Mwizi Maarufu Anayepapatikiwa na Wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwizi Maarufu Anayepapatikiwa na Wanawake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  Tony Musulin Thursday, November 26, 2009 2:33 PM
  Mwanaume mmoja wa nchini Ufaransa aliyetumia akili zake kuiba gari la benki kuu ya Ufaransa likiwa na pesa taslimu euro milioni 11 bila ya kutumia silaha yoyote, amejipatia umaarufu wa ghafla na amekuwa kipenzi cha wanawake kiasi cha mamia ya wanawake kutaka kuolewa naye Tony Musulin mwenye umri wa miaka 39, oktoba tano mwaka huu, alitoroka na gari la benki kuu ya Ufaransa likiwa na pesa taslimu kiasi cha euro milioni 11.6.

  Tangia alipoanza kutafutwa kila kona nchini Ufaransa mwezi uliopita kabla ya kujisalimisha mwenyewe tarehe 16 mwezi huu, Musulin amejipatia umaarufu wa ghafla na anaokena kama shujaa miongoni mwa watu.

  Mamia ya wanawake wamekuwa wakiwasiliana na wakili wake wakimtumia barua za kuelezea mapenzi yao kwake wakipigania kuolewa naye.

  Musulin anaonekana kama shujaa nchini Ufaransa kwa jinsi alivyopangilia mpango wake wa kuiba euro milioni 11.6 mchana kweupe bila kutumia hata bunduki.

  Kundi la washabiki wa Musulin liliundwa kwenye Facebook likijulikana kama "Tony Musulin fan club" likiwa na wanachama zaidi ya 2,000.

  Fulana zenye picha ya Musulin na maandishi ya "dereva bora wa mwaka 2009" zinauzwa kwenye internet kwa euro 22 na zinanunuliwa kwa wingi.

  Washabiki wake wanasema kuwa Musulin ni shujaa wao kwani hata kama akikamatwa atatupwa jela miaka mitatu tu.

  Musulin mwenye umri wa miaka 39 alikuwa mfanyakazi wa shirika la ulinzi lililokuwa likisafirisha pesa za benki kuu ya Ufaransa.

  Siku aliyofanya wizi huo, Musulin alikuwa na wafanyakazi wenzake wawili walipoenda kuchukua euro milioni 11.6 toka benki moja katika mji wa Lyon.

  Walipotoka kwenye benki hiyo walienda kwenye benki nyingine kwaajili ya kukusanya pesa zaidi toka kwenye benki hiyo lakini Musulin alibaki kwenye gari na kuwaacha wenzake waingie ndani kuchukua pesa hizo.

  Baada ya dakika chache wenzake waliporudi walikuta gari lililokuwa na pesa limetoweka na Musulin naye haonekani.

  Awali ilitangazwa kuwa majambazi wameliteka gari hilo huku Musulin akiwa ndani na msako mkali ulianza kulitafuta gari hilo.

  Haukupita muda mrefu walifanikiwa kulipata gari hilo likiwa limetelekezwa pembeni ya barabara lakini pesa zote zikiwa zimeibwa na Musulin akiwa hajulikani alipo.

  Baadae iligundulika kuwa Musulin ndiye aliyeiba pesa hizo akiwa peke yake bila ya kumshirikisha mtu yeyote na alikuwa amejificha sehemu isiyojulikana akiwa amezungukwa na viroba 49 vya pesa.

  Kabla ya kufanya wizi huo, Musulin alitoa pesa zake zote kwenye akaunti yake ya benki na kuchanachana nyaraka zake zote ili kuwafanya polisi wasimtilie shaka.

  Katika uchunguzi wao polisi walishangaa kuona kuwa Musulin ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa euro 2,000 kwa mwezi aliwezaje kununua gari aina ya ferrari la thamani ya euro 160,000 miezi sita kabla ya kufanya uhalifu huo.

  Walishangazwa zaidi kuona pia kuwa pesa alizozitoa kwenye akaunti yake ya benki siku chache kabla ya wizi huo ni zaidi ya euro 100,000.

  Musulin alijisalimisha mwenyewe polisi wiki iliyopita mjini Monaco na polisi walifanikiwa kuzipata euro milioni 9 kwenye gari lililokodishwa na Musulin.

  Euro milioni 2 hazijulikani zilipo na Musulin amekataa kusema chochote kuhusiana na pesa hizo.

  Marafiki zake wanasema kuwa Musulin alikuwa ni mfanyakazi hodari lakini alikuwa akilalamika mara kwa mara mshahara mdogo wanaolipwa na aliahidi siku moja benki zitakuja kumlipa.

  Musulin bado yuko rumande na huenda akatupwa jela miaka mitatu.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3617894&&Cat=2
   
 2. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu kweli ni kiboko!!!,
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,019
  Trophy Points: 280
  vp na wewe usha fika bei nini?
   
 4. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh...akija bongo anaweza ondoka na BOT......LOL!
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  umaarufu utaongezeka zaidi akiwa jela...............
   
Loading...