Mwongozo wa JF: What should start Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba?

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,169
10,786
Tuna miaka minne ya kuingia kwenye uchaguzi na kwa walio wengi bado ndoto ya kuiondoa CCM haijafa na kwanza ndio inakua.

Mabadiliko ya katiba in reality yanachukua muda mrefu sana, unless we need to rush into it na serikali iwe pamoja na wapinzani kitu ambacho si hakipo.

Ninavyoona naona kama pressure ikiwekwa kubadili tume ya uchaguzi angalau kunaweza kukawa na tumaini zaidi ya kuindoa CCM. Kwa mawazo yangu ya haraka ambapo nahitaji mwongozo kwa wanaojua je,

1. Kubadili tume ya uchaguzi ni lazima katiba ibadilike?
2. Je kama katiba ibadilishwe kwanza ndio tume ibadilishwe , je haiwezekani ikafanyika pressure ya kujadili ili kwanza?

3. Kama tume ya uchaguzi inaweza kubadilishwa kwa sasa naona kama ni vizuri tukaanzia hapo ili hali main objective/ajenda ya kubadili katiba isifutwe.

4. Hata kama katiba itabadilika kesho, we may have another time to implement it accordingly..that

Siasa za Afrika ni nani anatangaza matokeo ndio muhimu zaidi, si nani ameshinda

What do you think?
 
Waberoya

Mkuu tatizo la CDM ni kutumia sana mawazo ya wanaharakati, nadhani bado hawajapata wanasiasa waliobobea.

Nionavyo kosa kubwa ni kukubali musawda urudi tena serikalini,itachukua muda sana kuanza tena mchakato, na hata ukianza CCM watakua wameshajipanga kwa kujua CDM wataegemea wapi.

Kuhusu tume,ipo kwa mujibu wa katiba, hivyo haiwezi kubadilika bila kuibadilisha katiba. Itabidi labda tuweke tena kiraka ili tuibadili tume,ni kama kurudi kule tulipokukataa mwanzo.

Bila kucheza vizuri karata za kisiasa, Katiba mpya inaweza kupatikana siku chache kabla ya uchaguzi, kitu ambacho hakiwezi kuwasaidia wanamageuzi wengi
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tatizo la CDM ni kutumia sana mawazo ya wanaharakati,nadhani bado hawajapata wanasiasa waliobobea.

Nionavyo kosa kubwa ni kukubali musawda urudi tena serikalini,itachukua muda sana kuanza tena mchakato,na hata ukianza CCM watakua wameshajipanga kwa kujua CDM wataegemea wapi.

Kuhusu tume,ipo kwa mujibu wa katiba,hivyo haiwezi kubadilika bila kuibadilisha katiba.Itabidi labda tuweke tena kiraka ili tuibadili tume,ni kama kurudi kule tulipokukataa mwanzo.

Bila kucheza vizuri karata za kisiasa, Katiba mpya inaweza kupatikana siku chache kabla ya uchaguzi,kitu ambacho hakiwezi kuwasaidia wanamageuzi wengi

Mkuu asante kwa maelezo, Usiwataje chadema mkuu ili ni la wote wataka mabadiliko

je lipi bora tukubali tu kuweka kiraka cha tume huru ya uchaguzi au tubiri another decade for new const.

Naamini kuwa tukiwa na tume huru ya uchaguzi at least haki itatendeka kwenye uchaguzi lakini si kama ilivyo sasa hivi.
 
Mkuu asante kwa maelezo, Usiwataje chadema mkuu ili ni la wote wataka mabadiliko

je lipi bora tukubali tu kuweka kiraka cha tume huru ya uchaguzi au tubiri another decade for new const.

Naamini kuwa tukiwa na tume huru ya uchaguzi at least haki itatendeka kwenye uchaguzi lakini si kama ilivyo sasa hivi.

Ni bora tuweke kiraka tupate tume huru,lakini itatia shaka kuhusu umakini wa kudai haki zetu.

