Mwigulu hata hili la uvamizi wa mkutano wa CUF nalo utanyamaza?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,319
72,742
Wewe ndio kiongozi unayesimamia usalama wa RAIA na Mali zao ndani ya mipaka ya nchi. Sina mashaka na uwezo wako kiutendaji ila mashaka yangu ni jinsi ulivyo geuka bubu tokea upewe wizara hii na hasa unapo paswa kutolea kauli matukio yenye harufu za uhusika wa serikali.

Nikuulize tuu, jee na hili la uvamizi mkutano wa ndani wa CUF na watu kwenye silaha mbalimbali ikiwemo bastola nalo utanyamaza?
Anatajwa Lipumba kuhusika jee utahakikisha polisi wako wanamuondolea "kinga" ya kutokamatwa?

Tunajua pengine kuna uthibiti umefanywa dhidi yako ndio maana hufurukuti, lakini wewe bado kijana na una future katika siasa, mbona unakubali kuififisha? Hujui kimya chako (au woga) unakujengea picha kuwa wewe ni dhaifu na legelege asiye weza madaraka?

Ni katika kipindi chako tuu ndio tumeona silaha zinatolewa kweupe mchana na hakuna anaye chukuliwa hatua huku mamlaka zikihusishwa.
Fanya jambo Mwigulu na heshima yako itasimama juu bila kujali kwa sasa mteuzi atakufanyaje.
 
Mmmh!! Mkulu katuamuru tupige kazi,
Lakini kuwa makini ufanyaji wako wa kazi usiiguse hata harufu ya ya Wanakaya,labda anahofia wasije wakaMnape,
 
Inashangaza sana huyu kuwa kimya kwa siku nzima ya leo baada ya tukio hili. Halafu bado wanataka kutuaminisha nchi iko salama. Ndiyo hivyo hakuna wa kumnyooshea kidole huyu kama Waziri mzigo kama walivyofanya Nape na Kinana kuwanyooshea vidole baadhi ya Mawaziri mizigo kwenye awamu ya nne.
 
BAK unataka Mwigulu Nchemba aongee nini? Je hujui kuwa ni kada wa CCM na hao ndio halali hadi wahakikishe wanamtepetesha Maalim na kuimaliza nguvu CUF?
 
Mwigulu hata hili hawezi kuthubutu kunyanyua mdomo wake kuhusiana na hili lililotokea la hao 'wahuni' wa Lipumba waliovamia mkutano halali wa CUF ya Maalim Seif kwa kuwa vitendo hivyo vya 'kiuendawazimu' vimekuwa masterminded na Bashite na Baba yake wa kufikia anayeishi pale mjengoni Magogoni, huku vikiratibiwa kwa Karibu na Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Mutungi!

Hakika siyo siri tena kuwa nchi hi watakaosababisha machafuko makubwa kutokea nchini si wengine bali ni Bashite +Magu + Msajili!!
 
ukiwa kwenye upande wa watawala unafikia vyeo vikubwa kwa kuwa na uwezo wa kutetea na/au kuficha uovu unaofanywa,iweje leo aje akemee,lazma wote wakae kimya na kuendelea kutetea tu
 
BAK unataka Mwigulu Nchemba aongee nini? Je hujui kuwa ni kada wa CCM na hao ndio halali hadi wahakikishe wanamtepetesha Maalim na kuimaliza nguvu CUF?
Sasa kama hao watu uliowataja wanaamini kuwa Lipumba ni Mwenyekiti halali wa CUF ni kwanini hao watu wanatumia mbinu hizo za 'kishetani' za kutaka kummaliza Maalim Seif kwa kutaka kutuletea machafuko mabaya hapa nchini?

Kwa kweli muda umefika ambapo hatakiwi mtanzania yeyote kuendelea kukaa kimya iwapo tutataka kuliokoa Taifa letu kuingia kwenye umwagikaji wa damu, bali kukemea kwa nguvu zetu zote mambo haya ya hovyo kabisa yanayotokea hapa nchini huku yakionyesha wazi kuwa yana full blessings of the highest office in our country!
 
Binafsi nilikwishajihapiza, sintokaa nishangae tena kwa yaliyotokea na yanayotokea katika Taifa hili.

Hili la kuvamiwa Maalim Seif, najua ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya chama dola na ma agents wake, kuhakikisha kufikia 2020 hakutakuwa na upinzani katika nchi hii, (hata Bwana Pombe alikwisha liweka wazi jambo hilo).

Ila naamini Mungu ni wetu sote, na ndio maana uumbua na kufichua yaliyo gizani tupate kuyafahamu na kuyaona.

0c5119a9c78c2b565ae0ddb55d65fb36.jpg

YEYE AENDELEE KUKAA KIMYA TU, IKIWEZEKANA AFUNGE NA PLASTA KABISA. LAKINI "MUDA" NDIO UTAONGEA.
 
