Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,354
- 23,760
Ndugu Zangu watanzania,
Kiukweli na kwa hakika Waziri Mkuu Wetu Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba Mr Clean Ameiva kwelikweli. Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Hakukosea hata kidogo kumpendekeza au kupendekeza jina lake kuwa Waziri Mkuu wetu.
Mwamba anatoa hotuba kwa hisia kali sana, ni mzalendo wa kweli ,analipenda Taifa hili kwa Dhati ya moyo wake. Yupo Tayari kulilinda Taifa hili kwa nguvu zake zote. Anauchungu mkubwa sana na kuwapenda sana watanzania. Ana kiu ya kuona watanzania wanapata huduma zilizo bora ,stahiki na kwa wakati.
Mr Clean Daktari Mwigulu Nchemba Waziri Mkuu wetu Ametoa hotuba ambayo imewafanya vijana ,wazee ,akina mama na watu mbalimbali kutamani asimalize hotuba yake na wala asiondoke. Watu mbalimbali waliokuwepo eneo la Mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi walikuwa wanatamani aendelee kuhutubia tu na kuzungumza naye huku wao wakiendelea kumsikiliza tu.
Hii ni kwa kuwa ametoa na wakati wote alikuwa akitoa hotuba na maneno yenye Kugusa Maisha ya watu na ustawi wao. Alikuwa akizungumza Kama Baba Wa Taifa. Alikuwa akizungumza Maneno yenye kujenga na kuwaunganisha watu ,maneno yenye kujenga umoja wa kitaifa. Ni hotuba iliyowagusa sana vijana hasa katika suala zima la kulinda amani yetu na kutokubali kudanganywa na mtu au watu wanaoishi nje ya nchi kwa ajili ya kuchoma na kuangamiza Taifa letu.
Imefikia hadi hatua akatoa mkono wa zawadi ama Bahasha kwa watu waliokuwa wameimba nyimbo zenye kuhamasiha amani kwa Taifa letu. Hii ni baada ya kuguswa sana na ujumbe wa nyimbo hizo. Kwa hakika Mr Clean ni Balozi wa Amani kwa Taifa letu. Ni kiongozi aliyelibeba Taifa letu ndani ya Moyo Wake.
Anaeleweka vizuri sana kwa watu,ujumbe wake unawaingia na kueleweka kwa uharaka na wepesi sana kwa watu. Anatumia lugha nyepesi na rahisi kufikisha ujumbe wake kwa watu. Ndio sababu watu wanakuwa na hamu na kiu ya kuendelea kumsikiliza tu wakati wote na kutamani asiondoke.
Kwa hakika Rais wetu Mpendwa Amewapatia Watanzania mtu na kiongozi sahihi kabisa katika nafasi ya Waziri Mkuu. Hatajuta wala kujutia kwa uamuzi huo bali atatamani kuwa kama kungekuwa na uwezekano basi Mr Clean aendelee tu kuwa waziri Mkuu hata baada ya yeye Kumaliza muhula wake kikatiba.
Ningependa kusema tu ya kwamba Mheshimiwa Rais Atakuwa na kazi nyepesi sana katika kuendesha na kuongoza serikali yake kwa kuwa amepata mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali za kila siku mchapa kazi kwelikweliiiiiii. Amepata kiongozi ambaye anafanya kazi bila kusubiri kusukumwa ama kukumbushwa kumbushwa kama mtoto mdogo.
Hapa kwa hakika Mheshimiwa Rais amepata mtu wa maamuzi na jasiri kwelikweli katika kusimamia maslahi ya Taifa. Huyu mwamba havai tu Tai shingoni bali amelivaa Taifa katika Damu yake.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.