Kumbuka nako katika kubadili katiba ili tupate tume huru,kuna mapendekezo ambayo kwayo,yanahitaji kujadiliwa kwa kina,je ukiletwa tena utumbo itakuaje?
 
Waberoya;

Mkuu ni jukumu la wasiasa wetu kutambua kwamba moja ya matatizo makubwa ni hili la tume ya uchaguzi kama kweli wanasiasa wa nchi yetu pamoja na sisi wananchi wenye mawazo chanya kuhusu maendeleo ya taifa letu tungelitazama hili kwa jicho la tatu .

Ufumbuzi wa hili jambo ni muhimu sana tumeona athari zake Ivory Coast, Zimbwabwe na Kenya hata hapa kwetu kwenye uchaguzi uliopita maapungufu mengi yameonekana kwenye tume ya uchaguzi
 
Last edited by a moderator:
Maganga Mkweli

Vema,Lakini bahati mbaya hakuna mwanasiasa anaejali hilo labda Mch.Mtikila,aliwahi kusema uchaguzi kwa tume na katiba hii,ni ndoto upinzani kushinda.

Leo hata ukiitishwa uchaguzi, utaona mbio na mashindano ya kuingia katika kinyang'anyiro bila kujali udhaifu wa tume
 
Last edited by a moderator:
mkuu ni jukumu la wasiasa wetu kutambua kwamba moja ya matatizo makubwa ni hili la tume ya uchaguzi kama kweli wanasiasa wa nchi yetu pamoja na sisi wananchi wenye mawazo chanya kuhusu maendeleo ya taifa letu tungelitazama hili kwa jicho la tatu .ufumbuzi wa hili jambo ni muhimu sana tumeona athari zake ivory cost ,zimbwabwe na kenya hata hapa kwetu kwenye uchaguzi uliopita maapungufu mengi yameonekana kwenye tume ya uchaguzi

Vema,Lakini bahati mbaya hakuna mwanasiasa anaejali hilo labda Mch.Mtikila,aliwahi kusema uchaguzi kwa tume na katiba hii,ni ndoto upinzani kushinda.
Leo hata ukiitishwa uchaguzi,utaona mbio na mashindano ya kuingia katika kinyang'anyiro bila kujali udhaifu wa tume

Well said guys, I always call this as political games, where you know what to start , why to start and when to start.

Naogopa kutoa baadhi ya conclusion, ukweli ukiwaza sana kuhusu taifa letu na tunaowaamini watatukumboa basi imani yaetu imejengwa mchangani.

Are we real serious to remove CCM from power?

All these efforts, makongamano, midahalo n.k at least kwa sasa hivi tungekuwa tunajadili nani awemo nani asiwemo kwenye tume and how it shoud be operated!

If we find good referee then the match/game is worthy to be played
 
Mkuu asante kwa maelezo, Usiwataje chadema mkuu ili ni la wote wataka mabadiliko

je lipi bora tukubali tu kuweka kiraka cha tume huru ya uchaguzi au tubiri another decade for new const.

Naamini kuwa tukiwa na tume huru ya uchaguzi at least haki itatendeka kwenye uchaguzi lakini si kama ilivyo sasa hivi.

Anaweza kuepuka kuwataja CDM mkuu, lakini likifika bungeni, Makinda atasema ni la CDM, likienda kwa wananchi, Mufti, na 'wazee wa mila' na kwenye makongamano watasema ni la CDM, so huwezi epuka kuzingatia CDM hapa, hata kama pressure itakayowekwa itakuwa inaongozwa na watu ambao hawahusiani kabisa na CDM, at the end of the day litaonekana ni la CDM.

Then, kuhusu wazo lako ni zuri lakini chance ya kufaulu ni ndogo mno almost negligible. Kwa vyovyote vile mchakato wa aina hii lazima kwa namna moja au nyingine upite bungeni, ambako unajua majority wamewekwa na wanategemea kusaidiwa na hiyo tume mbovu.

