Mwinyi ashangaa ufisadi kumekithiri awamu ya nne

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
  • ASEMA WAKATI WAKE RUSHWA HAIKUWEPO
Hadija Jumanne

mwinyiruksa.jpg


Ali Hassan Mwinyi

RAIS mstaafu wa awamu ya pili, mzee Ali Hassani Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa ameshangaa kukithiri kwa rushwa katika utawala wa awamu ya nne ikilinganishwa na tawala zote zilizopita.

Mzee Ruksa alisema hayo jana jijini Dar e Salaam katika mahafali ya 12 ya Chuo cha Teknologia ya Habari (IIT) alikoalikwa kama mgeni rasmi.

Alisema kuwa miongo miwili iliyopita, akiwa madarakani kama rais wa awamu ya pili rushwa ilikuwa haipo na ilikuwa haina nafasi.

Mwinyi alibainisha kwamba, wakati anatangaza ruksa kwa kila kitu hapakuwa na rushwa wala mianya yake.


“Kipindi mimi niko madarakani miongo miwili iliyopita, rushwa ilikuwa haipo na hata wakati natangaza kila kitu ruksa katika serikali yangu, kulikuwa hakuna mifuko ya rushwa serikalini wala katika sekta binafsi,” alisema Mwinyi.

Alisema anashangaa kuona rushwa inakithiri katika serikali ya awamu ya nne (ya rais Jakaya Kikwete) huku mianya yake ikizidi kuongezeka kwenye taasisi za umma na sekta binafsi.


“Inashangaza kuona rushwa imeota mizizi katika sekta mbali mbali hapa nchini kitu ambacho kinakwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi,”alieleza Mwinyi.


Rais huyo mstaafu aliwataka vijana waliohitimu katika chuo hicho wakatumie ujuzi walioupata kujiajiri na siyo kusubiri kuajiriwa au kupata nafasi serikalini.


Aliwataka pia kuwa wapambanaji wa rushwa ambayo imeota mizizi katika sekta mbalimbali nchini.


Alipoingia madarakani miaka mitano, iliyopita Rais Kikwete aliahidi kuwa serikali yake itaongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa na kwamba, atafanya hivyo kisayansi kwa kushambulia kiini chake.


“Kwa kadri mapato ya Serikali yanavyoongezeka, ndivyo tutakavyoongeza mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ili kupunguza vishawishi vya rushwa. Tutaendelea pia kuongeza uwazi katika maamuzi ya Serikali. Tutaimarisha uwezo wa kifedha na kiutendaji wa taasisi zilizo mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya rushwa, hasa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Jeshi la Polisi na mahakama. Lakini yote hayo ni bure iwapo wananchi hawatajitokeza kusaidia vyombo hivyo," alisema Kikwete.


Kikwete alisema hayo Desemba 30, 2005 wakati akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nne wa Tanzania na kuomba ushirikiano kutoka kwa wananchi kwenye mapambano hayo.


"Naomba ushirikiano huo kutoka kwa wananchi,” alisema Kikwete na kuongeza kuwa mbali ya hayo, alibainisha kuwa katika kupambana na rushwa ataangalia kwa ukaribu suala la mikataba.


Alieleza kuwa serikali yake inakusudia kuangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa, hasa zile kubwa. Hata hivyo, katika juhudi za serikali ya awamu ya nne kupambana na rushwa, kesi mbalimbali za rushwa kubwa zinazofikia 25 zipo mahakamani.

Aidha, mwaka huu serikali imerekebisha sheria na kuipa meno Takukuru ili kuipa nguvu zaidi ya kupambana na tatizo hilo, na kidhinisha sheria mpya ya gharama za uchaguzi inayolenga kudhibiti na matumizi ya fedha haramu katika uchaguzi.


Katika mahafali hayo, Mwinyi alitoa shahada ya kwanza, stashahada na stashahada na digrii kwa wahitimu 150 katika masomo ya teknolojia ya habari, biashara na kompyuta.


Wahitimu 15 kati ya 150 ambao walichukua shahada ya teknologia ya habari walitunukiwa tunzo maalum baada ya kufanya vizuri katika masomo hayo.


Wahitimu wengine 50 pia walitunukiwa tuzo katika masomo stashahada na wengine 85 stashahada ya kompyuta na biashara.


Chuo hicho kilianzishwa Mei 1990 chini ya jina Microtek Computers Limited kabla ya kubadilishwa mwaka 1992 na kuwa Taasisi ya Teknologia ya Habari(IIT).


