Mwili wa Marehemu Dkt Reginald Mengi kuzikwa Alhamisi kijijini kwake Machame

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,696
22,729
Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame, ibada ya mazishi ni siku ya Alhamis wilayani humo kanisa la Kisereni (KKKT)- Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo.


=====

Mwili wa marehemu wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi utawasili jumatatu mchana Mei 6, 2019 jijini Dar es salaam kutoka Dubai na kupelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo .

Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo amesema mwili wa mfanyabiashara huyo maarufu nchini Tanzania utarejea jumatatu na kuagwa siku ya Jumanne katika viwanja vya Karimjee.

Siku ya Jumatano Mei 8, 2019 mwili utasafirishwa kwenda Machame mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika siku ya Alhamisi Mei 9, 2019.

"Baada ya mwili kuwasili Machame ibada ya mazishi itafanyika katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania la Kisereni,"

UPDATE
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi umewasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar

Msafara wa kuelekea hospitali ya Lugalo kuhifadhiwa utaanza majira ya saa 9:45 alasiri na utapita Tazara-Buguruni-Ilala-Kigogo-Magomeni-Kinondoni-Morocco-Bagamoyo Road-Sayansi-Mwenge na kisha Lugalo

IMG_20190506_171239.jpg
IMG_20190506_171232.jpg
IMG_20190506_171225.jpg
 
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dr. Reginald Mengi utawasili nchini siku ya Jumatatu- Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo.

Mwili wa Dr. Reginald Mengi utaagwa siku ya Jumanne Mei 7, katika viwanja vya Karimjee- Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo.

Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame, ibada ya mazishi ni siku ya Alhamis wilayani humo kanisa la Kisereni (KKKT)- Mwanasheria wa familia, Michael Ngalo.
 
Japokua hilo lipo ila ukiwa umetajirika na ukaja tafuta mwanamke dogo dogo lazima udanje maaana huyo dogo dogo atakua yupo fully fledge kutafuta hela...
Kweli Ila sikumaanisha huyu Dada yetu Jacky niliona Jana story ya mke mkubwa Wa marehemu alitarikiwa baada ya kumtegea sumu Mzee Bahati house girl akaokoa jahazi
 
Kweli Ila sikumaanisha huyu Dada yetu Jacky niliona Jana story ya mke mkubwa Wa marehemu alitarikiwa baada ya kumtegea sumu Mzee Bahati house girl akaokoa jahazi
Nilielewa mkuu ulichisema ila hilo ni angalizo tu kwa wazee wanaowafata vijana...
 
Back
Top Bottom