Binafsi naamini wapinzani wanaweza kujipanga wakiwa na tume hii hii, na wakashinda vizuri tu, tena kwa kishindo. Najua haikuwa nia hiari ya tume hii kuwapa wapinzani zaidi ya 35% uchaguzi uliopita. Sasa kwa maandalizi 'kidogo' waliyofanya wapinzani, kama waliweza kuambulia 35%, sio kitu cha ajabu tume ikashindwa kuwanyima 75% yao hapo 2015.

Yapo maeneo ambayo zikiwekwa nguvu, kura nyingi sana zitadhibitiwa, maana kwa mfano, chukulia CDM, katika uchaguzi uliopita yalikuwe majimbo mengi sana hawakuwa na mgombea ubunge, kata nyingi sana hawakuwa na wagombea udiwani, na vituo vingi sana hawakuwa na wasimamizi. Vilikuwepo vituo vingi sana walikuwa na wasimamizi ambao hawakuwa organized, wala equipped. Kulikuwa na majimbo mengi sana ambako kura zilibadilishwa baada ya kuhesabu bila kuwa na mtu wa kuzidai 'kwa nguvu' kama ilivyofanywa katika baadhi ya majimbo na kuzaa matunda.

Kinachonipa matumaini kuwa upinzani unaweza kushinda tukiwa na katiba na tume hii mbovu ni haya yafuatayo

  1. Kutumika kwa nguvu kama ilivyokuwa Arusha, Mwanza n.k
  2. Kufikia 2015, mwamko wa watu watu wenye uwezo kielimu na kifedha kugombea kupitia upinzani utakuwa mkubwa
  3. Amsha amsha ya nguvu ya umma itawatisha watu wa tume ya uchaguzi
  4. Kesi inayoendelea Kenya, na yanayowatokea watu kama Mubarak na BenAli itawafanya watawala wetu kuwa na hofu ya kutenda faulo hadharani
  5. Kufikia 2015 maendeleo ya miundombinu ya mawasiliano yatakuwa makubwa kurahisisha mtandao wa kulinda kura.
So, pamoja na juhudi zote zinazoweza kufanyika kupressurize tume huru na katiba mpya, bado yapo matumaini makubwa sana kwa vyamam vya upinzani kufanya vizuri sana hata kama mabadiliko hayatatokea kwenye tume na/au katiba.
 
Suala la tume huru ya uchaguzi ni muhimu sana, kwa kuwa ndio kati ya mihimili mikubwa inayotumika kukihakikishia CCM kuwepo madarakani. Katiba ni muhimili mwingine, sasa uzuri muhimili huu wa katiba tumeutikisa.

Ila suala la Tume huru ya uchaguzi halijaongelewa sana, ingawa ndio naweza sema wanaoongoza kuua demokrasia nchini kuliko hata polisi.
Tume hii ya sasa haiko huru, na zaidi ya hapo wao ndio wazee wa kukamilisha fitna za CCM. Silisemi hili kiushabiki la najua mnakumbuka malalamiko ya wazi kabisa na vitendo tofauti vya kiupendeleo vilivyokuwa vinatolewa kwa CCM na Mgombea uraisi mwaka jana katika kampeni. Mfano muda wa kampeni ulikuwa mwisho saa 12 lakini JK alikua anapitiliza muda na haambiwi kitu!