Mkurugenzi mkuu wa Taasisi hiyo Mujtaba Salemwalla, alisema kuwa elimu hiyo waliyopewa vijana hao hawana budi kuitumia ipaswavyo kwani wamebeba jukumu la kuihudumia jamii.

Chuo hicho kwa sasa kina matawi mawili katika jiji la Dar es Salaam, katika jengo la Kelvin lililopo mtaa wa Samora na katika jengo la Africab Tower barabara ya Kawawa karibu na Machinga Complex na kinatoa shahada na stashahada.


Mwinyi ashangaa ufisadi kumekithiri awamu ya nne
 
Huyu ni wa ajabu sana amesahau ufisadi alioufanya yeye na marehemu balozi diria na Bakhresa wakamatajiri wa kutupwa leo anashangaa wengine kula!!!! Ama kweli madaraka matamu bora asiseme maana atashushuka
 
Huyu ni wa ajabu sana amesahau ufisadi alioufanya yeye na marehemu balozi diria na Bakhresa wakamatajiri wa kutupwa leo anashangaa wengine kula!!!! Ama kweli madaraka matamu bora asiseme maana atashushuka

Mdondoaji, umesahau ile kauli ya wahenga kuwa nyan haaoni kundule!!! teh! teh! hata Mkapa naye ameanza kusema siku hizi!!
 
Huyu ni wa ajabu sana amesahau ufisadi alioufanya yeye na marehemu balozi diria na Bakhresa wakamatajiri wa kutupwa leo anashangaa wengine kula!!!! Ama kweli madaraka matamu bora asiseme maana atashushuka

Ufisadi alioufanya Mzee Mwinyi na utajiri wake ni upi? Tungependa kuujua ili tuweze kumhukumu kwa haki.
 
Ufisadi alioufanya Mzee Mwinyi na utajiri wake ni upi? Tungependa kuujua ili tuweze kumhukumu kwa haki.

Baba ntilie labda tuchokoze nyuki kama unakumbuka scandal ya pembe za ndovu na dhahabu iliwakumba akina Diria, aliyekuwa behind the scene uliza alikuwa ni nani? na Kwanini liletwa azimio la zanzibar kuua lile azimio la arusha? ukishayajua majibu ya hayo maswali utajua kwanini tunamuomba huyu mzee akae kimya maana ataumbuka kwakweli. Na hapo sijagusa ardhi waliojigaia yeye na washkaji zake ambazo ardhi sasa hivi hazigusiki kwa bei na hilo basi ndio limechangia mwanae sasa hivi kuwa ndio mdau mkubwa wa biashara za appartments mjini but ardhi hizo zilipatikana vp no one knows!!!!
 
Siti Mwinyi alikua anauza unga akiwa Ikulu..mara mia ANBEM Ltd. Mi nakwambia watanzania wanalalamika bure.. sibora kiwira..lol
 
Ufisadi alioufanya Mzee Mwinyi na utajiri wake ni upi? Tungependa kuujua ili tuweze kumhukumu kwa haki.

Pitia mada hii hapa, halafu go figure...

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ba-za-kupanga-wa-dr-hussein-mwinyi-dar-6.html

La nyongeza nasema: Hussein Mwinyi kupewa nyadhifa mbalimbali za juu Serikalini hadi kuukwaa Uwaziri Wa Ulinzi pia ni Ufisadi wa aina fulani kwa upande wa A.H Mwinyi, kwani ni wazi Hussein Mwinyi kabebwa tu moja kwa moja kutumia mkono wa babake na ameonyesha wazi kazi haiwezi.
 
:confused2::confused2::confused2::angel:
Tume ya Warioba ilikuwa wakati gani? Naomba mnisaidie!
Sababu ya kuwepo kwa tume ilikuwa ni nini?Tamko la "Ruksa"
 
Mimi nilidhani baada ya kile kibao atakoma kusema vitu vya kutumwa!

Tatizo najua ni hizi pesa baada ya kustaafu.Hii yenyewe ni rushwa ya kununua sauti za maraisi waliostaafu. Mbona anapokea.

Angeachwa aishi kwa jasho lake angekuwa mtu huru kabisa na asingekubali kutumwa kuzungumzia mambo ya watu amabayo mengine hata mwenyewe huwa hayaamini.

