Mwili umekosa kichwa

Mwili umekosa kichwa

Kichwa huweka mipango,kuyaongoza matendo, huvitawala viungo, viungane kwa upendo, kama kugeuza shingo, miguu yapunguza mwendo, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Kichwa ukikosa mwili, kiwiliwili jeuri, miguu yadai nauli, ili kuanza safari, japo haioni mbali, itazikwepa hatari, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Tumbo limejaa choyo, mpaka laitwa kitambi, laubana mpaka moyo, lina kiburi na dhambi, njaa likishikwa nayo, halitumii maombi, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Mikono ni watumishi, kuuhudumia mwili, kuuosha kwa marashi, ukanukie utuli, mbona yaleta ubishi, kwa mapete na bangili, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Panapoleta uzazi, napo pametaharuki, padai kukaa wazi, bila kificho ni haki, heshima yake mavazi, kama shombo na samaki, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Sijui kati ya watu, nani kichwa nani mwili, kama wapo baai fyatu, wamezikoaa akili, ilani yao si kitu, wameendekeza dili, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Mijini pakini gari, kwa gharama ya dizeli, vijijini ni sukari, tunyweni kwa pilipili, ujenzi tumeghairi, malighafi bei ghali, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Kazi wameiharibu, baba alipofariki, wote wana masharubu, walikuwa wanafiki, hawajali zetu tabu, wagombania miliki, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Watatutupa shimoni, waliokosa akili, tuchambue kwa makini, tupate wenye adili, tuwaache mashetani, wenye tamaa ya mali, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

Hapo ishirini na tano, Mola atupe pumzi, tumeshaona mifano, tutafanya maamuzi, tunafanya maagano, kuwatupa wapuuzi, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri,

[emoji2398] 2/12/2021
Nani kakwambia ushindi wa ccm inategemea kura yako? We kapige tu lakini Haina impact yoyote
 
Nani kakwambia ushindi wa ccm inategemea kura yako? We kapige tu lakini Haina impact yoyote
Mkuu wanapogombana makundi mawili lazima kuna mwwnye haki na muovu, kuna giza na nuru , hata magu alikuwa na wapinzani ndani tunaowaona leo, si lazima itoke ccm, hii inaweza kuwa fursa mpasuko huu kutupa nafasi ya kuchagua wazalendo, sio kweli kuwa ccm wote hawafai, tuwape nguvu team uzalendo,
 
Shairi zuri ila mpangilio wake unachosha kulisoma. ILA MESEJI IMEFIKA
Nadhani mpangilio ulikuwa ni sahihi... inaonekana shahidi ni knowledgeable labda tumuulize alimiliki nyaraka hii tangu lini, ila najua mada ni relevant.... tuzingatie chain of custody 2025 kwa kùwa ameifafanua vyema...
 
Nadhani mpangilio ulikuwa ni sahihi... inaonekana shahidi ni knowledgeable labda tumuulize alimiliki nyaraka hii tangu lini, ila najua mada ni relevant.... tuzingatie chain of custody 2025 kwa kùwa ameifafanua vyema...
Contemporary mkuu,
 
Samia anatapatapa Naona ana ziara ya kutembelea wastaafu, bila katiba mpya watu watauana
Majaliwa, Mpango Kabudi, na Mugilu hawa ni MAHARAMIA yanayo muongoza hiki kibibi cha kiarabu.
 
Back
Top Bottom