DAFTARI LA WAPIGA KURA:
Pia kwa kuwa lisemwalo lipo, ngoja niseme, HILI NI JAMBO MOJA TU. hapa kwenye hili daftari ni kwamba yasemekana kuna propaganda za kiutendaji zinaendeshwa ndani kwa ndani ili kufanikisha uchakachuaji.....Mfano Tume (QUESTIONING ITS NEUTRALITY, ZAMANI ILI UWE KWENYE CHOMBO NYETI CHA SERIKALI NA USALAMA ILIKUA LAZIMA UWE CCM) hili halijafa bado) huyaondoa majina ya watu wanaojua hawataipigia kura CCM, perhaps wataipigia Chadema, watu kama vijana nk.. then si hilo tu kabla ya kuyabandika wanayachelewesha kubandika majina haya, na si bure wakiyabandika tena siku chache tu kabla ya uchaguzi (yaweza kuwa) wanatumwa vijana (kama wale walioenda kulala usingizi Karimjee) wakayabandue makaratasi katika vituo, Mtu unaenda kuangalia jina lako hulioni, hadi uanze kufuatilia (utaratibu wake mgumu pia) unachoka, unaboreka na unaamua kupotezea and therefore hautapiga kura. Kwa wabishi kama mimi utaenda kituo cha kupiga kura tu siku ya uchaguzi na utashangaa ulijiandikisha hapo lakini jina lako halipo.

Na kwa kua wabongo wengi hawapendi usumbusfu mtu ataondoka zake. HATOPIGA KURA. wapiga kura halali wanakosa kutumia haki zao. Najua mnajua low turn out ya watu kupiga KURA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA JANA, ni ya kusikitisha. at the same time tume wanadai kazi ya kuelimisha na kuhamasisha wapiga kura si yao peke yao ni ya wote vikiwemo vyama vya siasa na wanasiasa (ambao leo hii wanakataliwa waisishiriki mchakato wa kampeni kuelimisha watu juu ya katiba mpya)

Hakika tume mbovu hupelekea kuwanyima watu haki yao ya kupiga kura kwa maslahi fulani.

In addition, CCM INA WATAALAMU WENYE ELIMU PANA YA TABIA NA AINA ZA WAPIGA KURA, AND THEY TEND TO USE THEIR MEANS AVAILABLE TO PLAY AROUND WITH THIS. MATOKEO YAKE THEY WIN EASLY. INGAWA UNAWEZA KUSEMA KUNA UCHAKACHUAJI LAKINI WAKICHEZA NA TUME YA UCHAGUZI TU, PAMOJA NA DAFTARI LA WAPIGA KURA WANAWEZA KUSHINDA BILA KUCHAKACHUA.

TENA WANACONSULTANTS na MEMBERS ( I personally know Phd holders) WALIOBOBEA MAMBO YA DEMOGRAPHICS, STATISTICS NA FORECASTING ZAKE (HIZI NI MATH KWENDA MBELE, WENGI TUNAKIMBIAGA MASOMO HAYA, kwa wale wanaokumbuka mf. Partial or Multiple regression analysis na forecasting!). THESE GUYS KNOW HOW TO FORECAST TRENDS AND HOW THEY CAN INFLUENCE THE OUTCOME (MATOKEO YA KURA) AND SO THEY EASILY WIN. NA MKABAKI KUSHANGAA KWANINI DR SLAA ALIPATA WATAZAMAJI WENGI KWENYE KAMPENI LAKINI HAKUSHINDA.

AND MIND YOU HADI KATIBA MPYA IWE TAYARI, KWA MUDA UNAOBAKI KABLA YA UCHAGUZI UJAO HAUTATOSHA KURESET THE SYSTEM

Ninachosema ni kwamba TUUNGÓE NA HUU MUHIMILI WA PILI MDUDU MAGAMBA AFEEE KABISA!
 
vema,lakini bahati mbaya hakuna mwanasiasa anaejali hilo labda mch.mtikila,aliwahi kusema uchaguzi kwa tume na katiba hii,ni ndoto upinzani kushinda.
Leo hata ukiitishwa uchaguzi,utaona mbio na mashindano ya kuingia katika kinyang'anyiro bila kujali udhaifu wa tume
macho na masikio yatulio wengi ni kwenye huu mchakato wa katiba mpya ila hili sura nafikiri lingetazamwa kwa mapana sana watanzania tuamke ushabiki ukae pembeni agenda za msingi kama hizi zina hitaji michango na ningeomba wasomi hasa wanasheria wa kitanzania wawe wazalendo kwenye masuala kama hili ambalo huwa linaguza watanzania wengi .hatuwezi ona madhara makubwa kwa sasa ila hatari iliyo mbele yake ni kubwa sana
 
Tuko,

Mkuu.
Hapa CDM wanapaswa kusawazisha kosa walilofanya ambalo bado wanayo nafasi kama wataamua kujipanga vyema.
Kosa kubwa la CDM ilikuwa ni kuunda kambi ya upinzani peke yao na ku-side line vyama vyengine na hata kuingia katika siasa za maji taka baina yao.

