Dar Es Salaam.
Member
- Oct 29, 2010
- 25
- 7
Natumai muwazima wana jf,nimekuwa na tatizo ambalo sielewi linasababishwa na nn,nasikia uchovu sana kiasi cha kuhisi kama naumwa na tena muda mwingi nakuwa najisikia kulala,naomba msaada madaktari.
Kuna mambo mengi saana yanayoweza kusababisha uchovu. Cha msingi, mtafute tabibu afanye upembuzi yakinifu. Baadhi tu ya matatizo yanayoweza kukusababishia ujisikie uchovu ni mfano anemia(upungufu wa damu), hypothyroidism(upungufu wa madini ya thyroid), Obstructive sleep apnea(kutopumua vizuri unapokuwa usingizini), infections (malaria, minyoo nk), depression, chronic fatigue syndrome, hiv, malignancy, na kadhalika.
Ni vigumu saana kwa kupata majibu bila ya kumhoji mgonjwa na kufanya vipimo ili kufahamu hasa ni nini kinachoeeza kuwa kinasababisha uchovu.
Nakushauri umtafute tabibu akusaidie kufanya upembuzi huo yakinifu.