My advice for 2016 kwa WanaJamiiforums wote

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
1-Tuzalishe Bidhaa+huduma zenye ubora na kiwango cha juu!
2-Tuweke bei zilizo Realistic
3-Tuwe waaminifu tunapokopeshana,turudishe kwa wakati Na...
4-Unapochukua bidhaa ya mtu if possible lipa kwa Cash .
5-Tunapokoseana tuombane radhi na kusameheana

6-Kila mwenye nguvu na afya ni lazima ujitume kufanya shughuli ya uzalishaji !

7-Invest Pesa +Muda ktk Matangazo coz bila mkakati Madhubuti wa matangazo hamna wateja &therefore hamna mapato!

8-Pokea Order unazozimudu, usizidishe kwa tamaa utaharibu kazi+jina lako!

9- Chukua muda kupata information about certain business kabla hujaingiza pesa kuifanya!

10-Kwa wenye Biashara tayari ukiweza kuwa na branch or ku-expand pls fanya hivyo,ina diversify Risks !

11-Kama unaweza miliki at least 2,3 or 4 businesses !Ili moja kama haizalishi unaendelea kupata pesa ktk Biashara ingine (myself ninafanya hivyo imenisaidia sana,unakuwa haukaukiwi )

12-Hudhuria events.
matamasha, maonyesho, seminars mbali mbali ili kumfungua Akili na kupata Ideas za nini cha kufanya!

13-Jitahidi u-save 10 %-30% ya kile ukipatacho kwa ajili ya kununua Assets(kuweka Fix deposits,kunuunua, shares ktk makampuni zenye kutengeneza faida , kununua viwanja/nyumba nk)..

14-Pia jiwekee lengo la kuwa na cash at least 5m na kui-Maintain ktk Bank account ikusaidie ktk emergencies zozote maishani (misiba,kuuguza, Kuvunjiwa, kuibiwa nk )

15-Bana matumizi yasiyo ya lazima (kuuendesha Magari yanayotumia fuel nyingi, Nguo, nywele, Viatu,kusafiri kusiko muhimu, kuwekeza hela ktk vikundi vingi visivyo na Tija, kupanga ktk nyumba expensive! Kukesha ktk Bar na sehemu za starehe kwa kisingizio cha 'networking ', kuchangia kila shughuli, jifunze kuchagua chache muhimu! )

16-Usikope hela Bank/VICOBA /Saccos kufanya Biashara usiyoielewa na usiyoifanyia research !

17-Tulia ktk Biashara yako, Tafuta mikakati ya kuikuza, tafuta solutions za vikwazo vyako, ulizia kwa waliovuka ili wakusaidie, also Googl.

18-Jielimishe, Noa Ubongo,
Soma Vitabu, Majarida ya Kibiashara , Sikiliza Cds, angalia Dvds, kila Mara tafuta kuongeza maarifa ya vitu vilivyopo ktk Industry yako! Pia soma makala za how to Manage your business efficiently!

Acha kuuangalia/kusiliza Junk news !Acha ku-idle ktk social media.

19-Kabla hujaenda popote asubuhi piga Goti Omba Mungu akutangulie ktk kila ufanyalo na akupe solutions za vikwazo! Pia akupe stamina kuhimili Magumu ya maisha utakayokumbana nayo!

Urudipo home kabla ya kulala Piga Goti kumshukuru Mungu aliyekuvusha ktk yote! Kama ni mtoaji Fungu la kumi endelea usiache ni kati ya vitu muhimu vinavyo Mgusa Mungu kukufungulia milango yake ya Baraka!

20-Ishi njia/maisha yaliyonyooka yenye Intergrity ,usiwe na Double standards, kuwa mkweli, Usiwe na Chuki na visasi,usitukane, usiwe mtu wa Hasira kali, Usiwe na wivu mbaya kwa maendeleo ya wengine, Usitapeli, usiwe majivuni na dharau, penda watu wote na heshimu watu wote!

Mungu akubariki kwa kazi uzifanyazo kwa bidii pasipo Ulegevu....

21-Tunza afya yako! Lala masaa ya kutosha, kula matunda na Mbogamboga kila siku kwa wingi, punguza kula nyama, hasa nyekundu,Kunywa maji ya kutosha, usitumie Pombe/sigara kwa wingi, usijamiiane pasipo tahadhari sahihi!

Kuwa na mahisiano mema & ya amani na mume/mke/watoto /wafanyakazi /majirani/wanakikundi nk.

Kwa Leo ni haya machache!

Ninaamini umepata kitu kitakachokusaidia mwaka 2016 !

Share na wengine uwapendao!
 
Asante kwa ushauri mzuri ila ni vyema ukakitambua chanzo pia
 
Ushauri mzuri sana. Maoni yangu, Namba 19 ndiyo ungeifanya ya kwanza. Nashukuru kwa hili.

Ahsante!
 
nimefurahi pale namba 21 kwenye kutunza afya umekemea uvutaji sigara kwa wingi..ila marijuana hujaitaja kabisa. ungeitaja negatively ungeruin ushauri woooooote kwenye thread yako.
 
Tumeupokea si useme tukutane basi kwa party ya pamoja kwa majina halisi haya ya JF yabaki siri ya mtu watu wasije shikana mashati
 
Asante mkuu,Mungu akubarik kwa nasaha njema nadhani itatufaa wengi km si wote,amen!
 
NI VIZURI UNAPO TOA ANDIKO AMBALO SI LAKO LIWE ZURI AU BAYA KUTOA CHANZO CHA ANDIKO HILO, KAMA ANDIKO HILI ASILI YAKE NI HAIKA LAWERE,OWNER WA MBEZI GARDEN HOTEL.,,, "PLAGIARISM
 
Back
Top Bottom