Mwigulu Nchemba - Utendaji na Uelewa Wenye Mashaka

KMANGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2014
Posts
674
Reaction score
369
Nachelea kusema Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba hana uelewa wa kutosha juu ya kazi aliyokabidhiwa kwenye wizara nyeti ndani ya taifa hili, Sababu inayonifanya kuwa na mashaka hayo ni kauli niliyomsikia leo akitamka ndani ya vyombo vya habari kuwa baada ya bunge kupitisha bajeti ya Serikali wizara yake itapitia bajeti za kila wizara ili kuzifumua na kuondoa mambo yasiyo na tija,

Swali la kujiuliza ni tangu lini wizara ya fedha ikawa na mamlaka kuzidi bunge na kuwa hivi Nchemba hajui kazi na mamlaka ya bunge. Kama wizara ya fedha itapitia upya bajeti za wizara ambazo kimsingi wizara hiyo ilishazipitia kabla ya kuwasilishwa bungeni, je vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea sasa huko Dodoma sio sahihi na kuwa vitarejelewa upya ili bunge liweze kujadili na kupitisha upya bajeti hizo?

Maswali ni mengi lakini kwa staili hiyo ya Mwigulu inatoa picha halisi ya aina ya viongozi walioko Serikalini na namna utendaji wao pamoja na uelewa wao wa mambo ya msingi ulivyojaa mashaka na utata.
 
Kiumbe kaduwaza wengi si wewe pekee
 
Hivi vyeo vya kupeana utata mtupu,kweli wa propaganda kama mwigullu anapewa wizara nyeti kiasi hicho?
 
Yupo katika wizara hiyo kwa kazi maalum na hakuna kitu kingine kilichomuweka hapo, tunachosubiri ni EPA PART 2
 
Nachelea kusema Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba hana uelewa wa kutosha juu ya kazi aliyokabidhiwa kwenye wizara nyeti ndani ya taifa hili, Sababu inayonifanya kuwa na mashaka hayo ni kauli niliyomsikia leo akitamka ndani ya vyombo vya habari kuwa baada ya bunge kupitisha bajeti ya Serikali wizara yake itapitia bajeti za kila wizara ili kuzifumua na kuondoa mambo yasiyo na tija,

Swali la kujiuliza ni tangu lini wizara ya fedha ikawa na mamlaka kuzidi bunge na kuwa hivi Nchemba hajui kazi na mamlaka ya bunge. Kama wizara ya fedha itapitia upya bajeti za wizara ambazo kimsingi wizara hiyo ilishazipitia kabla ya kuwasilishwa bungeni, je vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea sasa huko Dodoma sio sahihi na kuwa vitarejelewa upya ili bunge liweze kujadili na kupitisha upya bajeti hizo?

Maswali ni mengi lakini kwa staili hiyo ya Mwigulu inatoa picha halisi ya aina ya viongozi walioko Serikalini na namna utendaji wao pamoja na uelewa wao wa mambo ya msingi ulivyojaa mashaka na utata.
Nategemea hili suala liwe swali kwa waziri mkuu alhamisi....
 
Tutegemee kuduwaa zaidi hasa baada ya kuvuliwa skafu..

Unategemea nini wenzake wapo kny bunge la budget yeye busy na siasa uchwara Iringa? Atajifunza vipi wkt hii ndiyo budget yake ya kwanza? Nimeshawahi kusema kuwa kipindi hiki Wizara ya Fedha ni majanga, kuanzia Waziri mpaka manaibu!!
 
Mwigulu anaweza kuwa amesoma na nini..lakini anaonekana kichwani ana vurugu zinazompelekea kuwa na papara..ukiangalia hata matamko yake labda 3% ndo yana utulivu na kujipanga..
 
Yupo katika wizara hiyo kwa kazi maalum na hakuna kitu kingine kilichomuweka hapo, tunachosubiri ni EPA PART 2

Ila awamu hii wakimfanya mzaha wengi wataishia gerezani kama sio kufilisiwa kabisa!
 
Nchii hii bwana burudaaani bank teller anakuwa waziri,boss wa meneja wake
 
Wadau kama kuna mtu ana you tube ya haya maneno aliyosema Naibu waziri wa fedha jana atupie hapa kuna mtu nimemwambia kuwa huyu jamaa aelewi anafanya nini kanibishia. Mimi jana sikuamini kwa kweli inawezekanaje wizara ikafanya marekebisho katika bajeti iliyopitishwa na bunge? au ndo mchezo wanaofanyaga baada ya bajeti wanakaa tena na kuweka vipaumbele kwenye mambo ambayo yana maslahi kwao. Hapo kachemka kijana mwenzetu.
 
Naomba mbunge aombe muongozo kwa spika,sasa kama ni hivyo wanafanya nini pale bungeni
 
Nachelea kusema Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba hana uelewa wa kutosha juu ya kazi aliyokabidhiwa kwenye wizara nyeti ndani ya taifa hili, Sababu inayonifanya kuwa na mashaka hayo ni kauli niliyomsikia leo akitamka ndani ya vyombo vya habari kuwa baada ya bunge kupitisha bajeti ya Serikali wizara yake itapitia bajeti za kila wizara ili kuzifumua na kuondoa mambo yasiyo na tija,

Swali la kujiuliza ni tangu lini wizara ya fedha ikawa na mamlaka kuzidi bunge na kuwa hivi Nchemba hajui kazi na mamlaka ya bunge. Kama wizara ya fedha itapitia upya bajeti za wizara ambazo kimsingi wizara hiyo ilishazipitia kabla ya kuwasilishwa bungeni, je vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea sasa huko Dodoma sio sahihi na kuwa vitarejelewa upya ili bunge liweze kujadili na kupitisha upya bajeti hizo?

