Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 788
- 1,015
Kichwa huweka mipango, kuyaongoza matendo, huvitawala viungo, viungane kwa upendo, kama kugeuza shingo, miguu yapunguza mwendo, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Kichwa ukikosa mwili, kiwiliwili jeuri, miguu yadai nauli, ili kuanza safari, japo haioni mbali, itazikwepa hatari, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Tumbo limejaa choyo, mpaka laitwa kitambi, laubana mpaka moyo, lina kiburi na dhambi, njaa likishikwa nayo, halitumii maombi, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Mikono ni watumishi, kuuhudumia mwili, kuuosha kwa marashi, ukanukie utuli, mbona yaleta ubishi, kwa mapete na bangili, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Panapoleta uzazi, napo pametaharuki, padai kukaa wazi, bila kificho ni haki, heshima yake mavazi, kama shombo na samaki, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Sijui kati ya watu, nani kichwa nani mwili, kama wapo baai fyatu, wamezikoaa akili, ilani yao si kitu, wameendekeza dili, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Mijini pakini gari, kwa gharama ya dizeli, vijijini ni sukari, tunyweni kwa pilipili, ujenzi tumeghairi, malighafi bei ghali, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Kazi wameiharibu, baba alipofariki, wote wana masharubu, walikuwa wanafiki, hawajali zetu tabu, wagombania miliki, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Watatutupa shimoni, waliokosa akili, tuchambue kwa makini, tupate wenye adili, tuwaache mashetani, wenye tamaa ya mali, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
Hapo ishirini na tano, Mola atupe pumzi, tumeshaona mifano, tutafanya maamuzi, tunafanya maagano, kuwatupa wapuuzi, kichwa umekosa mwili, kiwiliwili jeuri.
[emoji2398] 2/12/2021