Mwl nyerere kumsaidia kabila kushika dola!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwl nyerere kumsaidia kabila kushika dola!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MTAZAMO, Oct 9, 2012.

 1. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Wanabodi ,

  Hii nimeitoa kwenye mtandao unaoitwa wiki.answers.com.Lengo si kuleta takwimu za kijeshi zilizotolewa kule bali madai juu ya Baba wa Taifa Mwl Julius K.Nyerere kuwasaidia akina Kabila na familia yake kushika Dola.
  Mwl Nyerere wakati ule hakuwa Rais wa Tanzania nashangaa mtandao huu kumtaja mtu alisiyekuwa na nguvu za Kidola eti kuwasaidia akina Kabila.

  Vyovyote vile nafikiri ni vizuri tukiweka sawa historia ili isipotoshwe kirahisi hasa kwenye mitandao inayopata nguvu kila kukicha.Hii hapa nukuu


  "6.Tanzania: Tanzania has the most powerful army in East Africa; The TanzaniaPeoples' Defence Force (TPDF) (Swahili: Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)the one defeated Idi Amin of Uganda with big help form Muammar Al-Gaddafi ofLibya and . The Palestine Liberation Organization (PLO) The Tanzania People'Defence Force includes Land Forces Command, Naval Command, Air Force Command,and MilitaryIntelligence. Julius Kambarage Nyerere (The first Tanzania'sPresident) prepared president Laurent Desire Kabila of DR Congo to take overthe powerful Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu WA Zabanga; also prepared his sonJoseph Kabila. Tanzania has trained Congolese solders in Tabora and Kigomaregion for Kabila to return in Congo and take over power. Both Kabilas fatherand son were schooled and lived most of their lives in Tanzania beforereturning to Congo. Tanzania Also prepared Yoweri Kaguta Museveni who alsoschooled and lived in Tanzania before the Tanzania and Uganda war that resultedin defeating Dictator Idi Amin. Most Uganda leader got help from Tanzaniabefore becoming leaders. This includes: Tito Lutwa Okello, Yusuf Kironde Lule,and Bazilio Olara-Okello. Recently, Tanzania did not want to send his soldersin Somalia but offer training to Somali solders who will soon return to protecttheir country. Tanzania sent 924 soldiers to lead the African Union Solders inComoros's Island to take Colonel Mohamed Bacar of Anjouan off power. Tanzaniahas the 3rd largest army in number troops after Ethiopia, and Eritrea, andrecently considered the second in equipment after Kenya, but with more welltrained troops. The recent estimation shows that Tanzania is the country inEast-Africa followed by Ethiopia."

  Je kuna ukweli hapa wakuu hasa wakongwe wa historia hapa JF?
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mnataka kuwatisha majirani akina Joyce.lol!
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Mkuu Joyce anatujua vizuri tu,lakini unadhani ni kweli Mwl Nyerere aliwaandaa Kabila and Son kushika Dola Congo?
   
 4. MWILI NYUMBA

  MWILI NYUMBA JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 819
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Source ni ipi mkuu? Mbona wametupa sifa tusizostahili?
   
 5. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Mkuu taarifa za JWTZ zinaweza kuwa kweli kwa asilimia kubwa lakini kilichonishangaza ni Nyerere kuhusishwa na Kabila kushika Dola!
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tupatie source please!
   
 7. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,339
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  Nadhani wengi wenu mmezaliwa juzi hapa hamjui historia ya Tanzania na Congo. Ukweli ni kwamba Raisi wa kwanza wa Congo DRC, Patrice Lumumba, alikuwa kipenzi cha Nyerere kwa kuwa na mtazamo sawa na Nyerere uliolenga kwenye misingi ya ujamaa (sio ukomunisti). Lumumba alikuwa ni viongozi wa walioweka sana maslahi ya waafrika mbele na waliopinga kuyumbishwa na mataifa ya kizungu.

  Marekani walimuona kama mwenye mwelekeo wa kikomunisti, na kwa kumtumia Mobutu, alieyekuwa Mkuu wa Jeshi la Zaire wakati huo, CIA walimuua Lumumba kifo cha kikatili sana na Mobutu kuwa raisi wa Zaire.

