CUF yamwandikia barua IGP na taasisi zinginezo za Serikali kuhusu uvamizi wa Mkutano wao

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,124
Watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba walivamia mkutano wa mwenyekiti wa mkoa na wanahabari wakiwa na bastola, fimbo na mikanda na kutishia maisha, kupiga watu waliokuwa kwenye ukumbi wa hoteli moja jijini na kufanya virugu.

Aidha, upinzani umemtupia lawana Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kuhusu uvamizi huo kwa kuwa hawakutekeleza majukumu yao.

Kadhalika, umelaani kitendo hicho cha uvamizi wa mkutano pamoja na waandishi wa habari kupigwa kwa kuitaka Serikali kutoa tamko na kuchukua hatua kali dhidi ya waliohusika.

Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni wa CUF, Ally Saleh akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema makundi ya uvamizi yamekuwa tishio katika jamii.

“CUF kimeshamwandikia barua IGP na taasisi zinginezo za Serikali kuonyesha matatizo yaliyotokea jana (juzi) na chanzo cha matatizo hayo," alisema Saleh. "Tunangojea Serikali itasema nini juu ya tukio lile.”

Saleh ambaye pia ni Naibu mnadhimu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) bungeni, alisema kitendo kilichotokea katika mkutano wa CUF cha watu kuvamia na kutoa bastola hadharani hakina utofauti na tukio alilofanyiwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Alisema ukimya wa Waziri Mwigulu na Dk. Mwakyembe juu ya tukio hilo umeonyesha hawajatimiza majukumu yao; hususani Waziri Mwakyembe ambaye alipaswa kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa salama.

“Mambo haya yanavyotokea mawaziri wawili tunataka kuwavisha mnyororo Waziri Mwigulu Nchemba na Mwakyembe," alisema.

"Mwakyembe alipaswa kujitokeza kwa haraka na kutoa tamko dhidi ya kitendo walichofanyiwa waandishi, tunahisi kwamba jukumu a Serikali halijatekelezwa, Mwakyembe anapaswa kuhakikisha usalama wa waandishi unakuwapo. Hivyo Mawaziri hawa wawili wanapaswa kutoa tamko."

Alisema kikundi cha Mungiki siyo kigeni hapa nchini na Serikali inakifahamu lakini hakuna hatua zozote ambazo zimeshachukuliwa hadi sasa.

Kadhalika, alisema Kutokana na tukio lililotokea juzi, mkutano wa ndani wa kikatiba uliotakiwa kufanywa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad leo Serikali wameufuta kitendo ambacho siyo sahihi.

Alisema kitendo cha Serikali kuufuta mkutano huo siyo sawa kwa sababu Profesa Lipumba anabebwa na mbereko ya Serikali kwa kufanya mikutano ya ndani kila wakati.

Alisema Serikali inalea Jamhuri ndogo ndani ya Jamhuri, vile vile Serikali imekuwa inalea kambi ndogo ndani ya Buguruni na kwamba wanufaika zaidi wa mgogoro unaoendelea ndani ya CUF ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao dhumuni lao ni kuchukua majimbo yanayoongozwa na CUF katika uchaguzi mkuu ujao.
 
IGP alimwa barua
www.ippmedia.com/sw/habari/igp-alimwa-barua

Nilitaka nimpe alama 100% kwa mtiririko wake uliokuwa mzuri ila kwa kuihusisha CCM huku mwisho wa maelezo yake sasa nampa alama 0% kwani amepotoka na nadhani haijui vizuri vita ya CUF Visiwani na CUF Tanzania bara ambayo kimsingi kabisa inachochewa na wana CUF wenyewe ambao bahati nzuri ni Makada wazuri tu wa Chama.
 
Hili linch ni la hovyo sana.... Badala ya kujikita kwenye mambo ya maendeleo, Serekali ipo busy kufanya mambo ya kipuuzi.
 
