Je, GenZ wa Tanzania wanaweza kusimama kidete kama wenzao wa Kenya?

Ikaria

Member
Jul 17, 2019
93
238
Bila shaka ni ukweli usiopingika kuwa maandamano dhidi ya serikali ni ya kwanza ya aina yake nchini Kenya.

Kwa nini?
Maandamano ya kupinga mswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2024 hayakuongozwa na Mwanasiasa yoyote Wala Chama chochote cha kisiasa; bali yaliratibiwa na vijana hasa wa kizazi Z kwa kutumia mitandao ya kijamii hususan wa X na TikTok.

Ni maandamano ambayo yalipelekea hata vyombo vya habari kubadili mbinu kwa kuwaalika studioni wageni kizazi cha GenZ, tofauti na ilivyozoeleka kualika wanasiasa na viongozi wakuu kutoka sekta mbalimbali.

Aidha kizazi hiki cha GenZ kilifanikiwa kuhamasisha watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia hashtag #RejectFinanceBill2024, na kuifanya trend hio kuwa nambari Moja duniani kwa zaidi ya posti milioni 2.

GenZ vilevile wanafanya michango mitandaoni kwa njia ya M-changa kulipa gharama za matibabu za wenzao waliojeruhiwa kwenye maandamano na kulipa gharama za mazishi ya wale waliopigwa risasi, mfano Rex Kanyeki Maasai, aliyeuwawa na polisi kwa risasi karibu na stendi ya Kencom Jijini, Nairobi.

Kizazi cha GenZ kimesisitiza kuwa hakina kiongozi na kuwa Kila mmoja ni kiongozi wa mwenzake.

20240621_125537.jpg

20240621_103010.jpg



Matukio ya Jana yameibua maswali mengi hasa hapa Afrika Mashariki:

• Wakenya wana uzalendo mkubwa kuliko wananchi wa taifa lolote lingine hapa Afrika Mashariki?

• GenZ wana athari Gani Kwa mustakabali wa siasa za nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

• Viongozi wa vyama vya kisiasa wajifunze nini kutoka kwa GenZ.

• Iweje ni Kenya tu ambapo kizazi hiki kinaweza kusimama kidete? Wako wapi Genz wa Tanzania, Uganda na Rwanda?

PIA SOMA
- Je, GenZ wa Tanzania wanaweza kusimama kidete kama wenzao wa Kenya?
 
Wafuasi wa Odinga hao, na muswada umepitishwa, Kwa hiyo labda unawahamisha wafuasi wa Chadema lakini usisingizie Gen Z, hiyo ni generalization
 
Not true. Nipo Nairobi muda huu na I can tell you kuwa hapa hakuana ufuasi wa mwanasiasa yeyote. Fahamu kuwa ngome kuu ya kisiasa ya Rais William Ruto iitwayo #Eldoret ilishuhudia maandamano makubwa pia. Wakenya ni wazalendo kuliko Wabongo. Hilo naomba kuwathibitishia.
Wafuasi wa Odinga hao, na muswada umepitishwa, Kwa hiyo labda unawahamisha wafuasi wa Chadema lakini usisingizie Gen Z, hiyo ni generalization
 
Wafuasi wa Odinga hao, na muswada umepitishwa, Kwa hiyo labda unawahamisha wafuasi wa Chadema lakini usisingizie Gen Z, hiyo ni generalization
Shida yako unawaza vyama Wala sio nchi. Wewe hujui kinachoendelea Kenya. Wala sio wafuasi wa Odinga. Ni vijana wa wadogo wameamua kusimama kidete. Tena mhamasishaji wao anaitwa Kiprop mfuasi wa Rutto. Uwe unafanya utafiti kabla ya kupinga Jambo.
 
Back
Top Bottom