Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

leroy

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2010
Posts
1,622
Reaction score
2,220
Wanajamii kwanza niambatanishe Ushahidi wa kauli ya Mh. Nchemba HAPA.
Nasikitika namna Mh. Mwigulu anavyoidanganya jamii, kuna mambo mawili anayoyabainisha.

La kwanza: Kwamba yeye ni mchumi wa daraja la kwanza kwa maana alipata G.P.A. ya kiwango cha first class (4.4-5).
La pili: Kwamba yeye ni alikua mchumi mwandamizi (Senior Economist) wa Benki kuu.

UKWELI NI UPI??

La kwanza.
Kwenye digrii ya kwanza Hakuwahi kupata first class. Mwigulu Nchemba alianza degree ya Uchumi UDSM mwaka 2001 na kumaliza mwaka 2004. Katika darasa lao kulikua na FIRST CLASS MOJA TU! Aliipata Mkenya anayeitwa George Omondi, na alipata 4.4. Mwigulu alipata Upper Second Class na Darasani alikuwa wa kawaida sana, wapo waliokuwa wakimzidi (Mmoja wao alibakizwa kufundisha UDSM).

Kwenye digrii ya pili napo hakuwahi kupata first class.

La pili.
Hakuwahi kuwa mwandamizi wa Benki kuu. Mwigulu alikuwa mwajiriwa wa Benki kuu tawi la Arusha hadi anaondoka. Akiwa Benki kuu HAKUWAHI KUWA MCHUMI MWANDAMIZI. Aliondoka akiwa mchumi wa daraja la kwanza (Ikumbukwe wengi huajiriwa kama wachumi daraja la pili na kupanda hutegemea umri kazini).

Nawasilisha.
 
So what?..yani umelalaaa, umewazaaa ukaona uje na hili asubuhiasubuhi?
 
maelezo kuhusu degree ya pili kuwa hakuPata 1st class hayajajitosheleza, rudi katafute evidence uje upya. Pia ilete CV iliyopo kwenye tofuti ya bunge uweke hapa tuone wapi unaposema kadanganya.. Ulete pia CV ya mbowe na lema
 
Huyu Mwigulu anapenda kujisifu sana kumbe hakuna kitu.
 
leroy Wivu n ugonjwa usio na tiba ww ulipata ngapi seems ulisoma nae
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na maelezo yooote bado Mwigulu atabaki kuwa Mwigulu Nchemba na Usomi wake.
 
Jk amemfuta kazi naibu waziri wa elimu kwa kufoji, wakati huo huo amempa unaib waziri Mwigulu aliye foji, hii ndo serikali yet dhaifu ilivyo, hapo unategemea nini?
 
maelezo kuhusu degree ya pili kuwa hakuPata 1st class hayajajitosheleza, rudi katafute evidence uje upya. Pia ilete CV iliyopo kwenye tofuti ya bunge uweke hapa tuone wapi unaposema kadanganya.. Ulete pia CV ya mbowe na lema
Chuki zisipumbaze akili yako. Hoja hapa ni Mh. Mwigulu na ikiwa ni baada ya yeye kujitapa elimu yake, wapi ulimskia Mh. Lema na Mh. Mbowe wakifanya hvyo. Jikite kwenye hoja mkuu, na utailinda heshma yako.
 
ujinga mtupu!..sasa wewe unakoroma nini, kwani wewe ni mwigulu? au ni mkewe!...kama mwigulu ametoa taarifa zisizo sahihi ni kiashiria cha jinsi huyo jamaa anavyoishi kwa mizengwe na tabia isiyokubalika katika jamii. Hii ni tabia yake ya ndani kabisa ambayo ninaamini hata wazazi wake walishindwa kumrekebisha.
Ndio maana nakubali kutumiwa na jamaa zake katika kufanikisha mikakati ambayo inatweza/inakiuka haki za binadamu. Hovyo kabisa!!..
 
maelezo kuhusu degree ya pili kuwa hakuPata 1st class hayajajitosheleza, rudi katafute evidence uje upya. Pia ilete CV iliyopo kwenye tofuti ya bunge uweke hapa tuone wapi unaposema kadanganya.. Ulete pia CV ya mbowe na lema

Umenisemea..! Na ya SUGU iwekwe hapa tuone kama walimaliza form four!
 
Back
Top Bottom