Mwigulu anyimwe mic tafadhali anazidi kukera 
----------
Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, amevituhumu vyama vya upinzani, hususan CHADEMA, kwa kile alichodai kuwa ni mkakati wa kutaka kuingiza nchi kwenye machafuko kwa kutumia kigezo cha mabadiliko ya Katiba ili kuchelewesha Uchaguzi Mkuu uliopita.
Akizungumza hivi karibuni na wananchi wa Bunju, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa soko na kituo cha mabasi, Dkt. Mwigulu alidai kuwa upinzani ulikuwa na mpango wa kusogeza mbele uchaguzi ili muda wa kikatiba wa Serikali uishe, jambo ambalo lingetoa mwanya wa kuitisha maandamano ya kuing'oa Serikali madarakani.
Waziri Mkuu alifafanua kuwa Katiba haiwezi kubadilishwa kupitia makubaliano ya vyama vya siasa pekee, bali ni mchakato unaohitaji kura za Watanzania wote.
Akigusia suala la ushindani katika uchaguzi huo, Dkt. Mwigulu alilinganisha hali hiyo na michezo, akisema kuwa wale walioamua kutoshiriki kwa ridhaa yao wasilalamike kuhusu ukubwa wa ushindi wa waliokuwepo uwanjani.