Mwili wa Binadamu hauna Spares

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,880
MWILI WA MTU HAUNA SPARES (VIPURI).

Na, Robert Heriel

Kwa masikitiko makubwa natoa pole kwa wazazi na ndugu wa Emanuel Mlelwa ambaye Mwenyekiti wa Seneti Vyuo Vikuu Iringa aliyeuawa na watu wasiojulika huko Iringa. Pia niwape Pole wana-UVCCM Na CCM kwa ujumla kwa kuondokewa na kijana wenu.

Kama ilivyo kwa mauaji mengine, ninalaani na kukemea tabia hii ovu ambayo inaumiza na haipendezi hata kidogo. Serikali kupitia vyombo vyake vya dola hakikisheni waliofanya mauaji ya kijana huyu, pamoja na watu wengine waliouawa wanapatikana na kuwajibishwa.

Sisi sote ni Ndugu, sote ni Watanzania. Tumezaliwa ndani ya nchi moja, lazima tupendana. Kwa nini umuue mwanadamu mwenzako wakati sheria zipo, kwanini?

Ndugu zangu, Mwili wa Binadamu hauna Spare, tunapaswa kuulinda na kuheshimu kwa maana umeumbwa kwa gharama kubwa sana na Mungu wetu. Huwezi ua mtu ambaye hujamuumba kienyeji. Unawezaje kumuua mtoto wa mtu. Unawezaje kumteka na kumjeruhi mtoto wa mtu?

Mbona usimuue mtoto wako?
Mbona usimjeruhi Baba yako au Mama yako?
Mbona usimuue mke wako au Mume wako?

Hata watu hao pia hupaswi kuwafanyia uhuni uhuni. Hii ni tabia ya kishetani, tania za kuzimu. Lazima ipigwe vita.

Unakuta jitu limeoa mtoto wa watu, linaanza kumshushia kipondo mpaka linamtoa jicho au kumvunja mikono. Jamani mwili wa binadamu hauna Spare, ukilitoa jicho ndio basi tena, ukiukata mkono ndio basi tena. Kwa nini ufanye ukatili wa namna hii? Kama umeshindwana na mtu taratibu si zipo. Mpe talaka mtoto wa watu.

Unampiga risasi mtoto wa watu, sio mwizi, sio muuaji, hajakukosea chochote, na hata kama amekukosea taratibu za kisheria zipo. Wewe unampiga mtu risasi, huo ni unyama. Na tutaulaani siku zote Dunia ingalipo.

Huwezi nyima haki ya mtu kuishi bhana. Wewe sio Mungu, hata shetani mwenyewe hana haki ya kunyima watu haki za kuishi sembuse wewe mwanadamu.

Tunalaani mauaji yoyote ndani ya ardhi yetu. Kumwaga Damu ya mtu bila utaratibu ni kuilaani ardhi ya nchi yetu wenyewe. Hatuwezi kubaliana na wapumbavu wachache wanaotaka kutuharibia nchi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Back
Top Bottom