  Kabila alikuwa kiongozi wa karibu sana na Lumumba (waziri kiama sikosei). Hivyo kabila na wenzake fulani walikimbilia Tanzania ambako Nyerere aliwapokea na kuwapa hifadhi, pamoja na nyumba za kukaa. Nadhani pia walikuwa wakipewa living allowance na serikali kwa muda waliokuwa Tanzania. Mwanzoni waliishi nyumba za serikali, baadaye walikuwa na nyumba zao wenyewe.

  Kipindi fulani ilionekana kama Mobutu ameanza kuwa mtu mwema, hivyo aliwaambia kina Kabila warudi nyumbani Zaire ili washirikiane kuendeleza nchi. Nyerere aliwaambia kinaKabila msimwamini huyu mtu. Mwenzake kabila (jina nimelisahau) aliyekuwa pia anafadhiliwa na Tanzania aliamua kurudi Zaire, ambako kama Nyerere alivyokuwa amehisi, aliishia kuuwawa na Mobutu.

  Hivyo Kabila aliendelea kukaa Tanzania hadi kipindi ambacho Nyerere alikubaliana naye kwamba kilikuwa wakati muafaka wa kuanza mapamabno rasmi kumtoa Mobutu. Wakati huu Nyerere hakuwa raisi, ila ni kweli alifanya kila awezacho kumsaidia Kabila katika ku-mobilize na kuanzisha mapambano dhidi ya Mobutu. Inasemekana Nyerere alimwezesha Kabila kijeshi kwa kuwatumia kina Kagame na Museveni. Sidhani kama askari wa JWTZ walihusika moja kwa moja katika vita - labda kwa ajili ya logistics tu.

  Hatimaye Mobutu aliondolewa. Na kweli Nayerere akawa viongozi wa kwanza kualikwa na Kabila kutembelea Zaire iliyokombolewa. Nyerere akaendelea kumpa Kabila ushauri mablimbali, pamoja na kumwambia akatae kulipa madeni ya nje yaliyoachwa na Mobutu kwa kuwa hizo fedha hazikusaidia Wa-Zaire bali ziliingia mfukoni mwa Mobutu.

  Unfotunately Kabila aliuwawa tena, na kwa mara nyingine inaonekana kama CIA/Marekani walihusika. Mfukoni mwa kijana aliyemuua Kabila kulionekana business card ya aliyekuwa military attache wa ubalozi wa Marekani pale Kinshasa, ambaye alikuwa Kanali mwanamke. Huyu military attache aliondoka Zaire siku hiyo hiyo Kabila alipouwawa.
   
 8. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Ndiyo. Delegation yao ilifika hapa Msasani,na nakumbuka kumsikia Mwalimu ansema ''Oh,so you want to give me a step by step account of what you want to do there? That's okay with me.'' [Yaani,Mwalimu alifurahi walipomwambia kwamba he would not just be watching it on TV,they would come to him for advice]all throughout the march to Kinshasa walikuwa wanawasilana na Mwalimu alikwenda katika meetings zao,especially the last one in which Mobutu came in a wheel chair to hand over power to Laurent Kabila. Mobutu was in a wheel chair. Kwa hiyo hawa watu they just took power from a decrepit man.
   
 9. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Kamanda pamoja na kuzaliwa siku nyingi kidogo lakini nondo hizi inabidi uwe mfuatiliaji haswa wa mambo.Nyanga kama hizi ndio huweka mambo mengi sawa hasa kwa wanaotafuta ukweli kwenye mitandao.

