Mwisho wa Maalim Seif kwenye siasa

DIZZO MTAWALA

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
240
767
Maalim.jpg

Maalim seif simba wa vita aliyesarenda kirahisi kwa CCM ya Magufuli yes uchaguzi wa 2020 ulikuwa uchaguzi uliochafuliwa kwa makusudi na watawala baada ya kufanya uchafuzi wakahitaji kuhalalisha uchafuzi kwa kuwatumia waliochafuliwa ili kujihalalishia kwa jamii ya kimataifa na umma.

Kwanini Maalim amesarenda iko hivi uchaguzi wa mwaka 2000 uliopelekea mauaji ya 2001 na kuzalisha wakimbizi ambayo hayati mzee mkapa amekiri ni doa kwenye utawala wake na kwenye kitabu chake alisema kunahitajika kuwepo na tume huru ili mambo kama ya 2001 yasitokee tena mauaji ya 2001 yaliileta cuf na CCM mezani wakafanya muafaka kila chama kuna vitu walipata na vingine walikosa na hata chaguzi zilifuata baada ya hapo kulikuwa na maridhiano pia lakini kubwa kuliko ni maridhiano ya 2010 hapa na katiba kubadilishwa ili serikali ya mapinduzi kuwa shirikishi hii ilikuwa ni hatua muhimu kwa Wanzazibar.

Uchaguzi wa 2015 huu Maalim alishinda kwa wazi kabisa kwa kutarajia vile alivyoridhia 2010 kwa Shein alijua shein ataridhia baada ya kumshinda kwa uwazi kabisa mzee jecha akafanya aliyofanya uchaguzi ukarudiwa maalimu hakushiriki uchaguzi wa marudio bado aliendelea kuitafuta haki yake kwenye Jumuyia ya Kimataifa huku watawala wakamtengenezea mgogoro ndani ya cuf mwisho akaporwa chama chenyewe akaona isiwe nongwa akatafuta chama kitachobeba ajenda ya miaka mingi ya Zanzibar yenye mamlaka kamili akaangukia Act wazalendo huku akakutana na zitto ikawa shusha Tanga pandisha Tanga.

Hoja inakuja kwenye uchaguzi mkuu uliopita ambao kimsingi haukufanyika bali kura feki na uchafuzi mwingi tu na hata press ya chadema na act wazalendo waliuambia umma kuwa huu uchaguzi haukuwa huru na haki na kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za kininadamu walienda mpaka kufungua kesi ICC.

Sasa jana karidhia kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa kwa hoja dhaifu ya takwa la kikatiba huku kuna watu wameuwawa wameumizwa wametekwa hii ilikuwa kete muhimu.

Kwa maalimu kufanya maridhiano yenye haki sio ohh takwa la kikatiba kwani 2015 halikuwepo.

Mwisho maalim ameserenda ili kuitengenezea familia yake uwakika hata kama yy hatakuwepo hapo amerudi kwenye kanuni ya asili ya binadamu yaani ubinafsi maana yeye kukubali kwake kuingia Serikalini ni kuhalalisha waliopigwa au kuuwawa walifanyiwa haki kwa makosa yao kushiriki uchaguzi na jana amezika rasmi Zanzibar kuwa huru tena sasa hivi atashiriki sanaa inayoitwa kero za muungano.

Kwa anguko hili pia ni kisu kikali kwa Zitto Zuberi Kabwe nani atamwamini kwa watu waliosarenda bila kukaa mezani ili kupata suluhu

Safari njema ya utulizo simba maalim kwa kwenda kushiriki uchafuzi.
 
Maalim ajawai kuchuja kwenye siasa za Tanzania na Zanzibar.
Hapo nyuma alishawai kuwa makamo wa kwanza wa Rais kwenye serikali ya SUK na bado aling'aa mpaka alipoamua kususa baada ya uchaguzi wa 2015.
Miongoni mwa wanasiasa wanyumbulifu na wanaojua kucheza na akili za watu ni Maalim Seif na Zito Kabwe.
hata watoe boko kubwa kiasi gani wanajua kujipanga na wakarudi kwenye pick.
 
Maalim seif simba wa vita aliyesarenda kirahisi kwa CCM ya Magufuli yes uchaguzi wa 2020 ulikuwa uchaguzi uliochafuliwa kwa makusudi na watawala baada ya kufanya uchafuzi wakahitaji kuhalalisha uchafuzi kwa kuwatumia waliochafuliwa ili kujihalalishia kwa jamii ya kimataifa na umma
huyo mzee labda afe,bahati mbaya umeanza kupiga kura mwaka 2020
 
Back
Top Bottom