Mwongozo wa JF: What should start Tume Huru ya Uchaguzi au Katiba?

Kuhoji tume?Yaani uhoji siri ya ushindi wao wa kishindo!Ni kama Barcelona kuwauzia Real Madrid Lionel Messi kirahisi rahisi tu!Kudai haki yoyote ile yenye ukombozi ndani yake lazma umwage damu!Kwasababu hatuko tayali kwa hilo tutapata haki ambayo sio haki.Sisi mara nyingi huwa tunaomba na kuwaramba miguu watawala kama vle wafalme vile,wakati wapo hapo juu on behalf of us wajameni!Tuendelee kulalamika tuone kama tutakuja kufanikiwa!
 
Inashangaza kuwa kwanini tume ya uchaguzi mpaka leo haijatangaza kuwa kiti cha ubunge cha IGUNGA kiko wazi
kama mnakumbuka kuna mbunge mmoja wa CUF alikuwa anaitwa salum msabaha alijiuzulu kwenye television kama RA hivi hivi na baadaye
kukanusha na kudai kuwa alilazimishwa kujiuzulu lakini tume ya uchaguzi ilisema kuwa ameshatangaza kwenye TV that is enough evidence na kutangaza kuwa jimbo liko wazi wakaitisha uchaguzi sasa ktk hii ya RA wanataka barua hii ni double standard ya ajabu.
 
Watakuwa walitumia sharia ku-handle issue ya CUF na sasa wanatumia sheria ku-handle issue ya CCM. This is a true double standard.

Katika sharia, ukitangaza hadharani kuwa umemuacha mkeo hiyo inachukuliwa ni talaka na ukifanya nae tendo la ndoa unakuwa unazini, hutaruhusiwa kumuoa tena mpaka atakapoolewa na mtu mwingine na kuachika. Hivyo basi mbunge wa CUF kutangaza amejiuzulu hiyo ni kama talaka na jimbo litachukuliwa na mgombea mwingine atakayeshinda labla ugombee tena uchaguzi mkuu ujao.

CCM wanachukulia majimbo ya uchaguzi kama vile sehemu za kugawana keki ya taifa na kama mpinzani akichukua jimbo wanamuona kama mzamiaji kwenye sherehe, hivyo akitoka na kusahau kadi haruhusiwi kuingia ukumbini tena. Kwa CCM wenyewe kwa wenyewe wanajiona wana haki ya kushikilia ubunge, na kwa kuwa wanasema kuwa RA kawashtua kuachia ubunge (Kauli ya Lowassa), huenda kuna effort ya kumtaka abadili uamuzi wake inafanyika nyuma ya pazia, na kujidai kuwa wanasubiri barua. Maana uchaguzi mdogo kwa sasa si jambo la kuifurahisha CCM, maana wanajua fika kuwa watahitaji nguvu ya ziada ya pesa na dola kujitangazia ushindi.
 
Kwani inachukua mda gani kwa tume kutangaza na mpaka uchaguzi kufanyika?
sidhani kuwa kuna muda maalum lakini inaelekea ccm huwa ina play a certain role ktk kuitisha uchaguzi wakiangalia upepo unakwendaje
naamini mpaka wamemruhusu kujiuzulu one would think that they are confident to retake the seat but the delay tells us something must be wrong. RA amesema kuwa ametuma barua kwa m-kiti wao wa taifa lakini ccm wanadai hawana taarifa. naamini kama mpinzani angekwenda
kwenye TV akafanya aliyoyafanya RA basi the next day tume ingetangaza kiti kiko wazi. there is double standard na hii inadhiirishia jinsi tume
ya uchaguzi kwa kiwango gani kuwa sio huru na tusubiri kuona vituko vya tume vingi zaidi wakati wa uchaguzi.
 
Je kuna uwezekano wa RA kukanusha na kuendelea kuwa Mbunge?,na kama kaenda Public na baadae kukanusha kuna sheria inayombana?
 
Inashangaza kuwa kwanini tume ya uchaguzi mpaka leo haijatangaza kuwa kiti cha ubunge cha IGUNGA kiko wazi
kama mnakumbuka kuna mbunge mmoja wa CUF alikuwa anaitwa salum msabaha alijiuzulu kwenye television kama RA hivi hivi na baadaye
kukanusha na kudai kuwa alilazimishwa kujiuzulu lakini tume ya uchaguzi ilisema kuwa ameshatangaza kwenye TV that is enough evidence na kutangaza kuwa jimbo liko wazi wakaitisha uchaguzi sasa ktk hii ya RA wanataka barua hii ni double standard ya ajabu.