Maswali ni mengi lakini kwa staili hiyo ya Mwigulu inatoa picha halisi ya aina ya viongozi walioko Serikalini na namna utendaji wao pamoja na uelewa wao wa mambo ya msingi ulivyojaa mashaka na utata.
Mawazo yangu ni kuwa alimaanisha wanapitia sasa bajeti za wizara kabla hawajaipitisha Bungeni, maana katika nchi ya kidemokrasia bajeti ya Serikali inakuwa bajeti ya matumizi tu pale inapopitishwa na bunge na kama kuna mabadiliko yanapaswa kupitishwa na bunge! Bahati mbaya sikusikia akiongea lakini nilielewa hivyo.
 
Wana jamvi hebu tuwe self adjustable kidogo,tusikurupuke kwa wivu kwa sababu aliyesema ni mwigulu na muna bifu naye,hebu fikiria kwa miaka takribani mitano imepita hakuna bajeti iliyojitosheleza wala iliyotekelezwa kwa asilimia 100,hapa nilivyomuelewa ni kuwa kwa vile kuna budjet deficit basi kidogo muhimu kilichopo kitakwenda kwenye matumizi muhimu,hapa amesisitiza kutoa priority kwa matatizo ya msingi kwani kupanga ni kuchagua.kuifumua budjet haina maana uianalyse upya bali wizara itatoa kipaumbele kwa matumizi ya msingi ndani ya kila wizara na yale yasiyo ya msingi yataachwa kwa vile budjet haitoshi.nafikiri alimaanisha hili wanajamvi.
 
Nachelea kusema Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba hana uelewa wa kutosha juu ya kazi aliyokabidhiwa kwenye wizara nyeti ndani ya taifa hili, Sababu inayonifanya kuwa na mashaka hayo ni kauli niliyomsikia leo akitamka ndani ya vyombo vya habari kuwa baada ya bunge kupitisha bajeti ya Serikali wizara yake itapitia bajeti za kila wizara ili kuzifumua na kuondoa mambo yasiyo na tija,

Swali la kujiuliza ni tangu lini wizara ya fedha ikawa na mamlaka kuzidi bunge na kuwa hivi Nchemba hajui kazi na mamlaka ya bunge. Kama wizara ya fedha itapitia upya bajeti za wizara ambazo kimsingi wizara hiyo ilishazipitia kabla ya kuwasilishwa bungeni, je vikao vya bunge la bajeti vinavyoendelea sasa huko Dodoma sio sahihi na kuwa vitarejelewa upya ili bunge liweze kujadili na kupitisha upya bajeti hizo?

Maswali ni mengi lakini kwa staili hiyo ya Mwigulu inatoa picha halisi ya aina ya viongozi walioko Serikalini na namna utendaji wao pamoja na uelewa wao wa mambo ya msingi ulivyojaa mashaka na utata.

Unaweza kushangaa kuwa hayo aliyoyasema ndio mawazo hata ya Boss wao. Inawezekana ndio mchezo wao siku zote. Hujiulizi ni kwa nini mwaka wa fedha unakwisha lkn wizara karibu zote zimepokea fedha za bajeti chini ya 50%?
 
Wana jamvi hebu tuwe self adjustable kidogo,tusikurupuke kwa wivu kwa sababu aliyesema ni mwigulu na muna bifu naye,hebu fikiria kwa miaka takribani mitano imepita hakuna bajeti iliyojitosheleza wala iliyotekelezwa kwa asilimia 100,hapa nilivyomuelewa ni kuwa kwa vile kuna budjet deficit basi kidogo muhimu kilichopo kitakwenda kwenye matumizi muhimu,hapa amesisitiza kutoa priority kwa matatizo ya msingi kwani kupanga ni kuchagua.kuifumua budjet haina maana uianalyse upya bali wizara itatoa kipaumbele kwa matumizi ya msingi ndani ya kila wizara na yale yasiyo ya msingi yataachwa kwa vile budjet haitoshi.nafikiri alimaanisha hili wanajamvi.

Na wewe ni walewale, kama kuifumua bajeti ifumuliwe bungeni, ikishapitishwa hana mamlaka ya kufumua na kuweka vipaumbele vyake. Au division five ndio inakusumbua hujui hata sheria na taratibu za kuendesha nchi.
 
Mambo ya msingi ni kama ifuatavyo:: TUMBO NIACHIE NIMWACHIE MANDAWA NA MANENGE CHAKULA!!

Uchaguzi unakuja huuuuoooo!!!!
 
OFKOZI huyu jamaa hana weledi wa kutosha na bila shaka huyu jamaa amewekwa hapo kwa sababu moja tu maalumu nayo ni kufanikisha uchaguzi mkuu 2015
 
Back
Top Bottom