Mwisho wa dunia!

Mwisho wa dunia!

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
649
Reaction score
583
WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa kutisha unaonesha kuwa mwaka.....
2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika mfumo wa jua. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet,-


sayari iitwayo Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.

-ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI


Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.

-DALILI KWAMBA IPO JIRANI


Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu mbalimbali. Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la miamba midogo na vimondo kutokea angani.

-DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE


Wakati volcano zote duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia itafunikwa na giza nene na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.-

NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo sasa).-

WANASAYANSI WAPINGANA


Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya nyota.

-MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO


Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu. Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.-

BAADA YA NDOTO


Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru). Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12, wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12. Nibiru.

-IMANI NYINGINE ILISEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014



Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini New York, Marekani ulisema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu. Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia. Walisema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.-

WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA



Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na ni siri ya Muumba. Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship la Zakaria Kakobe.-

FREEMASON WABARIKI



Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja. Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba, upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni wakiwa wengi.-

MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA



Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au ikapita kidogo). Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000. Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi kutokea
 
Kikubwa ni kuwa tayari muda wote kiimani na matendo, Mungu ndiye mwamuzi kwani sayansi ktk hili huuuuu! Ni sawa na siku ya kufa mwanadamu awaye yote amefichwa ila Mola pekee, jamani ktk hili msiumize vichwa gailini ila tumche Mwenyezi Mungu.
 
Eish kila siku mnaxidisha miaka site tutakufa 😕
 
wasabatho ndiyo wanaimani za namna hiyo mara nyingi, ata ukifuatilia 1843 waliwahi kutoa nyingi za mambo kama haya! ukwli ni kwamba ata sayansi za dunia zitaishia kuweka theory maana mwanasayansi mwenyewe Allah amue kwamba dunia inakwisha hizi nyingine propaganda za new world order!
 
Siku ile hakuna anayeijua hata Mwana hajui lini itakuja ila Mungu peke yake ndiye ajuaye. La muhimu ni kuwa tayari muda wote kwani siku hiyo itatokea kama radi au mwizi. Hivyo yatupasa kukesha kama wale wanawali watano wenye busara.
 
Mathayo 24:36 - Kuhusu siku ile na saa ile hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni wala Mwana, ila Baba tu.
 
mtoa mada wewe utakuwa umeiona sinema hiyo
 
Hivi unajua maana ya mchana?? Eti dunia itakumbwa na giza nene wakati wote wa usiku na mchana!! Ndio umeandika nini hapo?
 
Nilipofika kwenye mwezi ni sayari nikajitahidi kuvumilia, ila nilipofika kwa Mungu kuuwawa na wolf, duh! Sijaona ujinga ulioandikwa kwa mpangilio mzuri kama huu.
Sijui nilikuwa naenda wapi nikatokea huku nimeshasahau, aha! kwa jirani kula kozi.
 
Nilipofika kwenye mwezi ni sayari nikajitahidi kuvumilia, ila nilipofika kwa Mungu kuuwawa na wolf, duh! Sijaona ujinga ulioandikwa kwa mpangilio mzuri kama huu.
Sijui nilikuwa naenda wapi nikatokea huku nimeshasahau, aha! kwa jirani kula kozi.
Mkuu Mungu anayetajwa pale si yule unayemwamini wewe,ni Mungu wa Imani hiyo iliyokuwa ikifanya huo utabiri wa February 2014 ambao hata hivyo haujatokea.
 
innalillah wainna ilayh raju un, nadhani tunakiwa tunapoambiwa mambo tuchanganye na akili zetu, Mungu amuumbe shetan kisha shetan ampige Mungu hadi kumuua? Audhubillah mina dhwalala.ee Mola niepushe mimi kutokana na ujinga
 
Nilipofika kwenye mwezi ni sayari nikajitahidi kuvumilia, ila nilipofika kwa Mungu kuuwawa na wolf, duh! Sijaona ujinga ulioandikwa kwa mpangilio mzuri kama huu.
Sijui nilikuwa naenda wapi nikatokea huku nimeshasahau, aha! kwa jirani kula kozi.

shekh mswalie mtume mwezi mtukufu huu mambo ya kula kula yanatoka wap?
 
tje kuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba kuna sayari zilizowahi kugongana? if yes hilo litawezekana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom