Sasa nimeelewa kwa
nini CCM wahahunyahunya na harakati za kumchafua Dr.
Slaa; kumbe Bwana huyo ni noma kwao!
Jambo jingine pia nililokuwa silifahamu ni kwamba mtu akiwa m-CCM hata
akili kidogo alizojaliwa hupeperushwa na hubaki mweupee kama kijana huyu
niliyekuwa namheshimu kama msomi.
Kutapatapa kwa CCM ni daalili tosha kwamba CHADEMA wamewashika CCM
pabaya na sasa wame-resort kutapatapa na kauli za ki ramli ramli vile!
Kinachopaswa kufanywa na CHADEMA kwa sasa ni kuongeza mbinyo kwa
walegevu hawa kabla ya kuwashushia pigo kubwa litakalowaduwaza na
kuwamaliza kabisa 2015.
Wamejaribu kila njia na kushindwa
vibaya. Wamejaribu kuwanunua viongozi (kina
Kaburu, Akwilombe na wengine watakaofuata) wameangukia pua;
wameweka mapandikizi ya kina Shibuda na Shonza - wapi!
wamejaribu kutumia Polisi 'kuwanyonga' walioonekana kushabikia
CHADEMA kama walivyofanya kule Arusha, Songea, Morogoro, Iringa
na sehemu kadhaa; wapi. Wametumia Usalama wa Taifa kuwateka, kuwatesa na
hata kuwasababishia ulemavu lakini ndiyo kwanza wameimarika zaidi! Na
hili la sasa la kuropokaropoka mithili ya mtu
aliyefunguliwa toka kwenye kibuyu litashindwa vibaya kama lile la
kijinga la ati Dr. Slaa ana kadi yao na wanapokea ada yake! Naona
wamefyata baada ya kubanwa na vipengele vya Katiba yao
wenyewe. Na sasa wamerukia fani za watu - za unajimu na ramli -
watashindwa na kuaibika vibaya pia!
Waacheni waweweseke jamani ukoloni ni mtamu kwa mtawala,
si mmeona jinsi ilivyokuwa vigumu kuwaondoa wareno na walowezi kule
kusini?
Mwisho nasema tu CHADEMA ni A luta
continua!