Mkweliii
Member
- Apr 15, 2025
- 14
- 5
Tunapoelekea kuzindua kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika siku 61 zijazo, tume huru ya Taifa ya uchaguzi {INEC} ikiwa imeteua wagombea 17 wa kiti cha urais, chama cha Mapinduzi {CCM} kina silaha 3 muhimu katika uchaguzi mkuu huu wa 2025, ambazo ni;
1. Rekodi ya utekelezaji wa ilani ya 2020-25 katika mikoa yote 31, wilaya zote 184, kata zote 3960, vijiji vyote 12,333, mitaa yote 4269 na katika vitongoji vyote 64,274.
2. Dira mpya ya maendeleo kupitia ilani ya uchaguzi ya 2025-30 iliyozinduliwa rasmi Mei 30, 2025 na kushikanishwa moja kwa moja na dira ya maendeleo ya miaka 25 {dira 2050} pamoja na
3. Msingi mpana wa wanachama wanaofikia 13,000,670 kwenye kanzidata za wanachama.
Idadi hii ya wanachama ni kubwa kuliko ushindi wa juu wa kura waliowahi kuupata wapinzani katika historia ya chaguzi za nchi yetu ambapo ushindi mkubwa waliowahi kuupata wapinzani ni wa jumla ya kura milioni 6.07 sawa 39.97% ya kura zote zilizopigwa katika uchaguzi wa mwaka 2015 uliompa ushindi Hayati John Pombe Magufuli kwa kura milioni 8.8 sawa na 58.47% ya kura zote.
Kwa maandalizi makubwa na ya kisayansi yaliyofanyika chini ya uenyekiti wa Dr. Samia Suluhu Hassan, chama chetu sasa kinakwenda kushiriki uchaguzi mkuu wa 29 Oktoba kikiwa kina misingi ya ushindi mkubwa na wa kihistoria unaotarajiwa kupita ushindi katika chaguzi zote 6 zilizowahi kufanyika tangu 1995.
Hii ni sawa na kusema, tunaingia kwenye uchaguzi mkuu huu wa 7 tangu mfumo wa vyama vingi kuanza tukiwa na uwezekano mkubwa wa kupata ushindi mkubwa kuwahi kutokea katika chaguzi zote zilizotangulia.
Katika uchaguzi wa mwaka 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na 2020, CCM ilipata ushindi wa kiti cha urais kwa kura 61.8%, 71.7%, 80.3%, 62.8%, 58.8% na 84.4% mtawalia.
Katika uchaguzi wa mwaka huu wa 2025, na kutokana na takwimu hizi za wanachama waliosajiliwa katika mfumo wa chama wa kidigitali, ina maanisha kuwa CCM ina mtaji wa kura 13,000,670. Kazi iliyosalia ni kuhamasisha wanachama hawa wanapiga kura kikamilifu ifikapo Oktoba 29, 2025. Kuhamasisha Watanzania wanakiunga mkono Cha Cha Mapinduzi ndiyo jukumu kubwa linalofuata kwa miezi miwili ya kampeni ya uchaguzi huu, kama alivyosema Mwenyekiti wa CCM Taifa na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dr. Samia Suluhu Hassan wakati akizindua ilani ya uchaguzi mkuu wa 2025 mnamo Mei 30 jijini Dodoma.
Uthibitisho wa madai yangu ya kuwa CCM itapata ushindi mkubwa kuliko chaguzi zote zilizotangulia unaweza kuungwa mkono kwa misingi minne ifuatayo;
1. Rasilimali {watu na vitu} za chama. Hakuna asiyejua kuwa, ukiacha namba ya rasilimali watu {idadi ya wanachama} kuwa kubwa ukilinganisha na wanachama wa vyama vingine hapa Tanzania, chama cha Mapinduzi pia ni chama chenye utajiri wa mali unaokadiriwa kufikia thamani ya trilioni 2 {Majengo, uwekezaji na vifaa kwa kutaja vichache}, na kwamba, ni misuli hii ya uchumi inayokisaidia chama kufanikisha mazoezi ya kampeni, mikutano, maendeleo ya TEHAMA, usafirishaji na ugharamiaji wa mipango ya ushauri wa masuala uongozi na utawala. Mambo haya yote yanahitaji rasilimali ili yaweza kufanyika kwa ufanisi. Sababu hii inakifanya Chama Cha Mapinduzi kumudu siasa za ushawishi si tu kwa miaka zaidi ya 60 iliyopita bali kwa miongo mingi ijayo. Mathalani kwenye uchaguzi wa kura ya maoni uliohitimishwa tarehe 5 Agosti, 2025 zaidi ya wajumbe milioni 7 walipiga kura kuwachagua wabunge na madiwani katika majimbo yote 272 ya uchaguzi wa mwaka 2025. Wajumbe hawa pia, kimaheshabu ni wengi kuliko wanachama wa vyama upinzani kwa ujumla wao {rejea kura za UKAWA kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 zilizofikia milioni 6.07 kama kipimo cha idadi ya wapiga kura wao wa juu zaidi katika historia ya upinzani}.
