Mwigulu: CHADEMA hawatakwenda Ikulu 2015

Mwigulu: CHADEMA hawatakwenda Ikulu 2015

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
[h=2][/h]JUMATATU, DESEMBA 31, 2012 04:48 NA GUSTAPHU HAULE, KIBAHA


NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba, amesema ni ndoto kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kuingia Ikulu. Amesema kwamba hata kama CHADEMA wana nia ya dhati ya kuingia Ikulu, jambo hilo halitawezekana na badala yake wanachama wa chama hicho wanatakiwa kurudi CCM ambako ndiko walikotoka.


Nchemba aliyasema hayo juzi, Kibaha Maili moja alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

“Kama CHADEMA wanategemea mwaka 2015 ndipo waingie Ikulu, wakidhani watapata nafasi ya kushinda, wajue CCM itawasambaratisha mapema na hivyo kubaki wakinyoosheana vidole wao kwa wao.

“Nawaambia CHADEMA ifikapo mwaka 2016 itakuwa imekufa kabisa.

“CHADEMA wanadhani kuingia Ikulu ni jambo jepesi, siyo rahisi kama wanavyodhani kwa sababu hawana nguvu za kuweza kuongoza.

“CCM ni chama ambacho kimeota mizizi katika pembe zote za Tanzania, hivyo itakuwa vigumu kwao CHADEMA kuingia Ikulu.

"Nawaambia ndugu zangu wa CHADEMA, kwamba waache fikra za kutaka kuingia Ikulu mwaka 2015, kwani naamini hawataweza kwa sababu sisi tutawapiga mapema. Ni bora wakafanya kazi za kuwatumikia wananchi ili nchi yetu iwe na maendeleo na ikiwezekana waache kabisa kufikiria suala la uchaguzi wa mwaka 2015,'' alisema Nchemba.

Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi, alisema CHADEMA wanatakiwa kutowadanganya wafanyakazi, kwamba wakiingia madarakani wataweza kuboresha maisha ya wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara.

Alisema kwamba, suala hilo gumu kutekelezwa na chama hicho cha upinzani kwa kuwa hawana uwezo kwa kuwa hata mishahara ya viongozi wao wameshindwa kuiongeza.

"Mimi nafikiri muda wa kuanza kuwadanganya wafanyakazi kuwa wakiingia madarakani watawaongezea mishahara, hilo sio kweli kwani kama wanataka kufanya hilo ni vema wakaanza kuwalipa mishahara hiyo wafanyakazi wao, kwani mpaka sasa wapo baadhi wanalipwa Sh milioni 7 kwa mwezi wakati wengine wakilipwa Sh 60,000.

“Kitendo cha CHADEMA kuwadanganya wananchi, kwamba ili maendeleo yaje lazima wahamie kwenye chama chao, siyo sahihi kwa sababu maendeleo yanakuja baada ya kila mmoja kutimiza wajibu wake.

Katika mazungumzo yake Nchemba, alisema kuna wabunge sana wa CHADEMA wana mpango wa kuhamia CCM wakati wowote.

"Mimi leo natoboa siri katika mkutano huu, nasema hivi, mpaka sasa wabunge saba wa CHADEMA wameshakuja kuomba ili wahamie CCM, lakini tumewaambia wasubiri kwanza wawatumikie wananchi katika kipindi cha miaka hiyo mitano na kisha warudi CCM ili waendelee na siasa,'' alisema.

 

Wanasiasa kupiga kampeni kwenye majukwaa ni moja ya kazi yao lakini ukweli utabakia palepale wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho tusubiri masanduku ya kura mwaka 2015 yatatoa majibu gani.

Nchemba ni Vuvuzela jingine CCM... Asubiri kuukosa Ubunge jimboni mwake 2015 maana CHADEMA imeandaa Msomi anayefaa kuongozi jimbo la Nchemba... Nchemba sio Mwana Siasa.. Bali mpiga Porojo wa CCM.
 
Hata Makada wa KANU Kenya walikuwa wanasema KANU itatawala miaka 100. Kilichotokea wote tunajua. Ndio magamba kitakachowatokea.
 
  • Thanks
Reactions: JGG
nchemba ni tutusa tu linaongea pumba. ni mpumbuvu wa kumdharau tu.
 
  • Thanks
Reactions: JGG
anabwabwaja tu hana jipya
hajui alisemalo, maneno haya haya aliyasema Moi lakini sasa KANU iko WAPI?
aache upuuzi asidhani watanzania wa leo ni wale wa miaka iliyopita.
kwanza yeye mwenyewe atasambaratishwa na dr Kitila Mkumbo akae mkao wa kilia kama toto lililokosa maziwa
 
Arumeru alisema hivyohivyo kuwa Chadema haiwezi kushinda jimbo hilo, kwa vile hawana hata kitongoji huko na mgombea wake (Nasari) ni mtoto! Kwa hiyo hata akiongea hivi tunaelewa matokeo yake ni nini.
 
