Kingcobra
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,000
- 309
Wadau,
Leo kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia kituo cha ITV nimemwona Bw. mwigulu mchemba akimlalamia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mhe. Mbowe kwamba eti alimwandikia kimemo cha vitisho. Bila aibu anasema eti hali hiyo ilijitokeza baada ya yeye kuipitia bajeti ya upinzani na kuitupilia mbali baada ya kuona hakuna cha maana.
Kinachonishangaza ni namna kibuli kilivyomjaa Bw. mchemba kiasi cha kutotambua kwamba kitendo cha kuitupa bajeti iliyoandaliwa na Kambi Rasmi ya Upinzani usiku na mchana kilikuwa ni ishara ya dharau kubwa isiyoweza kuvumilika kamwe.
Kimsingi, mpaka leo bado najiuliza ilikuwaje spika hakumchukulia hatua za kinidhamu Bw. mchemba kwa kitendo hicho cha dharau na dhihaka kubwa kwa upinzani makini kama wa CHADEMA!!!