Vijana wa Taifa Tanzania na Afrika kwa ujumla wake tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa kiongozi huyu makini ambaye ki ukweli ni alama halisi ya utii , bidii, utu wema na unyenyekevu uliotukuka na usio na chembe ya unafki. Mwigulu katika muda wote wa utumishi wake kama mwakilishi/mbunge, utumishi ndani ya chama CCM na hata serikalini ameonesha uwezo mkubwa katika kuhudumia wananchi na kutii mamlaka.
Mwingulu hana kashfa yoyote iwe ni ndogo au kubwa, iwe ni rushwa au matumizi mabaya ya madaraka. Mwigulu ni mvumilivu na mstahimilivu mno. Amejawa utii na ni mwenye kuheshimu walio juu yake na hata walio chini yake yaani wale wa daraja la chini kabisa. Viongozi vijana wa karba ya Mwigulu ni wachache mno na kwake yeye tunaweza kujifunza namna nzuri ya kuishi na kutenda pasipo kulewa madaraka.
Yako mengi ya kuandika kuhusu kiongozi huyu mwenye sifa lukuki na ipo siku nitaandika kitabu ili kiwe mwongozo na kumbukumbu kwa kizazi cha sasa na baadae.
Wito: viongozi vijana wa Tanzania na hata wale wanaotamani kuingia kwenye siasa /uongozi kwake Mwigulu kuna mengi ya kujifunza.
Mungu tulindie kiongozi huyu. Kwake yeye tunaiona nyota ing'arayo ambayo inatoa mwangaza na tumaini kuu la baadae.