Mwigulu Nchemba azungumza na wananchi walioathiriwa na mvua Kilosa

Mwigulu Nchemba azungumza na wananchi walioathiriwa na mvua Kilosa

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
261
Reaction score
199
- Autaja mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi maji ya Mvua eneo la Kidete.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 02, 2026 amezungumza na wakazi wa Tindiga wilaya ya kilosa mkoani Morogoro ambao wameathirika na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaeleza wakazi hao kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ilishaanza mikakati ya kukabiliana na athari za mvua katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa morogoro kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa Mabwawa eneo la Kidete.

Amesema kuwa ujenzi wa mabwawa hayo ya maji yatakuwa ni suluhisho la kudumu ya mafuriko katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro.

Ameongeza kuwa kwa sasa mpango huo upo katika hatua za kitalaam ikiwemo kumpata mkandarasi.

Fedha imepatikana kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa kwa sasa tunaendelea na taratibu za kitaalam, Wizara zinazohusika hakikisheni mnakamilisha taratibu hizo ili ujenzi uanze”

IMG-20260102-WA0073.jpg
IMG-20260102-WA0072.jpg
IMG-20260102-WA0075.jpg
IMG-20260102-WA0074.jpg
IMG-20260102-WA0076.jpg
 
Back
Top Bottom