepindukia kiasi cha kumdhuru yeye mwenyewe bila kujua.
Ninathubutu kusema haya yunayoyaita maendeleo hakika ni maangamizi kwetu.

Ninaizungumzia GMO, neno linalobeba sentensi yenye maneno matatu ya kingereza, yaani Genetically Modified Organisms, ikimaanisha viumbe(mimea) vitengenezwavyo maabara, au viumbe(mimea) vilivyoboreshwa kijenetiki.

Kwa macho yanayoongozwa na Ubongo wenye uvivu wa kufikiri hii inaitwa maendeleo kwa sababu tu mbegu ya mmea wa Papai au Nyanya iliyotengenezwa maabara inakupa mapapai au Nyanya kubwa na nyingi zaidi ya ile mbegu ya asili.

Yes, ninamaanisha ukiwa mvivu wa kufikiri utaona Mpapai kufungasha mapapai mengi na makubwa tangu ukiwa mfupi na ndani ya miezi michache ni maendeleo,THUBUUUTUU!

SASA kwa taarifa yako ukisikia changa la macho ndo hili sasa na sababu ni hizi zifuatazo:

1. Mbegu hii ya Nyanya hutoipata popote zaidi ya duka la kilimo na wao wamenunua kiwandani.

2. Mbegu hii ukiipanda haitomea isipokuwa umeinunulia na madawa/kemikali ambazo ni aidha kwa mfumo wa mbolea ya kupandia na kukuzia, na madawa ya viuatilifu, yaani zile kemikali za kuzuia au kuua wadudu wanaoshambulia mimea ya mbegu hizo. Kumbuka mbegu hizo zimetengenezwa kuzalisha mmea unaovutia sana wadudu waharibifu kuliko ile mimea ya asili.

3. Mbegu hizi huzalisha mazao kwa kuzingatia wingi (Quantity) na wala si ubora(Quality). Na matokeo mazao yake yamepoteza ile ladha nzuri ya asili.

4. Matokeo ya ujumla ni kwamba ile ardhi yetu nzuri yanye rutuba tuliyozawadiwa na Mungu wetu leo haitokuwa na thamani tena kwa sababu haitokupa mazao isipokuwa mmea wako umeunyunyizia mbolea za viwandani na makemikali ambayo mengi ni sumu kwa afya zetu.

5. MSIBA zaidi ni zile mbegu za asili zenye ladha ile tamu mdomoni sasa baada ya muda hazitopatikana tena kwa sababu ya hamasa kubwa inayofanywa na Serikali kushawishi wakulima kutumia hizo mbegu wanazoita za kisasa.

Serikali imekuwa kipaumbele sana kuhamasisha matumizi ya mbegu hizi za kisasa, na zaidi ikisemwa kwamba haikwepeki!

Natamani pia ituambie ni upi mpango wa serikali kuhakikisha tunakuwa na akiba ya ARDHI na MBEGU zetu za asili ili tusiingie mazima kwenye mtego huo unaoitwa maendeleo ilhali wazi ukionesha TATIZO siku za usoni??

ONYO:
Wakati ukifurahia Tufaa (APPLE) kubwa la rangi nyekundu, jaribu kujiuliza namna lilivyozalishwa kabla hujalila!

IMG-20230905-WA0010.jpg
 
GMO haina shida, shida ipo kwenye Serikali zetu hazina mikakati ya kuhifadhi mbegu.. Imagine now unakula tikiti bila mbegu au size ya tikiti kubwa au mahindi yasiyoharibiwa na wadudu huoni mafanikio kwa mwanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo watu wengi wanashindwa kutofautisha kati ya hybrid seeds na GMO seeds
Isitoshe tu kusema hivyo mtaalam turudisheni shule kidogo. Labda niulze hivi zile mbegu za matunda kama yale ya vimiti vifupi tu lakini vimeza sana ni vya mbegu zipi ni hybrid au ndo hizo GMO .. halaf kwani hizi za hybrid siwezi kuindeleza mbegu tena mpaka nikanunue tena nyingine? nikitaka kuipanda sehemu nyingine
 
Naomba nikuulize mleta mada, hivi ugali huwaga unakula? Mboga mboga je?

Tuanzia hapa halafu ndio tuje huko kwenye GMO
 
Back
Top Bottom