  Mkuu Synthesizer kwanini Mkapa hatajwi mara nyingi kwenye harakati hizi wakati ndie alikuwa amri jeshi mkuu?
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,228
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  ndiyo, aliwaandaa
   
 11. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,339
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  Mtazamo, mambo ya Mkapa na mahusiano yake na viongozi wengine wa Afrika we acha tu. Labda Comorro, ambako hata hivyo Nyerere alikuwa ameshaweka foundation. Mkapa alikuwa na tatizo moja, thinking alikuwa as intelligent as, or even more intelligent than Nyerere, na pia the most intelligent president in Africa. Nadhani utaona wazi kwamba alikuwa na assumption kwamba he was more intelligent than all other Tanzanians. Ninaamini ilifika mahali Nyerere ali-regret kum-support Mkapa kuwa raisi wa Tanzania. Lakini pia Nyerere was very disappointed na Mwinyi. That was Nyerere, mzalendo wa Afrika to the inner core.
   
 12. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Pengine ndio maana Gen Mboma alikuwa mtu wa kwanza kuiunga mkono serikali ya Kabila kabla hata ya Rais wake mara tu baada ya mapinduzi!
   
 13. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hapo msisahau kumsoma Profesa mmoja wa kiCongo akiitwa Wamba Dia Wamba alikua anaiva sana na mwalimu wakati huo anafundisha UDSM ila baadaye akaingia kwenye mtego wa kina Kagame
  All in all ni kweli Mwalimu aliwasaidia kina Kabila japokua hakuaa Amiri jeshi ila alikua na nguvu sana kwenye majeshi bado
   
 14. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kwa mawazo yangu, sidhani kama Mkapa anajiona/alijiona intelligent kuliko watanzania wengi au zaidi ya Nyerere. nadhani Mkapa alikuwa anahangaishwa na inferiority complex. kwa wanaomjua na wanaolijua cabinet ya mwalimu wakati ule, Mkapa was amongst the most sidelined ministers. ilikuwa kama vile alikuwepo wepo tu. non comittal non influencial nobody. kuwepo na kutokuwepo kwake ilionekana kama kawaida. more so kwa vile pia alionekana kutekwa sana akili na mkewe na kujikuta anaishi/kwenda zaidi moshi kuliko kwao. naambiwa alikuwa na bifu na wazazi wake kutokana na kuonekana kama aleoewa yeye. yote haya, kama ni ya kweli for sure yalimwongezea zile inferiority complex zake.

  kwa wanaojua Mkapa alikataa kata kata kugombea urais kama si shinikizo la mwalimu. nadhani pia mwalimu alikuwa impressed na mkapa sio kwa vile ni mwanafunzi wake tu bali pia ile hali ya kutokuwa na 'matukio' kwenye maisha yake. lkn kumbe Mkapa hakuwa na 'matukio' kwenye maisha yake kwa vile alikuwa anajiregard kama inferior kwa hiyo kwake ni bora kujifungia ndani na kuwaacha wanaotaka makubwa wahangaike nayo.

  nadhani Mkapa was not at the fore front kuutambua utawala wa Congo/Zaire mapema hivyo kwa vile alikuwa bado hajajijua afanyeje. Mkapa alikuja kubadilika na kuonekana mkali mara tu baada ya Mwalimu kufariki (huenda zile tuhuma za kuhusika kwake na ule msiba kimazingira zinaanzia hapa). Tukumbuke chini ya katiba, rais wa Tz ana mamlaka kubwa sana na ana nguvu nyingi sana. Mkapa hakuwa na uhuru wa kuyatumia mamlaka yake wakati Mwalimu akiwa hai manake alijua jinsi Mwalimu alivyom-ridicule Mwinyi wakati wa utawala wa Mwinyi kwa matumizi mabaya ya mamlaka na udhaifu wa katiba. Mkapa ainawezekana aliona project ya COngo kama ya Mwalimu zaidi kumwadhibu Mobutu kama yeye alivyomwaibisha Lumumba. Hivyo Mkapa kwenye vurugu ya Congo/Zaire hakuwa na mashiko yoyote zaidi ya kumuunga mkono Godfather wake. Nyerere na Mobutu hawakuwa na wasingeweza asilani kuwa marafiki kutokana na historia zao na perspectives zao za maisha na Afrika kwa ujumla
   
