A. SAUTI
Nimependa kuwa kwa kiasi kikubwa sauti zimeendana na matendo mf. ngumi, mateke na hata urukaji. Sauti ya muziki ingeweza kuwa chini zaidi ili vitendo visikike vizuri. Vinginevyo,
sauti naipa alama 60%.
B. VITENDO/MIJONGEO
Hapa pia natoa alama nyingi kwa kuwa mijongeo
(movements) ni za kasi ya kukubalika/kupendeza. Kuanzia ukimbiaji, ngumi na mateke ni ya kiwango kinachokaribia kurandana na vitendo katika maisha halisi.
Natoa alama 70%.
C. PICHA/MICHORO
Bado. Ningependa kuona sura na maumbo ya watu na vitu/mazingira vinakuwa dhahiri zaidi kuliko sasa. Picha kwa sehemu kubwa ndiyo humvuta mtazamaji. Miti
ionekane wazi kabisa kuwa ni miti na watu vivyo hivyo.
Natoa alama 30%.
D. CHANGAMOTO
Boresha zaidi ubora wa picha zako. Waweza kuona mfano hapa chini. Ni kazi ya Watanzania hii, japo kuna mkono wa Wazungu (utawala) lakini aliyefanya sanaa ni Mtanzania (kwa kadri ya ufuatiliaji wangu).
Waweza kutembelea tovuti yao
hapa.
ANGALIZO: Lakini kama ni hobby tu ni ruksa kutotilia sana maanani maoni yangu, wakati mwingine napata taabu kidogo kuwa wa wastani.
Kila la Heri.