Mwigulu Nchemba bado Mwiba mbio za Urais

Robert PR

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
591
57
Mwigulu Nchemba hakamatiki Urais. Ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Maendeleo la Utafiti la Elimu (Tedro), iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Katerri, alisema ripoti hiyo ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji watu 2,000 kutoka vijijini na mijini. Alisema katika ripoti hiyo kipengele cha watangaza nia walioshuhudiwa na watu wengi katika hotuba, Lowassa anaongoza kwa kushuhudiwa kwa asilimia 54, akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (46), Naibu Waziri wa Fedha , Mwigulu Nchemba (44), Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira (40) na Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (39).

Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba(34), Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya (31), Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere (27), Waziri wa Ujenzi, John Magufuli (23), na Mbunge wa Sengerema, Willium Ngeleja (19) na wengine wakifuata.

Katika Kipengele cha kupunguza tatizo la ajira, ripoti hiyo ilieleza kuwa wananchi walipohojiwa walieleza kuwa wana imani na Lowassa kwa asilimia 19, Nchemba (14), Magufuli (13). Makamba (13), Membe (12), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (10), Mwandosya (7), Dk. Harrison Mwakyembe (7), Wassira (2) na wengine (3).

"Utafiti huu umebaini kuwa watangaza nia wengi pamoja na mambo mengine walijikita sana katika kusema watatatua tatizo la ajira kwa vijana," alisema Kaserri. Kadhalika ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha kuinua elimu nchini, ambacho wananchi waliohojiwa walitoa nafasi kubwa ya uwezekano wa kutekelezewa kwa kipaumbele hiki kwa Lowassa kwa asilimia 25. Nchemba (18), Membe (16), Makamba (13), Magufuli (12), Mizengo Pinda (12), Wasira (3) na wengine (9).

Pia ripoti hiyo ilizungumzia kipengele cha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo waka 2025, na wananchi walikuwa na imani na Nchemba kwa asilimia 13.4 kuwa ataweza kulipeleka taifa kufikia kipato cha kati. Lowassa (11), Wasira (9), Membe (9.20), Magufuli (9.0), Makamba (5.3), Mwandosya (4.60), Pinda (3.5) na Dk. Mwakyembe (1.40).

Hata hivyo, utafiti huo ulielezea kipengele cha kuinua sekta ya Kilimo na Mifugo nchini ambacho kwa watangaza nia hao, wananchi walikuwa na imani kwa Pinda kwa asilimia 23. Lowassa (17), Nchemba (16), Membe (11) Wasira (9), Makamba (7), Magufuli (5), Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (3.3), Mbunge wa Nzega, Hamisi Kigwangala(3.2) na Mwakyembe (2.6).

Katerri alisema utafiti huo pia ulihusu kipengele cha Utawala bora na vita dhidi ya ufisadi ambapo ulionyesha kuwa Mwigulu Nchemba amepata asilimia 17.4 ya uwezo wa kupambana na tatizo hilo. Wengine waliomfuata ni Magufuli (14.2), Membe (11), Lowassa (6.10), Jaji Ramadhani (6) na Mwandosya (5).

Wengine ni Mizengo Pinda (8), Mwakyembe (8), Makamba (7), Samuel Sitta (6), Dk. Kigwangala (3). Katika kipengele za Uadilifu usiotiliwa shaka katika utumishi Nchemba alipata asilimia 15, Membe (13), Mwandosya (13), Pinda (8), Makamba (8) Jaji Ramadhani (7), Lowassa (10%).

Katika kipengele cha hotuba iliyo bora, Katerri alisema Nchemba alipata alama (A), Wasira( B+), Membe (B+), Mwandosya (B+) Lowassa (B) na Membe (B). Katerri Alisema lengo la utafiti huo ni kutathmini Elimu katika Nyanja ya uraia kwa watanzania kupitia vipaumbele katika hotuba za waliokwisha kutangaza nia kupitia CCM.

Alizitaja wilaya ambako utafiti huo ulifanyika kuwa ni Kinondoni, Kibaha Vijijini, Kilombero, Rombo, Arumeru, Mbulu na Babati, Lindi, Mtwara, Njombe mjini, Njombe Vijijini, Mbeya Mjini, Nyamagana, Biharamulo, Tabora, Nzega, Bahi, Chamwino na Kasulu.
 
