Mwigulu anatupa funzo kuhusu taifa letu

Mwigulu anatupa funzo kuhusu taifa letu

Umeandika nini, na huyu Mwigulu wako Kafanya nini cha Kuigwa tofauti na Kupigania tumbo lake na CCM yake. Hakuna lolote mmejadili na Kuona uandike hapa Ili akumbukwe.. Ni Kipindi cha Uteuzi, Mbona utaangaika sana...

Tatizo mnakimbilia matusi leta hoja yenye mantiki
 
Ujana hauna deadline, inategemea upo na nani!

Kuna siku tukiwa 'pension' pale Wizara ya fedha ya zamani Jijini Dar es salaam mkabala na Ikulu ndogo ya Nchi, watu walistuka (mimi mmoja wapo) Mama wa watu kastaafu anafatilia Mafao akakutana na Mkongwe aliewapokea kazini miaka hiyooo anaekaribia miaka 85 akamtuma Mlinzi akamwambia 'nistulie yule Binti'…

Mlinzi akawa anamtafuta huyo 'binti' kumbe binti mwenyewe ni bibi


Hivi ujana mwisho waliozaliwa mwaka gani
 
Tofautisha kutetea tumbo lako na kutetea taifa, ungekuwa utaifa kungekuwa na usawa na katiba huru, hizi fingusi za uchaguzi kuiba kura zisingekuwepo
 
umesoma kilichoandikwa au unaleta mihemko yako tu
Nimesom

Nimesoma na nimejibu kwa ufasaha tatizo ni uwezo wako wa kufikiri

Anyway, Mwigulu ni mtu wa singida, alivyokuwa rais wa singida united aliwachukua wachezaji waliokuwa bora akawapeleka Yanga hadi singida united inashuka daraja.

Pia,tundu Lissu alipigwa risasi yeye kama moja ya wabunge wenzake wa mkoa wa singida hakuwahi kwenda hata kumpa pole
Sasa huyu mwigulu aliyeshindwa kuwa mzalendo kwa mkoa wake atawezaje kuwa mzalendo kwa nchi yake?
 
Huyu akifanikiwa kuwa Rais 'atamfunika' JPM

Kama wewe unaamini JPM ni Rais bora basi Mwigulu atamfunika kwa ubora

Kama Wewe unaamini JPM ni Rais Mbovu basi Mwigulu atamfunika kwa ubovu
Wala hujakosea mwigulu ni katili afadhali Mara mia mbili ya jiwe, jiwe huwa anatuma vijana kuua wanaomkosoa, ila nchemba akiwa rais, yeye mwenyewe kwa mkono wake atakuwa anaenda kuwaua wanaomkosoa ktk serikali yake!
 
Chupi ya mbuzi ni mkia wake mwenyewe, Tajiri na hela zake na maskini na watoto wake. Waliosema ukipenda boga penda na ua lake nahisi kuna kitu walikiona kwamba umuhimu wa boga lenyewe ndio unafanya hata ua nalo lipewe thamani.

Tunapouzungumzia uzalendo ni ile hali ya mtu kuwa tayari kujitolea kulipigania taifa lake. Tumeona namna Rais wetu anavyopambana asubuhi na mchana kuhakikisha tunaipata Tanzania tuitakayo yenye kujitegemea na kuweza kusimama kwa miguu yetu wenyewe. Halafu wanatokea watu kwa maslahi ya wao wenyewe na wale wanaowatuma kulitaka kulichafua taifa letu.

Kwanini ninasema tujifunze kwa Mwigulu na hata kwa wengine wanaofanya kama Mwigulu kulitetea taifa letu. Kuna watu wanajisahaulisha kwamba eti mitandao ya kijamii ni ya kuipuuzia wakati dunia ya sasa ipo huko. Unambezaje mtu ambaye akiona watu hao wanatumia hiyo mitandao ya kijamii kuichafua nchi yetu naye anaitumia hiyo mitandao kuwapinga.Ukiua kwa upanga na wewe utauwawa kwa upanga

Teknolojia inaenda kasi sasahivi china wanaingia 6G sisi huku bado 4G inasumbua. Hii inatuonyesha ambavyo dunia inaenda kasi. Sisi vijana huu siyo wakati wa kushangilia watu wanaolipaka taifa letu matope sisi wajibu wetu ni kulisafisha kwa maji na kuondoa tope hilo. Baadhi ya wanasiasa uchwara sasahivi wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kutugombanisha na mataifa ya nje wakati nchi yetu iko shwari na maisha yanaendelea kama jana.

Tanzania ni moja na hakuna Tanzania nyingine ni wajibu wetu kuitetea. Mwasisi wa taifa letu aliposema tunahitaji vijana jasiri alimaanisha vijana ambao wako tayari kuifia nchi yao. Hili Mwigulu anatupa funzo kwa kuonyesha mfano namna ya kulitetea taifa lako. Endelea kutufunza na mlimwengu mimi nitaendelea kuwakumbusha wanapojisahau.

Narudia tena Rais wetu ni mmoja naye ni Magufuli na ndio amezidi kutuheshimisha kwa mataifa mengine kutokana na uongozi wake uliotukuka.

Hili kwetu ni funzo na vijana wazalendo tumelichukua. Na hapa vijana wa UVCCM ni wajibu kukitetea chama pamoja na taifa letu. Huwa napenda Mwigulu anavyomkosoa Zitto pale ambapo anataka kupotosha umma juu ya taifa letu kwenye mitandao ya kijamii.

17/11/2020


Imeandikwa na
Mo Mlimwengu
Mwingulu anachofanya ni ile kitu tunaita unaingia kwenye uwanja wa dansi kudansi ngoma unayoijua maana na tafsiri ya mdondo wake...wanatumia mitandao kwa leo la kuchochea upotoshaji kwa haraka naye anatumia mitandao kwa lengo la kuzima na kuzuia upotoshaji kulitetea taifa.
 
Back
Top Bottom