Alipotaka kuhalalisha kondomu najua msomi kama yeye alijua sio sahihi,lakini asikose tu kusema katika hadhara ya waliotaka kupata sauti yake halafu wapite kujidai.
 
· 18th March 2010 04:03 PM #1
https://www.jamiiforums.com/members/jojipoji.html
Mradi wa nyumba za kupanga wa Dr. Hussein Mwinyi Dar

Project
Sea View Apartments


Status

July – December 2007 All detailed designs and bills of quantities completed. Building permit obtained in January 2008 Construction due to start


Client

Dr. Hussein Ali Mwinyi P. O. Box 9380
Dar es Salaam


Description

A 12 storey apartments building with 27 luxurious apartments; 1st to10th floor accommodating 5 duplex apartments occupying the middle, 20 deluxe apartments, two on either side of the floors; the 11th floor accommodating 2 identical penthouses.


Estimated cost
Tshs. 10 billion


Philip Mangula: Itafika mahali kura zitakuwa kama mnada, mwenye pesa nyingi ndio mshindi
 
Kweli nyani haoni kundule! Ila kundule zinazidiana!. Mimi namshauri babu Ruksa Anyamaze ili heshima ibaki pale pale!
 
Kweli nyani haoni kundule! Ila kundule zinazidiana!. Mimi namshauri babu Ruksa Anyamaze ili heshima ibaki pale pale!

Mie pia nadhani atafanya la busara akae kimya awaachie akina Butiku, Warioba na Salim waendelee kusema maana wale angalau wanatizamika but sio yeye.
 
Watanzania tuna machungu na huyu babu. Anyamaze! Huyu babu tunamkumbuka kwa:
1. Udhaifu wa uongozi,
2. Mfadi wa kwanza mkubwa wa kifisadi wa IPTL,
3. Kashfa ya kuuza Loliondo,
4. Kuuzwa kiholela kwa maeneo ya beach za Dar,
5. Alishindwa kabisa kuweka 'Fiscal discipline'. Inflation ilikuwa kubwa sana. Serikali yake ilikuwa haikusanyi kodi, 'ruksa za kukwepa kodi zikawa nyingi. Kama ingekuwa hakuna kikomo cha utawala sasa tungekuwa kama Zaire ya Mobutu au Zimbabwe (tungekuwa na noti za milioni 1 na milioni 10).
6. Mikutano na 'wenye shida' pale ofisi ya CCM Lumumba. Alikuwa akitolea maamuzi hata mashauri/kesi zilizokuwa Mahakamani. Baadaye ndipo akashauriwa ndiyo akaacha.
7. Inasemekana eti mwanaye babu (Hussein Mwinyi) alikwepa kwenda JKT kwa mujibu wa sheria (wakati huo baba yake ndiye alikuwa Rais). Eti sasa ndiye Waziri wa Ulinzi!
Misamiati kama: Usawa wa gudulia, Pololo, 'Disco', Kujongo, Kunyakua, Uchaka, etc. anavisikia kwa kuhadithiwa tu!
8. VIBALI VYA IKULU... Vilikuwa na 'nguvu' hata kama maagizo yake ni kinyume cha sheria.
9. Lady wa kwanza wa wakati huo alikuwa na nguvu (ambazo si za kisheria) kuliko. Ila huyu wa sasa naye anafuata nyayo...
10. Baya zaidi, ndiye alimtoa Meja (wakati huo) Jakaya Kikwete kutoka huko kusini na kumpa ubunge wa kuteuliwa na kisha kumuingiza Baraza la Mawaziri. Safari ikaanzia hapo...

Mengine ongeza...
 
Kwa mawazo yangu ufisadi wake mbaya zaidi kwa Taifa letu ulionekana wazi pale aliporuhusu au alipoanzisha kwa siri maoni ya kutaka kuongezewa muda wa Uraisi ambao ulishtukiwa na Mwl. Nyerere, refer Uongozi wetu na hatma ya Tanzania. That was shameful!!:angry::painkiller:
 
Ndio maana huwa nasema kila mara Tanzania hatuna Viongozi, tuna Majuha tu.....!!
Hivi Mwinyi kushangaa ufisadi wa leo si Ujuha huu jamani. Naona sasa mizaha ni kila sehemu. Aliyepo madarakani ni Mizahaa tuuu, Aliye toka ni mizahaa tu hivi wanafikiri sisi watanzania ni viwete wa akili.....

Huu ni upuuzi wa wazi wazi that can make someone mad.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom