Mwigulu, Nape na Lusinde mnatupeleka wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigulu, Nape na Lusinde mnatupeleka wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Siasaniupendo, Apr 9, 2012.

 1. S

  Siasaniupendo Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya chaguzi ndogo mbili,Igunga na Arumeru Mashariki, tumeona vitendo vya umwagaji damu, lugha za matusi na rushwa. Mh Mwigulu, msomi wa hali ya juu na meneja wa kampeni nini tadhimini yako baada ya hizi chaguzi?
  Mh Nape nawe pia ni msomi, tupe tafsiri ya ccm kuwa na walinzi (green guards), kwani police wameshindwa kazi?
  Lusinde, Je unawafundisha nini watoto wako?
   
 2. C

  Chiume Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani mkulu TUANZE NA KAULI YA MWANZILISHI NA MSHAURI MKUU WA CHADEMA( Brain ya CDM) MZEE MTEI JUU YA UDINI KWENYE TUME YA KATIBA!!! SHAME ON CHADEMA....
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Hiyo ya mtei haina mashiko,mbona wakongwe wenu wa magamba wanaongeaga fyongo ktk ushauri kwenu? Kwani mtei ndo chadema? Ana cheo kipi? Mbona mliponda alivyoshauri zitto achinjwe uchaguzi mwenyekiti? Mlisema ahusiki nasi 2mekubali ahusiki...leteni hoja yenye mashiko.Mbona waziri wenu kasema kikwete ana mapepo hatuongei.
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tarajia kitu toka kwa Mwigulu and not Nape.
   
 5. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  shame on you! Mtei is right, zanzibar hakuna christians? Wacha kutumia akili za shomolo, ukweli wa mzee mtei ukuuma??
   
 6. M

  Murukulazo JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 576
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  lisemwalo lipo kama halipo.......!!
   
 7. E

  Eddi New Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani kiongozi kama Lusinde sio mfano wa kuigwa, kama ningelikuwa na uwezo ningempa Lusinde kazi ya kuimba taarabu, kwani inaonekana kwamba anaweza kukaa kimwambao. Tulichotegemea kutoka kwa Lusinde ni kutoa hoja, sio matusi kama yale. Kwa kweli huo ni ukosefu wa busara na adabu. Kushindana kwa hoja ndilo jambo la muhimu kuliko kupayuka payuka bila kujua unachokisema.:kev:
   
 8. m

  mopaomokonzi JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lusinde ndiyo kiboko cha watukanaji, walikuwa wanajifanya wanajua kutukana sasa kwa lusinde ni break
   
 9. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Nionavyo mimi hawa wote ni vijana ambao wameamua kuendleza career zao katika nyanja za siasa. Kwa vyovyote vile wana malengo makubwa katika career hiyo kwa kuzingatia kuwa ndiyo tu safari zao kisiasa ni changa. Hata hivyo, bila wao kujua kinachendelea kwa sasa watajikuta safari yao inaishia njiani. Endapo kutaendelea kuwepo na changuzi ndogo na mambo ya yakaendelea kama ilivyokuwa kwa Igunga na Arumeru, watu kuacha kuuza sera na kueleza jinsi watakavyoshughulikia matatizo ya wananchi basi jamii baadaye itaamini kumbe vijana walioaminiwa kuwa wataleta mageuzi ya kiasia na kuwa chachu ya kusukuma masuala ya maendeleo mbele ili wajijengee heshima katika career hiyo, siyo waadilifu na hawajui chochote juu ya maisha ya mtazania zaidi ya mipasho. Mwisho wa siku watashindwa kujipigia kura wenyewe kwa kuwa umma ukiwasikia tu utawakimbia kwa kuogopa kusikiliza matusi mbele ya watoto wao, kaka, na dada zao au wazai wao suala ambalo ni kinyume na maadilia ya mtanzania. Ni vyema kujitathmini matarajio yao ya mbeleni kwenye siasa vinginevyo wanaweza kujichimbia kaburi katika ulingo wa siasa za Tanzania. Kwa sasa wazee wanawatumia ili kuwaangamiza na kuaminisha umma kuwa wazee bado ni muhimu kwa kuwa kazi ya vijana ni kutukana.
   
 10. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nadhani hakuna lingine zaidi ya hilo mnaloweza kujisifu nalo, ushenzi na ubazazi tu na huwa mnaujua. Kama ccm walitukanwa walitukwaje na kwanini matusi hayo yasisambae kama ya Lusinde na vyombo vya habari mnavyo vya kutosha? Tafuta mema ya kujisifu nayo siyo hayo bongolala wewe!!!!
   
 11. M

  MGIDEON Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu daima hamfichi mnafiki.Isingekuwa rahisi kwa CCM kushinda kwa aina ile ya kampeni walizofanya Arumeru.Kampeni zimejaa matusi,uongo na kejeli kibao.Hivi watu wa kusaidia kampeni ndan ya chama wamekwisha? Kulikoni kuwaleta hao?
   
 12. k

  kwitega Senior Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwigulu Nchemba na Lusindo ni uchafu katika siasa za Tanzania. CCM imejaa makapi yanayonuka rushwa, matusi na ujinga mwingine mwingi tu. Hivyo kauli zao haziwezi kutushangaza wala kutushtua maana ndivyo walivyo. Hawana sera, sera zao ni matusi, uchakachuaji na ufisadi. Lakini wao na wapambe wao wajue kuwa, uchafu wao una mwisho wake nao uko karibu. Ole wao mafisadi, ole wao wenye midomo inayonuka matusi. siku hiyo hawataamini macho na masikio yao.
   
 13. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Tuache unafiki kwani ni siri kusema kuwa tume ya maandalizi ya katiba mpya ina udini? Ni jambo liko wazi, tume ina waisilamu 19 na wakristo 11 katika nchi kama ya Tz tusijejivunia mbinu chafu hizi. Mi nawapenda wakenya tunawaita wana ukabila lakini wanasema pale pale kwamba rais kateua asilimia hizi toka kabila hili au dini hii wakati uhalisia huenda ungekuwa huu. Hii imewasaidia wao. Sisi watanzania, tunajifanya kuogopa kutoa maoni eti haya ni mambo nyeti tusiyaongelee. Katika hili, JK ni mdini na ana agenda ya udini kwenye katiba hii. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye kutaka kuona bila kuvaa miwani ataona tu!
   
Loading...