Mkuu Msabaha alikuwa Mbunge wa Jimbo gani vile?
 
Je kuna uwezekano wa RA kukanusha na kuendelea kuwa Mbunge?,na kama kaenda Public na baadae kukanusha kuna sheria inayombana?

Najua logic inakataa ila watacheza na mambo mengi likiwemo ni hilo la kuwa hajaandika barua; kisha alikuwa amejisikia kudhalilishwa sana hivyo akachukua uamuzi wa haraka na kisha wasema wapiga kura wake wameonyeshwa kusikitishwa na wamemwomba sana abadili uamuzi na hivyo na yeye kwa kushauriana na wenzake ameona asiwaangushe watu wa jimbo lake. Full stop! Is that not enough. Imagine I am RA and you are the public.
Na hilo likipita (Nasema kwa masikitiko makubwa): RA atarudi na nguvu kubwa ajabu ambayo hakuna wa kumzuia. Atafanya apendavyo bila kusutwa na yeyote. [Naomba kutoa utabiri]
Tukumbuke tu kuwa pacha mwingine (EL) ameshasema anasikitishwa na uamuzi wake wa kujiuzulu.
 
Mimi sina wasiwasi CCM na NEC wamekalia ncha ya mkuki hawawezi wakala matapishi yake
RA keshatapika basi iliyobaki wazoe.
 
Najua logic inakataa ila watacheza na mambo mengi likiwemo ni hilo la kuwa hajaandika barua; kisha alikuwa amejisikia kudhalilishwa sana hivyo akachukua uamuzi wa haraka na kisha wasema wapiga kura wake wameonyeshwa kusikitishwa na wamemwomba sana abadili uamuzi na hivyo na yeye kwa kushauriana na wenzake ameona asiwaangushe watu wa jimbo lake. Full stop! Is that not enough. Imagine I am RA and you are the public.
Na hilo likipita (Nasema kwa masikitiko makubwa): RA atarudi na nguvu kubwa ajabu ambayo hakuna wa kumzuia. Atafanya apendavyo bila kusutwa na yeyote. [Naomba kutoa utabiri]
Tukumbuke tu kuwa pacha mwingine (EL) ameshasema anasikitishwa na uamuzi wake wa kujiuzulu.
CCM si wajinga kiasi hicho hawawezi kufanya kosa hilo Nape ataficha wapi uso wake
kwanza ndio watakuwa wamewapa wapinzani mchongo.
 
Je kuna uwezekano wa RA kukanusha na kuendelea kuwa Mbunge?,na kama kaenda Public na baadae kukanusha kuna sheria inayombana?
Kwa serikali ya magamba na tume yake ya uchaguzi inawezekana maana sidhani kama sheria imesema chochote kuhusu kitu kama hiki huenda iko silent. Hapo ndo nitacheka mwenzenu mpaka tumbo liniume. Nadhani maana ya kujivua gamba limaanisha kuondoka kwenye vyeo vya ccm tu ndo maana wanashangaa kwa RA kuachia mpaka ubunge.

Kama RA alifanya hivyo kwa kutekeleza kujivua gamba basi huenda aka recall kuachia ubunge na ndo itakuwa kichekesho au atagombea tena mwenyewe. Lakini kama ameondoka kwa maana ya kuudhika basi ataachia mpaka kila kitu hata kama alikuwa anakidai ccm ataomba hela yake na pengine atahama nchi. Kama kujivua gamba kuna maana ya kuachia ngazi ccm peke yake basi bado wanayo kazi maana sisi wananchi hatuathiriki na vyeo vya ccm bali serikali. Kama mtu hataachia vyeo serikalini na kushitakiwa kwa maovu yake basi wanancheza kiduku tu hapa.

Kinachotakiwa ni kwa gamba
1. Kuondoka ccm
2. Kuondoka serikalini kama wapo
3. Kufikishwa mahakamani
4. Kurejesha mali yote aliyotuibia.

