singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,531
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amesema kuwa shughuli ya kupata mgombea urais kwa tiketi ya CCM haikuwa rahisi na akashukuru kwamba imemalizika kwa amani.
Mchakato huo ulihitimishwa Julai 12 mjini Dodoma wakati Mkutano Mkuu wa CCM ulipopitisha jina la Dk John Magufuli kugombea nafasi ya kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake mwishoni mwa mwaka.
Jumla ya makada 38 walijitokeza kuwania nafasi hiyo, na majina matano ndiyo yaliyopitishwa kwenda Halmashauri Kuu na baadaye matatu kwenda Mkutano Mkuu.
Mchakato wa urais ndani ya CCM ambao kwa kawaida hutawaliwa na msuguano kabla ya kumalizika kwa maridhiano, safari hii ulienda mbali zaidi baada ya wajumbe watatu wa Kamati Kuu kupinga nje ya kikao uamuzi wa chombo hicho na baadaye wajumbe wa Halmashauri Kuu kumwimbia mwenyekiti wao, Jakaya Kikwete wimbo wa kuonyesha wana imani na Edward Lowassa baada ya jina la mbunge huyo wa Monduli kuenguliwa na Kamati Kuu.
Jana, akitoa hotuba fupi baada ya kumalizika kwa sala ya Eid el Fitr kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mwinyi alizungumza kwa mara ya kwanza hadharani kuhusu mchakato huo, akidokeza hali ilivyokuwa.
Haikuwa kazi rahisi kwenye mchakato huu wa kumtafuta mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM, alisema Mwinyi lakini akawahi kuipoza kauli hiyo kwa kuelezea amani ilivyotawala mwishoni.
Kama ni jahazi basi sasa tunashukuru limefika pwani salama.
Uchaguzi huu ni kwa ajili ya kuwapata viongozi wetu, tunataka viongozi bora wa kutuletea maendeleo, mapatano na wenye mahaba na wananchi.
Akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya mchakato huo wa kumtafuta mgombea wa urais kukamilika mjini Dodoma, Mzee Mwinyi alimshukuru Mungu kwa mchakato huo kuisha salama.
Haikuwa kazi rahisi kwenye mchakato huu wa kumtafuta mgombea mmoja atakaye peperusha bendera ya CCM, kama ni jahazi basi sasa tunashukuru limefika pwani salama. Sasa, ninawaomba Watanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi wa nchi tunaoufanyika kila baada ya miaka mitano, alisema Rais Mwinyi ambaye alikuwa mmoja ya wajumbe wa Baraza la Ushauri waliofanya kazi ya kutuliza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM hadi kuafikiana kuendelea na mchakato wa kumpata mgombea urais.
Aliwasisitizia Watanzania kuacha tabia ya kupenda mno na kuacha kubaguana, akisema hakuna aliye bora na kuwataka kuzidisha mapenzi miongoni mwao na kusherehekea vyema Sikukuu ya Eid el Fitr. Hakuna jambo lenye maana kama hili la kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye kutufikisha salama siku kama hii ya leo (jana) ambayo tunasherekea Sikukuu ya Eid, alisema Mwinyi.
chanzo Mwananchi