Mwingine auawa huko Mabwepande...

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2009
Posts
3,444
Reaction score
265
ASKARI wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), wanatuhumiwa kumpiga na kumsababishia kifo, Musa Amiri Lihonga, Mkazi wa Mbezi-Makabe, jijini Dar es Salaam, katika msitu wa Mambwepande.Tukio hilo linadaiwa kutokea Januari 5, mwaka huu, baada ya askari hao wa TANAPA kumkuta Musa Amiri Lihonga akiokota kuni katika msitu huo.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu aliyejitambulisha kuwa ni Abdul Lihonga, siku ya tukio, ndugu yao alikwenda kutafuta kuni lakini alikamatwa na askari wa Tanapa, wakamtuhumu kuwa anachoma mkaa. Alisema baada ya kumkamata, walikwenda nyumbani kwa marehemu kupekua lakini hawakukuta mkaa zaidi ya kiasi kidogo tu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kumpeleka kituo cha polisi Mbezi.

Ndugu huyo alisema mara tu baada ya kufikishwa polisi, ndugu yao alianza kuugulia maumivu makali, ikidaiwa ni matokeo ya kipigo alichokipata kutoka kwa askari wa Tanapa, walipomkamata msituni Mabwepande.

Hali ya marehemu ilizidi kuwa mbaya, jambo lililowafanya polisi kumpeleka katika Hospitali ya Mwananyala na kulazwa wodi namba 5, lakini siku moja baadaye alifariki. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alipohojiwa juu ya jambo hili aliomba muda aweze kufuatilia na kulitolea ufafanuzi.

Hata hivyo, uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi, umebaini kuwa askari watatu wa Tanapa wanashikiliwa kuhusu tukio la kifo hicho.
 
Hayo ya askari wa tanapa kuua raia tumeshayazoea huku kwe2 kagera.Wanaingza mifugo yao kwenye maeneo ya hfadh na kuwatoza faini wakikataa huwaua wao na mifugo yao kwa kuwapga rsasi wakisingzia wameingza mifugo kwenye hfadh.
 
Dunia imekwisha yani kuni ina thamani kuliko uhai wa binadamu hao askari ni wa kunyongea hadi kufa........
 
Mabwepande haipo chini ya TANAPA wewe na gazeti lako mnapotosha umma.
 
Mkuu Kichwa cha habari kinapingana na maelezo,maana inaonekana walioua ni askari wa wanyama pori na siyo hawa wanaojiita wanalinda raia.

Hili tukio limenikumbusha jamaa mmoja alikuwa anaitwa Meng'anyi, alikuwa askari wanyama pori SENAPA. Huyu jamaa aliua sana watu waliokuwa wanaingia mbugani. Lakini na yeye alishatangulia huko mbele ya haki, nafikiri walikutana huko.

Hawa jamaa wana roho mbaya sana.

Nawapa pole wafiwa.
 
Heading inapotosha.

Umeanza kutoa hukumu kabla hata ya kesi kupelekwa mahakani. Hata kama huwapendi CCM, upotoshaji hautasaidia harakati zako.

Please, be firm but fair to everyone..
 
hakuna litakalofanyika, dawa ni kuitoa CCM madarakani, hapo ndipo tutaaza kuona uhuru wa kweli na haki kwa wote.
 
JF kuna vituko Mabwepande na TANAPA wapi na wapi.
 
JF kuna vituko Mabwepande na TANAPA wapi na wapi.

yaani katika wajinga nchi hii wewe ni first class .... wewe siyo mtanzania aisee ... either hujui msitu wa mabwepande ni hifadhi ya taifa au hujui maana ya TANAPA na kazi zake

nenda shule ya ngumbaru ... uondoe ujinga
 
Kweli Tanzania tumefikia mwisho wa kuuana. Yaani mtu anayeokota kuni anapigwa hadi kufa? Je hao wanauza meno ya tembo na pembe huku wakiwa wamevaa suti na tai watauawa pia?

Jamani askari msidhani mna haki ya kumwuua kila mnayemkuta msituni. Vitendo hizi vinalishushia laana jeshi la polisi na matawi yake. Hatujasahau mlichomtendea yule mama maskini aliyekuwa anakata majani kule KINAPA. Hizi laana zitawamaliza na familia zenu. Angalieni sana matendo yenu. Mungu atawarudishia hapa hapa duniani.
 
Ukiuwa kwa upanga, nawe utauawa kwa upanga! Ee Mungu ibariki Tanzania na watu wake, R.I.P Mpendwa,
 
Heading inapotosha.

Umeanza kutoa hukumu kabla hata ya kesi kupelekwa mahakani. Hata kama huwapendi CCM, upotoshaji hautasaidia harakati zako.

Please, be firm but fair to everyone..

Watanzania, au wewe msomaji kwenye JF, Soma taratibu, hoja ya neno CCM imeingiaje hapa? haijatajwa katika habari nzima, haijatajwa katika heading kama wewe unavyotaja, unajua kusoma na kuandika au unasimuliwa ndo unakuja kuchangia?. Aliyekuambia hapa kuna kupenda au kuchukia CCM hapa nani? Suala linazungumzwa Mwananchi kauawa, ameuawa na Askari wa TANAPA kwa kipigo, iwe eneo hilo lipo chini ya Tanapa au hapana, tunajadili Uhai wa mtu aliyeuawa......, hayo masuala ya CCM, au kama msitu wa Pande unalindwa na watu wa TANAPA sio hoja yetu zinajua mamlaka husika.
 

Mkuu,
Hiyo heading ilikuwa imeandikwa "Polisi wa CCM waua mwananchi mwingine Mabwepande" naona mods wameibadilisha baada ya kulalamikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…