Kwa maana hiyo hakuna haja ya kupoteza fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2015, maana tayari matokeo yanajulikana.

I am also curious to know, kwa kauli ya Mwigulu, nini kitatokea kama wananchi watachagua chama kingine tofauti na CCM? What will happen? Kama Kenya?
 
Kule jimboni kwake kwenyewe hajui atarudi au vp maana wananchi wamebadilika kifkra. Kila aliposimamia uchaguzi aligonga mwamba sasa anataka wananchi wapi tena wamhakikishie kipigo tena.
MWIGULU ANAWAJUA CHADEMA KWA JUKWAA NI NOMA.
 
Pamoja na mapenzi yangu kwa CCM, bila haya wala soni napenda kusema kwamba kwa hili MH. Mwigilu Nchemba ameishiwa point. Ameshindwa kujenga hoja kutetea kauli yake.
 
Bwana Mdogo MWIGULU kwanza kabisa ww unajiita msomi tena msomi wa uchumi daraja la tatu lakini mböna hufanani nalo? Kuanzia ulivyo mavazi mpaka na tabia! Kwanza kabisa kazi ya siasa huiwezi kama unaiweza basi muda wako wa kuwepo siasani ulikuwa bado hujafika,naomba ukae ufikirie siasa si matusi tena matusi ya nguoni sasa ww kazi yako ni hasa? Manake hueleki kabisa unachokifanya iwe ndani bunge nje ya bunge ww ni vurugu za ajabu tu hivi umelelewa mazingira gani? Manake maadili kwako ni kitu adimu sana yaani mdomo wako hauna breki mpaka unasababisha watu waanze kuwa na mashaka na ww kila kukicha,nadhani labda ulikulia maisha ya umaskini hohe hahe manake saikolojia yangu nikikupimia naona kuna kitu kama hicho kwani ngazi uliyonayo ww unaona kama vile yule aketiye mahali pa juu sana na kumbe ni kitu cha kawaida kabisa, punguza makeke yasiyoleta tija katika chama chako au ndo unatimiza usemi usemao maskini au fukara akipata ------ hulia bwata? Sasa ww hata chama chako hakishtuki? Kwa mambo unayoyafanya?Hii ama sikio la kufa halisikii dawa? Lakini hii ni poa sana mambo haya ya ajabu yaendelee ili CHADEMA wachukue nchi kwani usiku ukiendelea sana kumekaribia kucha sisi wanyönge hatuna la kufanya sana zaidi tunalaani kwa mungu kwa mnayotufanyia manake kila kitu mshaahodhi migodi mbuga za wanyama mashirika yetu yote mmesha yachukua lakini fresh tu
 
First class economist, msukuma mwigulu nchemba, ooh sorry mnyiramba (mkolansi) lameck madelu is just another vuvuzela in sisiem!
 
"Mimi leo natoboa siri katika mkutano huu, nasema hivi, mpaka sasa wabunge saba wa CHADEMA wameshakuja kuomba ili wahamie CCM, lakini tumewaambia wasubiri kwanza wawatumikie wananchi katika kipindi cha miaka hiyo mitano na kisha warudi CCM ili waendelee na siasa,'' alisema.
mchumi mwandamizi daraja la kwanza,kweli?
 
atakwenda yeye kukurupuka na wake za makada wenzie, tena kwa hela za kampeni. huyu ndiye kiongozi wetu 2015
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Na warakini na akiri za huyu mtu! Huenda alisha wai kupatwa na tatizo la ubongo ile sehemu ya kufikiria
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Nashukuru nimebahatika kufika Iramba jimboni kwa mwigulu, hakika ni lazima aweweseke, si suala la ccm tu hata yeye harudi bungeni kwa kipindi kingine, ukipita iramba kila kona wanamtaja Dr Kitila Mkumbo kama mkombozi wao anayekuja, sasa chombo chake kinazama atawaoka nani ghasia au wassira au kawambwa au makinda. wadau mtumbwi wa ccm umetoboka!!!!
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Mwigulu and Lusinde are the best politicians CCM can offer!!
 
:A S 11:Mwigulu Mchemba Igunga ulifanya nini kule?,You better shut your mouth:shut-mouth: sababu wewe ni nchafu hufai kunyooshea wrnzako vidole wakati vinne vinakugeukia wewe
 
Wale wabunge saba aliotangaza kwenye FB yake kuwa watajiunga na CCM waliharibikiwa gari siku hiyo kabla hawajafika Kibaha? Mbona hatujasikia tena kuhusu hao wabunge? How can he be trusted kuhusu CHADEMA kufa 2016 wakati tamko kuhusu hao wabunge 7 kuhamia CCM kwenye mkutano Kibaha halikutimia???
 
Back
Top Bottom