Mwigulu Nchemba hakamatiki Urais.
Ripoti ya utafiti
uliofanywa na Shirika la Maendeleo
la Utafiti la Elimu (Tedro),
iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam
jana.
Akizungumza katika uzinduzi huo,
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob
Katerri, alisema ripoti hiyo
ilijumuisha Wilaya 20 na kuwahoji
watu 2,000 kutoka vijijini na mijini.
Alisema katika ripoti hiyo kipengele
cha watangaza nia walioshuhudiwa
na watu wengi katika hotuba,
Lowassa anaongoza kwa
kushuhudiwa kwa asilimia 54,
akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bernard Membe (46), Naibu Waziri
wa Fedha , Mwigulu Nchemba (44),
Waziri wa Kilimo, Chakula na
Ushirika, Steven Wasira (40) na Jaji
Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani
(39).
Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, January Makamba(34),
Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Profesa
Mark Mwandosya (31), Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki,
Makongoro Nyerere (27), Waziri wa
Ujenzi, John Magufuli (23), na
Mbunge wa Sengerema, Willium
Ngeleja (19) na wengine wakifuata.
Katika Kipengele cha kupunguza
tatizo la ajira, ripoti hiyo ilieleza
kuwa wananchi walipohojiwa
walieleza kuwa wana imani na
Lowassa kwa asilimia 19, Nchemba
(14), Magufuli (13).
Makamba (13), Membe (12), Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda (10),
Mwandosya (7), Dk. Harrison
Mwakyembe (7), Wassira (2) na
wengine (3).
"Utafiti huu umebaini kuwa
watangaza nia wengi pamoja na
mambo mengine walijikita sana
katika kusema watatatua tatizo la
ajira kwa vijana," alisema Kaserri.
Kadhalika ripoti hiyo ilizungumzia
kipengele cha kuinua elimu nchini,
ambacho wananchi waliohojiwa
walitoa nafasi kubwa ya uwezekano
wa kutekelezewa kwa kipaumbele
hiki kwa Lowassa kwa asilimia 25.
Nchemba (18), Membe (16),
Makamba (13), Magufuli (12),
Mizengo Pinda (12), Wasira (3) na
wengine (9).
Pia ripoti hiyo ilizungumzia
kipengele cha Tanzania kuwa nchi ya
kipato cha kati ifikapo waka 2025, na
wananchi walikuwa na imani na
Nchemba kwa asilimia 13.4 kuwa
ataweza kulipeleka taifa kufikia
kipato cha kati.
Lowassa (11), Wasira (9), Membe
(9.20), Magufuli (9.0), Makamba
(5.3), Mwandosya (4.60), Pinda (3.5)
na Dk. Mwakyembe (1.40).
Hata hivyo, utafiti huo ulielezea
kipengele cha kuinua sekta ya Kilimo
na Mifugo nchini ambacho kwa
watangaza nia hao, wananchi
walikuwa na imani kwa Pinda kwa
asilimia 23.
Lowassa (17), Nchemba (16),
Membe (11) Wasira (9), Makamba
(7), Magufuli (5), Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu (3.3),
Mbunge wa Nzega, Hamisi
Kigwangala(3.2) na Mwakyembe
(2.6).
Katerri alisema utafiti huo pia ulihusu
kipengele cha Utawala bora na vita
dhidi ya ufisadi ambapo ulionyesha
kuwa Mwigulu Nchemba amepata
asilimia 17.4 ya uwezo wa
kupambana na tatizo hilo.
Wengine waliomfuata ni Magufuli
(14.2), Membe (11), Lowassa (6.10),
Jaji Ramadhani (6) na Mwandosya
(5).
Wengine ni Mizengo Pinda (8),
Mwakyembe (8), Makamba (7),
Samuel Sitta (6), Dk. Kigwangala (3).
Katika kipengele za Uadilifu usiotiliwa
shaka katika utumishi Nchemba
alipata asilimia 15, Membe (13),
Mwandosya (13), Pinda (8),
Makamba (8) Jaji Ramadhani (7),
Lowassa (10%).
Katika kipengele cha hotuba iliyo
bora, Katerri alisema Nchemba
alipata alama (A), Wasira( B+),
Membe (B+), Mwandosya (B+)
Lowassa (B) na Membe (B). Katerri
Alisema lengo la utafiti huo ni
kutathmini Elimu katika Nyanja ya
uraia kwa watanzania kupitia
vipaumbele katika hotuba za
waliokwisha kutangaza nia kupitia
CCM.
Alizitaja wilaya ambako utafiti huo
ulifanyika kuwa ni Kinondoni, Kibaha
Vijijini, Kilombero, Rombo, Arumeru,
Mbulu na Babati, Lindi, Mtwara,
Njombe mjini, Njombe Vijijini, Mbeya
Mjini, Nyamagana, Biharamulo,
Tabora, Nzega, Bahi, Chamwino na
Kasulu.

Hizi mimi kwa sasa naziita ripoti makamasi za kiutafiti.
 
Kumbe Mwigulu bado yupo, sijamsikia kitambo zaidi ya kuona maandishi ya jina lake kwenye mawe tu huko mikoani.
 
Maajabu haya, ni lin Magufuli alitoa hotuba juu ya urais?

Inanikumbusha UDSM kuandaa kura za maoni feki bahati mbaya hawapo smart.

Hilo pembeni, best wishes Mwigulu.
 
Back
Top Bottom