Pasipo kufanya haya mambo manne basi hii itakuwa ni kucheza kiduku tu. Kama wanatupiga changa la macho kwa kuelewana na hawa mafisadi wabki underground fighters hii itakula kwao.Hata hivyo lakini ccm ikiamua kufanya kitakachotokea ni kwamba
1. Itapoteza ufadhiri wa mafisadi kitu ambacho ni muhimu kwa magamba ili waendelee madarakani
2. Kupoteza waumini na washabiki wengi ambao walikuwa wameng'ang'ania ccm kwa sababu kulikuwa na mgao wa pesa.
3. Mpasuko mkubwa utatokea maana mafisadi wataondoka na waumini na washabiki wao ambao ni kundi lenye nguvu kubwa especially la EL.

My conclusion is that, there is no way ccm escape the big fall in a near future. They missed the timing and therefore there is no way they can catch up again. This should have happened five years back when Jk just come into power! Jk was and is benefiting from this system so has no credibility to abolish itWe need a president or institutions which will declare from his/her/its inception to completely overhaul the system ground up. Let's sit back and watch kiduku cha magamba!
 
salum mbarouk msabah alikuwa mbunge wa mkunazini huko zanzibar kwa ticket ya CUF kama sikosei ilikuwa mwaka 1995.
tume ilitangaza uchaguzi mara baada ya msabah kujitokeza kwenye TV na hata alivyokanusha the next day TUME ilikataa kuwa
kwa kuwa ameshangaza kwenye TV hiyo pekee inatosha.
 
Wanajamvi hebu tujikumbushe hizi ibara za katiba yetuili tujue kinachotokea

Ibara ya 76
.- (1) Kila mara baada ya Bunge kuvunjwa, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika majimbo yote ya uchaguzi.
(2) Hali kadhalika, kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge (ikiwepo kujiuzulu-msisitizo ni wa kwangu)

Ibara ya 149.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, Naibu Waziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa madaraka ya kazi yake, aweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiliwa sahihi kwa mkono wake, kwa kufuata masharti yafuatayo:… (d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.
(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku ile ambayo taarifa yake ya kjiuzulu itakapopokelewa na mtu anayehusika …"

Sasa kinachosubiriwa hapo ndiyo hiyo taarifa ya kujiuzulu, ili Speaker aitaarifu tume
 
msabaha alitangaza na alimwandikia spika MSEKWA baadaye akaja sema alilazimishwa wakati barua imeshamfikia spika.......SIO KUTANGAZA PEKEE
BE FAIR KIDOGO UNAPOYAFUATA MAWAZO YAKO
 
Wanajamvi hebu tujikumbushe hizi ibara za katiba yetuili tujue kinachotokea

Ibara ya 76
.- (1) Kila mara baada ya Bunge kuvunjwa, kutakuwa na uchaguzi wa Wabunge katika majimbo yote ya uchaguzi.
(2) Hali kadhalika, kutakuwa na uchaguzi wa Mbunge katika jimbo la uchaguzi, ikiwa kiti cha Mbunge yeyote aliyechaguliwa kuwakilisha jimbo hilo kitakuwa wazi kwa sababu nyingine yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge (ikiwepo kujiuzulu-msisitizo ni wa kwangu)

Ibara ya 149.-(1) Mtu yeyote mwenye dhamana ya kazi yoyote iliyoanzishwa na Katiba hii (pamoja na kazi ya Waziri, Naibu Waziri au Mbunge, isipokuwa Mbunge ambaye ni Mbunge kwa mujibu wa madaraka ya kazi yake, aweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa iliyoandikwa na kutiliwa sahihi kwa mkono wake, kwa kufuata masharti yafuatayo:… (d) iwapo mtu huyo ni Mbunge, basi taarifa hiyo ya kujiuzulu ataiwasilisha kwa Spika.
(2) Mtu aliyetoa taarifa ya kujiuzulu kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo ya (1) ya ibara hii, atahesabiwa kuwa amejiuzulu tangu siku ile ambayo taarifa yake ya kjiuzulu itakapopokelewa na mtu anayehusika …"

Sasa kinachosubiriwa hapo ndiyo hiyo taarifa ya kujiuzulu, ili Speaker aitaarifu tume
Kifungu hiki ndicho nilichokosa jana nikaanzisha ile thread ya Katiba ya Tanzania- Rostam anauachaje ubunge. Nashukuru nimeelimika sana. Huenda Rostam hata hii KATIBA hana au hajawahi kuisoma kabisa. Jana alipoulizwa alisema amemwandikia Mwenyekiti wake wa CCM. Aelekezwe cha kufanya ili tuendelee na mambo mengine muhimu ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom