Mwingiliano wa falsafa za Dr. Magufuli, Kikwete na Lowassa, ni ukweli usiopingika

Albert Einstein

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
384
560
KILIMO KWANZA ELIMU KABLA NA MWELEKEO WA TANZANIA YA VIWANDA IFIKAPO 2025.

Ni Ukweli Usiopingika kwamba ili chama fulani kishike dola lazima kwanza watu wakikubali kuanzia sera zake, Itikadi, falsafa, Mitazamo, Mipango kazi na utayali wa kuleta maendeleo pasipo shaka kwa wananchi. Kauli hiyo hapo juu ni miungoni mwa kauli za kishujaa kwa kiongozi aliyekuwa chama tawala na akaamua kuachana na chama hicho kwa sasa zisizokuwa rasimi sana. Itakumbukwa kwamba sera ya Kilimo kwanza ilishika moto sana kipindi cha Mhe Mizingo pinda. sera hii ya kilimo kwanza ilikuja kwa kuwahi mno ndio maana matamko kadhaa ya viongozi mahususi yalileta sintofahamu miongoni mwa watanzania.

Kwanza, ninasema Kauli mbiu ya Kilimo kwanza ilikuja kwa kuwahi sana nikifananisha na elimu ambayo watanzania walikuwa nayo kwa kipindi hicho, aidha ni ukweli usiopingika mioyoni mwa watanzania kwamba Kilimo cha Jembe hakina manufaaa yoyote zaidi ya kupata chakula kwaajili ya kujikimu kimahitaji. Ukizingatia kwamba hata pembejeo hazifiki kwa wakati kwa watu wanaotegemewa hivyo tatizo linakuwa kubwa zaidi.

Pili, Kauli mbiu ya Kilimo kwanza ilikuja kwa matukio ndani ya nchi. Kuna tatizo kubwa sana nchi yetu inarasimisha kwamba ili watu wasahau jambo flan potential huleta maada ambaye itawafanya watu wapoteze concentration kwenye jambo husika kitu ambacho ninakipinga kwa asilimia mia moja. lazima tufanye mambo kwa mipango endelevu ambayo huwekwa kwenye maandishi miezi sita kabla ya kufanyika kwa tukio husika.

Tatu, Kauli mbiu ya Kilimo kwanza ilikuja kipindi cha Matokea makubwa sasa yaani (BIG RESULTS NOW). na hii ilikuwa kwenye Elimu ambayo waanzilishi walifanya pasipo tafiti chanya katika mpango kazi wake. huwezi ukaleta matokea makubwa sasa kwenye Kilimo wakati watu wanaofanya kilimo hawajapata elimu ya kutosha. ndio maana Matokeo Makubwa sasa imefeli kwa zaidi ya asilimia 80 sababu ni Kufanya mambo pasipo kushirikisha wataalam kwenye fani husika wanatumia nguvu ya uanasiasa kuharibu nchi ambayo ipo huru miaka zaidi ya 53 lakini Uchumi wake bado unateteleka. Haiwezekani nchi ya Tanzania ikawa miongoni mwa nchi Masikini Afrika wakati tunavitega uchumi vya kutosha. Maana nchi kama indonesia ina kitega uchumi kimoja tu lakini wanatupiku kimaendeleo.

Suala la Elimu ni miongoni mwa mambo nyeti sana kwa taifa letu tunakiwa tuwe na kizazi kichoelimika na hata matamanio ya Tanzania ya viwanda haiwezi kufikiwa mpaka Elimu iwe imemfikia kila Mtanzania, Elimu sio suala Mtambuka kama baadhi ya wanazuoni wanavyodai kwenye machapisho yao, Tunahitaji kuhakikisha kwamba tunabadilisha mtaala kama ikiwezekana ili tupate vijana makini wa mambo ya Ufundi ili mambo yaweze kwenda sawa, Lazima tuaddress Elimu kwa vitendo( Technical Education-VETA, & HANDS-ON Education) ili watu wetu ndani ya viwanda waelewe baadhi uendeshaji wake unavyofanyika.

Hivyo basi ili Tanzania iendelee tunahitaji Elimu kama kipaumbele cha kwanza, Elimu kama kipaumbele cha pili na Elimu kama kipaumbele cha tatu. nataka watanzania na Mhe Rais atambue kwamba elimu ni hitaji muhimu sana kwa taifa changa kama Tanzania. Tunapaswa kupeleka watu wakasome kwa wenzetu walioendelea ili walete tekinolojia nchi, Napenda kumshauri Mhe Rais aanzishe Ufadhili kwa wanafunzi makini maana Taasisi ya Urais ni Kubwa sana anaweza akafadhili wanafunzi wakaja hapa wameiva vya kutosha.
Bila kubadilisha mifumo ya utawala kuanzia ngazi ya kitongoji Tanzania hatutaweza kupiga hatu (We neeed to strengthen Our Systems).

Lazima Urasimu wa utendaji ndani ya serikali uweze kuondolewa ili shughuli za kiserikali ziweze kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria zilizopo, aidha serikali ihakikishe kwamba mfumo wa Rushwa unaondolewa kwa kuwapa TAKUKURU MENO kisheria na Kikatiba kuweza kuchunguza na kushitaki mtu anayesadikika ametoa au amepokea Rushwa.

Hitimisho, namshauri Mhe RAIS aongeze wigo wa ukusanyaji kodi ili pato kila mwezi lipande mpaka Trillion 1.5 ili kwa mwaka tuweze kukusanya Trillion 18. hii itaongeza wigo wa kubuni miradi kwa ajili ya maendeleo lakini pia deni la taifa litapunguzwa kwa asilimia kadhaa. Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mungu dumisha amani duniani kote..........................................
Nawasilisha
 
Kudos Avatar , User name vinaakisi uliyoyaandika mkuu.

Je! serikali/viongozi wetu wapo tayari kwa hayo?
 
good. ni mada nzuri , nilitaka kuandika mada kama hii sema umeniwahi. title yangu ilikuwa ni MAWAZO YA KİKWETE, MAGUFULİ na LOWASSA kwenye KİLİMO, VİWANDA na ELİMU ndio msingi wa Tanzania ya uchumi wa kati.
 
Back
Top Bottom