Hakuna cha maendeleo watu wanawaza jinsi ya kukaa madarakani milele sasa CCM wamepata kibaraka wao Lipumba.
 
Pale RAIA nao watakapo amua nini wafanye, hatutaki mambo ya kuanza kuihubiri amani.

Haiwezekani watu wapo busy na shughuli zao walau waweze jipoza na ugumu Wa maisha uliopo, alafu wanatokea wahuni wanaanza kutoa bastola hadharani, na serikali iliyopewa dhamana ya kuilinda na kuidumisha amani wanaangalia tu... Mambo haya hayavumiliki
 
Nilitaka nimpe alama 100% kwa mtiririko wake uliokuwa mzuri ila kwa kuihusisha CCM huku mwisho wa maelezo yake sasa nampa alama 0% kwani amepotoka na nadhani haijui vizuri vita ya CUF Visiwani na CUF Tanzania bara ambayo kimsingi kabisa inachochewa na wana CUF wenyewe ambao bahati nzuri ni Makada wazuri tu wa Chama.
acheni unafiki wa kutetea visivyopaswa kutetewa.kila mtu anajua huyo lipumba anapata wapi hiyo jeuri, na kwa maslahi ya nani.msijifiche katika mashamba ya karanga.
 
Nilitaka nimpe alama 100% kwa mtiririko wake uliokuwa mzuri ila kwa kuihusisha CCM huku mwisho wa maelezo yake sasa nampa alama 0% kwani amepotoka na nadhani haijui vizuri vita ya CUF Visiwani na CUF Tanzania bara ambayo kimsingi kabisa inachochewa na wana CUF wenyewe ambao bahati nzuri ni Makada wazuri tu wa Chama.
Unajua nyuma ya lipumba kuna nani?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Nilitaka nimpe alama 100% kwa mtiririko wake uliokuwa mzuri ila kwa kuihusisha CCM huku mwisho wa maelezo yake sasa nampa alama 0% kwani amepotoka na nadhani haijui vizuri vita ya CUF Visiwani na CUF Tanzania bara ambayo kimsingi kabisa inachochewa na wana CUF wenyewe ambao bahati nzuri ni Makada wazuri tu wa Chama.
Mkuu ni Nani wa kuwaamrisha polisi wausapoti upande mmoja Kati ya pande 2 zinazo hasimiana? Polisi wanaonekana kuwa pamoja na mzee Lipumba.
 
Hata Malaika wa Mungu huwa na Yule anayefuata na kuzitii amri Kuu za Mungu na si Yule mwenye Ushetani uliotukuka.
 
Nilitaka nimpe alama 100% kwa mtiririko wake uliokuwa mzuri ila kwa kuihusisha CCM huku mwisho wa maelezo yake sasa nampa alama 0% kwani amepotoka na nadhani haijui vizuri vita ya CUF Visiwani na CUF Tanzania bara ambayo kimsingi kabisa inachochewa na wana CUF wenyewe ambao bahati nzuri ni Makada wazuri tu wa Chama.
Duh! Kutoka 100% mpaka 0%. Uwe fair, mpe 50%.
 
Simpi hiyo kwani amehitimisha ki hovyo hovyo sana Mkuu. Napatwa na wasiwasi kuwa kuna Watu huu ni mwaka wa pili sasa unaenda na sioni wala wakikiimarisha Chama chao zaidi tu ya kila siku kuwekeza kukisema, kukikosoa na kukinanga chama cha CCM huku wakiwa wamesahau kuwa wakati wao wakifanya hivyo wenzao wa CCM ndiyo kwanza wanazidi kujiimarisha kwa kutekeleza Sera zake kitu ambacho hadi kufikia 2020 tayari Wananchi watakuwa wameona maendeleo waliyokuwa wakiyataka na hatimaye kukiweka tena madarakani na hao wanaopoteza muda sasa kama kawaida yao watakuwa wanasema wameibiwa Kura.

Muda haungoji!
 
Back
Top Bottom