CDM wanaona kuwa wana nguvu ya umma lakini wanasahau walipata kura 26%. Muda upo kama wanataka kuunganisha nguvu na vyama vyengine. Si lazima kuwaingiza ndani ya upinzani lakini wanaweza kufanya rapprochement na vyama vyengine ili kukuza sauti ya upinzani katika suala kama hili la kudai tume huru kabla ya uchaguzi mwengine.

Haionekani kuwa "Katiba mpya" itakuwa tayari wakati wa uchaguzi mkuu ujao.Tayari CCM wameshinda raundi ya mwanzo, kupeleka Rasimu mbovu ya muswada wa "Katiba mpya" ili kupima joto. Kwa hiyo wamepata breathing space ya kutayarisha "uchafu" mwengine. Kwa kifupi dana dana imeanza. Na muda hausubiri,unakimbia.
 
Linalowezekana leo na lisingoje kesho; Tume Huru ya Uchaguzi wa Bara na Visiwani ipelekwe mara moja bungeni huku tukiwa tunaendelea na mlolongo mzima wa kuunda katiba mpya ya wananchi nchini.
 
Linalowezekana leo na lisingoje kesho; Tume Huru ya Uchaguzi wa Bara na Visiwani ipelekwe mara moja bungeni huku tukiwa tunaendelea na mlolongo mzima wa kuunda katiba mpya ya wananchi nchini.


Swali la kwanza, je Tume ya uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa Katiba au la?
 
Katiba inayokidhi haja za watanzania ikiwemo tume huru ya uchaguzi ndio kinachotakiwa. Tatizo ni serikali kutokuwa na nia ya dhati ya kuunda katiba mpya. Kwa mfano, wameleta bungeni mswaada kandamizi unaompa rais madaraka makubwa na kuwa ndio mwamuzi wa mwisho wa namna katiba itakavyo patikana, afadhari umekataliwa.

Cha msingi kwa sasa ni kuendelea kudai kwa nguvu zote katiba mpya, tukisema tukomalie tume huru ya uchaguzi tu itakuwa mtindo ule ule wa viraka! Ni afadhari hata katiba ikichelewa lakini mwisho wa siku tume na katiba nzuri inayokidhi mahitaji ya watanzania wote wakiwemo CCM wenyewe!!
 
Swali la kwanza, je Tume ya uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa Katiba au la?

baadhi ya watu hapo juu wamesema ndio, imeundwa kwa mujibu wa katiba. Swala ninaloona ni vyema basi hata tukalazmisha kiraka hiki kizibwe, kwa kuwa na tume huru, then tukaendelea na mchakato wa katiba mpya
 
Katiba kwanza, kwa kuwa tume huru ya uchaguzi itatokana na katiba.Tatizo watu wanaangalia uchaguzi 2015 .Tusiangalie uchaguzi 2015 bali miaka 200 mbele.
 
baadhi ya watu hapo juu wamesema ndio, imeundwa kwa mujibu wa katiba. Swala ninaloona ni vyema basi hata tukalazmisha kiraka hiki kizibwe, kwa kuwa na tume huru, then tukaendelea na mchakato wa katiba mpya

Kama mpango ni kwenda kwa kulazimisha, tutalazimisha mangapi?

Je hii nchi itatawalika? assume mwaka 2015 CHADEMA watatawala nchi!
 
Back
Top Bottom