Mwigulu anatupa funzo kuhusu taifa letu

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Chupi ya mbuzi ni mkia wake mwenyewe, Tajiri na hela zake na maskini na watoto wake. Waliosema ukipenda boga penda na ua lake nahisi kuna kitu walikiona kwamba umuhimu wa boga lenyewe ndio unafanya hata ua nalo lipewe thamani.

Tunapouzungumzia uzalendo ni ile hali ya mtu kuwa tayari kujitolea kulipigania taifa lake. Tumeona namna Rais wetu anavyopambana asubuhi na mchana kuhakikisha tunaipata Tanzania tuitakayo yenye kujitegemea na kuweza kusimama kwa miguu yetu wenyewe. Halafu wanatokea watu kwa maslahi ya wao wenyewe na wale wanaowatuma kulitaka kulichafua taifa letu.

Kwanini ninasema tujifunze kwa Mwigulu na hata kwa wengine wanaofanya kama Mwigulu kulitetea taifa letu. Kuna watu wanajisahaulisha kwamba eti mitandao ya kijamii ni ya kuipuuzia wakati dunia ya sasa ipo huko. Unambezaje mtu ambaye akiona watu hao wanatumia hiyo mitandao ya kijamii kuichafua nchi yetu naye anaitumia hiyo mitandao kuwapinga.Ukiua kwa upanga na wewe utauwawa kwa upanga

Teknolojia inaenda kasi sasahivi china wanaingia 6G sisi huku bado 4G inasumbua. Hii inatuonyesha ambavyo dunia inaenda kasi. Sisi vijana huu siyo wakati wa kushangilia watu wanaolipaka taifa letu matope sisi wajibu wetu ni kulisafisha kwa maji na kuondoa tope hilo. Baadhi ya wanasiasa uchwara sasahivi wamekua wakitumia mitandao ya kijamii kutugombanisha na mataifa ya nje wakati nchi yetu iko shwari na maisha yanaendelea kama jana.

Tanzania ni moja na hakuna Tanzania nyingine ni wajibu wetu kuitetea. Mwasisi wa taifa letu aliposema tunahitaji vijana jasiri alimaanisha vijana ambao wako tayari kuifia nchi yao. Hili Mwigulu anatupa funzo kwa kuonyesha mfano namna ya kulitetea taifa lako. Endelea kutufunza na mlimwengu mimi nitaendelea kuwakumbusha wanapojisahau.

Narudia tena Rais wetu ni mmoja naye ni Magufuli na ndio amezidi kutuheshimisha kwa mataifa mengine kutokana na uongozi wake uliotukuka.

Hili kwetu ni funzo na vijana wazalendo tumelichukua. Na hapa vijana wa UVCCM ni wajibu kukitetea chama pamoja na taifa letu. Huwa napenda Mwigulu anavyomkosoa Zitto pale ambapo anataka kupotosha umma juu ya taifa letu kwenye mitandao ya kijamii.

17/11/2020

da566485-96ca-41ac-a959-695cfc2f0be0.jpg

Imeandikwa na
Mo Mlimwengu
 
Mtazamo wako na huyo wala hamtofautiani unacho jaribu ni kuwa kama panya mla visigino, ili afanikiwe lazima ajifunze kupuliza ili usipate maumivu, ilhali anashiba kwa kutafuna kisigino cha mguu wako, unaotumia kutafutia riski.
 
Umeandika nini, na huyu Mwigulu wako Kafanya nini cha Kuigwa tofauti na Kupigania tumbo lake na CCM yake. Hakuna lolote mmejadili na Kuona uandike hapa Ili akumbukwe.. Ni Kipindi cha Uteuzi, Mbona utaangaika sana...
 
Back
Top Bottom