Bosco Laifa
Member
- Apr 25, 2018
- 18
- 14
Nawasalimu tena,
Haya mambo wakati mwingine huwa ni kwa neema tu za Mwenyezi Mungu. Leo tunaianza Jumapili kwa kumshukuru Mungu kwa ukuu wake upitao nguvu za kibinadamu. Ndugu yetu Mwita Waitara alikuwa Rais wetu pale UDSM miaka hiyo na amepambana katika maisha na leo, anakuwa Naibu Waziri TAMISEMI. Wizara ya TAMISEMI ina kazi kubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu. Ninaamini, uwezo wake katika uongozi utakuwa na tija kubwa na kuwa kivutio kwa watu wengi ndani na nje ya CCM. Vilevile, namwona WAITARA kuwa kivutio kwa wale ambao wanataka kuachana na wenzao ambako naona kuna tetesi punde zitakuwa habari kamili.
Binafsi, nampongeza sana Mheshimiwa Waitara kwa kuona mbali. Tunafanya siasa ila mwisho wa siku, watoto watulie, wale vizuri, nchi ipate maendeleo na kuepuka kadhia zisizo na tija. Nimemsikiliza mara kadhaa tangu ajiengue CHADEMA. Kuna mambo hebu tuendelee kujifunza maana. Kuondoka kwa Waitara, Milya na wengine kutaendelea kuitafakarisha Chadema kwa kiasi kikubwa. Hebu tusubiri kidogo, muda ni mwalimu mzuri sana. Tuendelee kuliombea taifa letu kuwa na umoja. Kyala Tununu!!