Wewe ndio kiongozi unayesimamia usalama wa RAIA na Mali zao ndani ya mipaka ya nchi. Sina mashaka na uwezo wako kiutendaji ila mashaka yangu ni jinsi ulivyo geuka bubu tokea upewe wizara hii na hasa unapo paswa kutolea kauli matukio yenye harufu za uhusika wa serikali.
Nikuulize tuu, jee na hili la uvamizi mkutano wa ndani wa CUF na watu kwenye silaha mbalimbali ikiwemo bastola nalo utanyamaza?
Anatajwa Lipumba kuhusika jee utahakikisha polisi wako wanamuondolea "kinga" ya kutokamatwa?
Tunajua pengine kuna uthibiti umefanywa dhidi yako ndio maana hufurukuti, lakini wewe bado kijana na una future katika siasa, mbona unakubali kuififisha? Hujui kimya chako (au woga) unakujengea picha kuwa wewe ni dhaifu na legelege asiye weza madaraka?
Ni katika kipindi chako tuu ndio tumeona silaha zinatolewa kweupe mchana na hakuna anaye chukuliwa hatua huku mamlaka zikihusishwa.
Fanya jambo Mwigulu na heshima yako itasimama juu bila kujali kwa sasa mteuzi atakufanyaje.
Well said Chakaza, Lameck alikuwa mtendaji mzuri sana tangu akiwa naibu waziri Wa Fedha hadi waziri Wa kilimo na mifugo, lakin sielewi nn kimempata sasa
 
Binafsi nilikwishajihapiza, sintokaa nishangae tena kwa yaliyotokea na yanayotokea katika Taifa hili.

Hili la kuvamiwa Maalim Seif, najua ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya chama dola na ma agents wake, kuhakikisha kufikia 2020 hakutakuwa na upinzani katika nchi hii, (hata Bwana Pombe alikwisha liweka wazi jambo hilo).

Ila naamini Mungu ni wetu sote, na ndio maana uumbua na kufichua yaliyo gizani tupate kuyafahamu na kuyaona.

0c5119a9c78c2b565ae0ddb55d65fb36.jpg

YEYE AENDELEE KUKAA KIMYA TU, IKIWEZEKANA AFUNGE NA PLASTA KABISA. LAKINI "MUDA" NDIO UTAONGEA.
Muda utaongea lini!!muda ni ss na hakuna mwingine wa kutimiza ila ww au unataka mwanao ,mjukuu wako?BIG NO inatakiwa ss hata kama wako na siraha lkn kwakile utakachofanya ww razma watie Adabu na ikifika 2020 uchaguzi uwe as haki vinginevyo kwa mambo haya hakutakuwa na mbunge wa upinzani hata mmoja amini usiami hiyo ndo hali halisi wakati wa mapambano ni na kuilekebidha serilika yenye his mbaya ni ss.
 
BAK unataka Mwigulu Nchemba aongee nini? Je hujui kuwa ni kada wa CCM na hao ndio halali hadi wahakikishe wanamtepetesha Maalim na kuimaliza nguvu CUF?
Hasante Sana mkulu, Kwanza tusisahau kuwa vurugu kama hizi hata kuuwa ni biashara pendwa ya Mwigulu, historia yake ni ktk siasa ni shahidi. Anafahamu anaelewa vizuri kinacho endelea, amini nawaambieni hatuwa stahiki hazitachukuliwa dhidi ya wahusika.
 
Mwigulu hata hili hawezi kuthubutu kunyanyua mdomo wake kuhusiana na hili lililotokea la hao 'wahuni' wa Lipumba waliovamia mkutano halali wa CUF ya Maalim Seif kwa kuwa vitendo hivyo vya 'kiuendawazimu' vimekuwa masterminded na Bashite na Baba yake wa kufikia anayeishi pale mjengoni Magogoni, huku vikiratibiwa kwa Karibu na Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Mutungi!

Hakika siyo siri tena kuwa nchi hi watakaosababisha machafuko makubwa kutokea nchini si wengine bali ni Bashite +Magu + Msajili!!
Akumbuke aligombea urais sasa anatudhihirishia kua asingeuweza
 
Nadhani ilikuwa ni mihemuko tu ila kwa sasa atleast tunaiona utendaji wake halisi bila make-up
 
Mwigulu atathubutu kushughulikia suala hili na kuwatafuta wahusika ikiwa tu hataki tena Uwaziri.

Ni lazima ahakikishe anamfurahisha Malaika mkuu na malaika wengine wadogo.

AIBU sana hii kwa kijana kushindwa kuyafanya yale yaliyomo moyoni mwako na ndani ya uwezo wako kwa kuwaogopa watu na kujipendekeza.
 
Hivi Huyu jamaa Yale mabomu ya mikutano ya CDM Arusha,si alikuwa anahusishwa au siku hizi amemrudia muumba wake?
 
Back
Top Bottom