 15. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,339
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  Manumbu, nakubaliana nawe 100% Mkapa alibadilika baada ya Nyerere kufa vibaya mno. Basi kama ni inferiority complex ni wakati Nyerere akiwa hai. Lakini tusisahau Nyerere aliwahi mpa wizara nyeti ya mambo ya nje kwa muda mrefu tu, kutia ndani wakati tukiwa na vita vya Kagera. Kumbuka ni Mkapa huyo huyo kama waziri wa mambo ya nje alikuwa anatumwa na Nyerere kupeleka ujumbe mzito kama ule wa kwenda kumwambia Banda wa Malawi wakati wa vita kwamba Tanzania ina uwezo wa kupigana vita kwenye frontline mbili - Kagera na Malawi, na bado tukakupiga! Unajua Banda kwa akili yake ndogo aliingiza kikosi cha wanajeshi waliokuwa pia na askari wa makaburu kule ziwani Nyasa akidhani wanajeshi wetu wote wako Kagera - kumbe Nyerere alikuwa ameshamwotea bwana, kulikuwa na tahadhari kubwa mpaka wetu na Malawi wakati wa vita vya Kagera. Jamaa waliuwawa na miili yao kuondolewa haraka, halafu Mkapa akatumwa kwenda kumpa ujumbe Banda.
   
 16. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  Kumbe Banda alitaka kutuvaamia kipindi tunapigana na Uganda?i never heard of this stori mkuu,mimi mtoto wa juzi juzi,embu funguka kama kuna la ziada.
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Banda alikuwa anatumiwa na Kaburu. Kumbuka wakati wa harakati za ukombozi Kaburu alikuwa anaingia Zimbabwe, Swaziland na Zambia kama apendavyo. Lakini lengo lake lilikuwa ni kushambulia kambi ya Nachingwea. Alishindwa.
   
 18. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Ni kweli. Pia Nyerere ndo aliyewakutanisha Laurent Kabila na Paul Kagame na kuwasaidia sana kuwa na mlengo moja wa kimapinduzi.

  Chanzo ni mimi mwenyewe. Wakati huo nilikuwa insider.
   
 19. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,142
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  thanxs mkuu,nashukuru sana kwa ufafanuzi wako,watu kama nyinyi ndio mnazidi kufungua akili zetu,msichoke pale tutakapohitaji msaada wenu wa kimawazo ktk kuweka kumbukumbu zetu sawa
   
 20. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Naikumbuka hii wakati wa vita ya kagera. tena zilianza kampeni/propaganda kuwa vita ya kagera ilianzishwa ili kudhoofisha mapambano ya ukombozi kusini kwa afrika. nadhani ndo wakati Banda alikuwa ameleta chokochoko zake ziwa nyasa. siku zote jamaa alikuwa analiota ziwa lote liwe lake (kama ilivyo sasa). nakumbuka tuliwahi kupigananae vita ya saa 3 nadhani ndani ya ziwa, miaka ya 60s na akafyata mkia. na nyimbo zikatungwa na mashujaa wetu "Bandaa wa Malawi, katuvalia ngozi ya simba, kututishia watanzani...Hatujali! Hatujali!"

  Kuhusu Mkapa, pre and post nyerere mkapa was/is a very different person. najua mikwaruzano ilishaanza anza na mwalimu hasa kwenye ubinafishaji. mwalimu alishaanza kupiga kelele kuhusu kubinafsisha mashirika yenye kutengeneza faida akitolea mfano wa NBC na TTCL. Mkapa alishakuwa focused kubinafsisha NBC kwa uwezo wake wote. iko siku nchi ikiwa chini ya Upinzani tutajua ukweli mzima wa sakata ya ubinafsishaji wa NBC na kama ilikuwa chanzo cha 'kuondolewa' mwalimu ili uendelee kama ulivyopangwa...kuwapa ABSA bure! Mwalimu pia asingekubali tuwe na mikataba kwenye migodi yetu kama ilivyofanywa na Mkapa.

  Binafsi sishangai Mkapa kugeuka mbogo baada ya Nyerere kufariki. mtu mwenye inferiority complex akipewa madaraka makubwa anakuwa mbogo kupitiliza ili kufidia/kuficha udhaifu wake!

   
Loading...