Mwisho wa upigaji? Mfumo mpya wa manunuzi

Mwisho wa upigaji? Mfumo mpya wa manunuzi

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
73,268
Reaction score
103,446
Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amesema utafiti mdogo uliofanyika juu ya mfumo mpya wa manunuzi umeonyesha kuwa zaidi ya Sh2 trilioni zitaokolewa kwa kutumia mfumo huo.

Dodoma. Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amesema utafiti mdogo uliofanyika juu ya mfumo mpya wa manunuzi umeonyesha kuwa zaidi ya Sh2 trilioni zitaokolewa kwa kutumia mfumo huo.

Chande ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 5,2022 wakati akichangia taarifa za Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC), Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).

Amesema zaidi ya asilimia 70 ya fedha za bajeti zinatumika katika manunuzi na hivyo kutokana na unyeti wa eneo hilo Serikali imechukulia hatua kuanzisha mfumo mpya wa manunuzi ili kuepuka changamoto.
“Sababu mfumo wa TANAePS (mfumo wa manunuzi), tuliokuwa nao si rafiki kwa matumizi ya watumiaji lakini kwa utoaji taarifa sahihi. Mfumo mpya faida nyingi sana, utaongeza uwazi kwasababu mfumo wa awali ulikuwa na usiri mkubwa sana ambao unapeleka mianya ya rushwa,”amesema.

Amesema lakini mfumo huo mpya utakuwa wa uwazi na watu wote watakuwa na uwezo wa kuupata, utaongeza uwajibikaji na utaweka bei katika ukomo wa bidhaa ili kuepuka manunuzi holela ambapo itapuka bidhaa moja kununuliwa kwa bei tofauti.

“Huu utakuwa mwarubaini pekee wa kuserve (kutunza) fedha za umma. Mfumo huu utaokoa zaidi Sh2 trilioni lakini utapunguza hoja za ripoti ya CAG kwa kuwa na matokeo mazuri. Tutaenda kujadili kuona wapi kuna upotevu wa mianya ya fedha kabla ya mradi kuanza,”amesema.

Ametoa wito kwa taasisi kujiunga na mfumo huo utasaidia manunuzi halali.
 
Mrongi ndugu yangu kunyonga hakujawahi kuwa suluhu ya matatizo hasa kama haya ya manunuzi na matumizi sahihi ya fedha za umma.....SWALA LA MSINGI NI SISI WOTE WAUZAJI,WANUNUZI,MAOFISA WENYE DHAMANA KATRIKA MNYORORO WAHATUA ZOTE KUMUOGOPA MUNGU,KUFUATA SHERIA ZOTE NA KUTOA NAFASI WAZI BILA UPENDELEOA KWA wote naoshiriki katika manunuzi.....nchi nyingi zimeweza na mimi nikuwepo huko na kuona SINGAPORE wameanza kutumia mifumo hii na wako vizuri mno mno na hawana mkopo wa WORLD BANK.IMF nk ns wako dunia ya kwanza bila idara ya mifugo wala kilimo.....tutembee na kutumia the best practice .....
 
Hata muweke mfumo gani,upigaji uwizi hauwezi isha
Mkitaka uwizi,upigaji,rushwa wa Mali,pesa za umma uioshe tungeni sheria ya kunyonga/kuuaaaa

Ova
Au sheria ya kufilisiwa, wewe na ndugu zako. Hii itasababisha wizi usiwepo
 
Watu wanatengeneza mpaka control namba feki itakuwa hyo m.bongo kwenye wizi anashika namba moja Africa pale south Africa na ujanja wao wote ila kwa m.bongo anapotea anajua kupigwa nje nje.
 
Back
Top Bottom