2. Uzoefu wa kiuongozi na uratibu wa mifumo. CCM ni miongoni mwa vyama vya siasa vichache duniani vyenye uzoefu mkononi wa mrefu wa kuongoza serikali. Leo ni zaidi ya miaka 63 chama hiki kikiwa kinaongoza dola. Maana yake CCM ni chama kilichobahatika kufanya makosa mengi na kupata bahati ya kurekebisha makosa hayo kwa nyakati na mazingira yaliyotakikana kisiasa. Kwa maana nyingine CCM imejifunza mengi kutokana na makosa hayo. Sababu hii ndiyo iliyopelekea vyama vingi vya ukombozi kusini mwa jangwa la Sahara {MPLA cha Angola, SWAPO cha Namibia, ANC cha Afrika kusini, FRELIMO cha Msumbiji, ZANU PF cha Zimbabwe n.k} kukubali kujenga chuo cha uongozi pale Kibaha- Pwani, malengo makubwa ya chuo hicho yakiwa ni kuwaandaa viongozi wa taasisi mbaimbali katika nchi hizo. Hii ni sawa kusema CCM ni chama chenye heshima na umaarufu mkubwa barani Afrika. Kutokana na ujuzi wa mifumo ya kisiasa katika nchi hii, vyama vingi vya upinzani vimeundwa na wazee wa CCM, hata vile ambavyo baadhi ya wapinzani wamekuwa wakivitumia kupambana na CCM yenyewe.
3. Mafungamano na uhusiano wa kikanda na kimataifa wa vyama vingine vya kidunia. CCM ni chama rafiki wa serikali nzima ya Uchina, Urusi, Cuba na nchi nyingine katika bara la Ulaya, Asia na Amerika ya kusini. CCM imetumia mahusiano haya kujifunza mifumo ya usimamizi wa fedha, viongozi, teknolojia, ujenzi wa sera, tafiti na mifumo. Jambo ambalo limekisaidia chama kufanikisha uhuishaji wake binafsi kulingana na zama. Uimara wa vyama na nchi rafiki kimifumo na kifedha, CCM umekuwa ikinufaika na masuala hata yanayohusu fedha. Tofauti na vyama vingine hapa nchini ambavyo havijafanikiwa kutengeneza mahusiano na vyama/nchi zenye nguvu kifedha, kiushawishi na kiteknolojia. CHADEMA, chama ambacho kimefikiriwa kuwa ni chama kikuu cha upinzani kwa muongo mmoja kina vyama rafiki kutoka mataifa mengine ambavyo ni dhaifu katika maeneo hayo niliyoyataja kikiwemo chama cha Patyja BPF cha Belarus, chama cha New Rights cha nchini Georgia, Nationalist Party cha Malta, chama cha Democratic Turnhalle Alliance cha nchini Namibia na vyama kama hivyo ambavyo navyo havina ukomavu wa kisiasa ama wa kifedha kama ilivyo kwa vyama washirika wa CCM.
4. Mpango thabiti wa kuachiana madaraka {solid plan to relinquish power}. Tofauti na vyama vingine ambavyo uongozi wake umekuwa wa kisultani, CCM ina succession plan inayotoa unafuu wa kuendelea kubaki salama kwa miaka mingi ijayo. Wakati Hayati Mwl. Nyerere anaachia madaraka wapo waliodhani kuwa CCM itakosa mwelekeo sahihi lakini chama kiliendelea kuwa salama chini ya uenyekiti wa Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, na baadae chini ya Hayati Mzee Mkapa chama kiliimarika tofauti mafikirio ya wengi. Vilevile mwaka 2005 alipokabidhiwa kijiti Mzee Kikwete mambo yaliendelea kuwa bora hadi kipindi cha Hayati Mzee Magufuli. Wapo waliofikiri baada Magufuli chama na nchi vingeyumba lakini uwepo wa Rais wa sasa, Mama Samia Suluhu Hassan umethibitisha kuwa CCM itaendelea kuwa bora mara dufu, na sasa chini ya utawala wa Mama Samia, Chama Cha Mapinduzi kinakwenda kupata ushindi mkubwa kuliko ushindi wowote uliowahi kutokea katika chaguzi zote sita zilizotangulia. Suala hili la kupishana kwenye madaraka na chama kubaki salama limeshindikana kwa vyama vingine nchini, tukipigia mfano wa NCCR ya Mzee Mbatia, TLP ya Marehemu Mzee Mrema, UDP ya Mzee John Cheyo, UPDP ya Mzee Dovutwa, CUF ya Mzee Lipumba, ACT ya Marehemu Mzee Maalim Seif na hata hata leo, CHADEMA ya Mzee Mbowe. Kuondoka kwao madarakani kwa viongozi hawa au kuzeeka kwao huhusiana moja kwa moja na vifo vya vyama vyao, hali ambayo ni tofauti kwa Chama Cha Mapinduzi, ambacho huimarika zaidi kila baada ya power transition kufanyika.
Ukweli mchungu lakini unaopaswa kuvumiliwa na kila mpinzani ni kuwa, katika vyama vyote 19 vyenye usajili wa kudumu, hakuna chama chenye misuli ya kuiongoza Tanzania isipokuwa Chama Cha Mapinduzi {CCM} tu.
29 Oktoba nenda kaweke TIKI kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye nafasi ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, tia TIKI nyingine kwa Dkt. Emmanuel Nchimbi kwa nafasi ya mgombea mwenza wa urais na piga TIKI nyingine nzuri kwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, mgombea urais wa Zanzibar.
Baada ya kufanya kazi nzuri hapo, kwa wewe mwenzagu wa hapa Biharamulo, nakusihi ukaweke TIKI kwa Mhandisi Ezra John Chiwelesa kwa nafasi ya mgombea ubunge na kwa madiwani malizia kuweka TIKI kwa kila mgombea udiwani wa CCM aliye katika karatasi ya kura utakayopewa na msimamizi mapema 29 Oktoba.
Mwl. Mbelwa Petro,
+255759886429,
Biharamulo.
28 Agosti, 2025.