Mwili wa mwanasiasa wa Kenya 'wapatikana mtoni'

kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,092
2,128
Polisi nchini Kenya wanasema mwanasiasa aliyehusishwa na uvamizi wa mashamba ya kibinafsi amepatikana ameuawa.

Wanaamini mwili uliotolewa mtoni hii leo ni wa Thomas Minito, ambaye alikuwa akichunguzwa kwa kujihusisha na kupigwa risasi kwa mhifadhi Mwitaliano Kuki Gallman.

Mwili huo ulipatikana ukielea kwenye mto mmoja eneo ya Machakos, kilomita hamsini mashariki mwa Nairobi.

Polisi wanasema walimtambua kupitia stakabadhi zilizokuwa mfukoni mwake. Familia yake hata hivyo haijadhibitisha haya.

Polisi wanasema wanashuku aliuawa kwa kuwa alikuwa na majeraha kichwani.

Minito alikamatwa tarehe 30 mwezi Machi na kushtakiwa kwa kosa la kuchochea ghasia katika kaunti ya Laikipia, yaliyofanya mhifadhi mashuhuru wa mazingira na mwandishi, Kuki Gallmann kupigwa risasi.

Polisi wangali wanafanya operesheni katika Kaunti ya Laikipia iliyoko Kenya ya Kati. Hii ni baada ya wafugaji kuvamia mashamba ya kibinafsi wakitafuta lishe. Mmiliki mmoja wa mashamba hayo makubwa aliuawa mapema mwezi Machi, Wafugaji wanadai polisi wamewauwa mamia ya wanyama ili kuwafurusha.

Mwili wa mwanasiasa wa Kenya 'wapatikana mtoni' - BBC Swahili
 
Haha lol ...go around inciting people to invade private properties and this is what u get!!..the same people will turn on u
 
_96121249_politician.jpg

Polisi nchini Kenya wanasema mwanasiasa aliyehusishwa na uvamizi wa mashamba ya kibinafsi amepatikana ameuawa.

Wanaamini mwili uliotolewa mtoni hii leo ni wa Thomas Minito, ambaye alikuwa akichunguzwa kwa kujihusisha na kupigwa risasi kwa mhifadhi Mwitaliano Kuki Gallman.

Mwili huo ulipatikana ukielea kwenye mto mmoja eneo ya Machakos, kilomita hamsini mashariki mwa Nairobi.

Polisi wanasema walimtambua kupitia stakabadhi zilizokuwa mfukoni mwake. Familia yake hata hivyo haijadhibitisha haya. Polisi wanasema wanashuku aliuawa kwa kuwa alikuwa na majeraha kichwani.

Minito alikamatwa tarehe 30 mwezi Machi na kushtakiwa kwa kosa la kuchochea ghasia katika kaunti ya Laikipia, yaliyofanya mhifadhi mashuhuru wa mazingira na mwandishi, Kuki Gallmann kupigwa risasi.

Polisi wangali wanafanya operesheni katika Kaunti ya Laikipia iliyoko Kenya ya Kati. Hii ni baada ya wafugaji kuvamia mashamba ya kibinafsi wakitafuta lishe. Mmiliki mmoja wa mashamba hayo makubwa aliuawa mapema mwezi Machi, Wafugaji wanadai polisi wamewauwa mamia ya wanyama ili kuwafurusha.

Chanzo: BBC
 
Kwa hiyo wazungu wamemfanyia ufedhuli pia, Kenya is a mafian state.
Not wazungu necessarily, unajua hiyo genge pia iliwaua polisi, na polisi wa Kenya si unawajua? Halafu pia the politically connected ranch owners ambao si wazungu mali yao pia iliharibiwa.

This guy alichokoza watu wengi sana. Hako connected na powerful pipo in politics na analeta umbelembele ati kuchochea fujo.
 
Tujiandae kupokea wakimbizi kutoka kenya
Mngewapokea 2013 juu ndio ilikuwa kubaya, lakini 2017 sioni kama kutakuwa na fujo. Huyu jamaa hajauliwa juu ya political rivalry as such, na sio politician wa kutajika- mini mwenyewe nilimjua ile siku alikamatwa juu ya zile vurugu huko Laikipia.

Yale mambo alifanya haikuwa mazuri, na kama ni serikali imefanya hivi wamekosea sana.

Anyway, RIP, you inciter of violence.
 
Wacha kuelekeza kidole bila kujiangalia pia, vipi ile miili saba ilipatikana kwenye mto Rufiji ikielea ndani ya viroba mliizika kirasmi au ndio yale yale ya Afrika Serikali yacharuka suala la maiti saba Mto Ruvu | Magazeti ya leo| Tanzania News |Tanzania Today

wewe fala wale ni Wahabeshi aka Waethiopia or waamihaji haram. Lete hapa news yeyete ikieleza watu wanatafuta ndugu zao hawaonekani.

Hizi za waethiopia kukutwa wamekufa or kutekelezwa mahala ni mambo ya kila siku. Huyo ni mwanasiasa wenu mmemuua na wale watoto 3 mewaua.

Kenya inajulikana kwa mauaji, mwaka jana extrajudicial killings Africa nzima zilikua 160+ Kenya pekee ni 140+.

Usisahau Tom Mboya aliuwawa, Gama Pinto, Kariuki, Robert Ouko. Nakumbuka nikiwa mdogo tulioneshwa mwili wa Robert Ouko ukiwa shambani, umetobolewa macho, umechomwa, Jamaa alikua na Mwanya, wakamtoa na meno duh! Nyang'a soo!
 
Back
Top Bottom