Mwigulu amwonya spika Anne Makinda

Geeky

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
307
195
Dodoma. Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwigulu Nchemba, amemwonya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuacha kutumia vibaya fedha za Serikali kwa kuwapa posho wabunge kwa ajili ya kwenda kwenye michezo nje ya nchi.

Nchemba ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa bidhaa ya mwaka 2013 iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salumu.

Mkuya katika maelezo yake alisema kuwa kodi hiyo imefutwa kwa laini za simu kwa mtu mmoja mmoja na badala yake imeongezwa katika kodi kutoka asilimia 14.5 hadi asilimia 17.

Katika mchango wake, mbunge huyo alionya kuwa kumekuwa na tabia ya kutumia vibaya fedha za umma jambo alilosema linaanzia ndani ya bunge.

"Naomba tukubaliane katika kubana matumizi, na hivyo ninakuomba Mheshimiwa Spika tuanze na ofisi yako achana na kutoa fedha kwa kuwapa wabunge kwa ajili ya kwenda Dubai kwa burudani,"alisema Nchemba.

Alisema umefika wakati ambao Serikali inatakiwa kufanya uamuzi wa kutumia fedha katika mambo muhimu ambayo yanaigusa jamii kuliko mambo ambayo hayana maana. Kwa upande mwingine aliwalaumu watendaji kuwa wameiangusha Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kushindwa kutoa ushauri na usimamizi mzuri katika makusanyo ya kodi.

Kwa upande wake Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia aliinyooshea vidole Serikali kuwa ndiyo iliyovuruga mchakato mzima wa makusanyo ya kodi ambayo muswada wake ulishapitishwa.

Mbatia alitoa sababu kuwa ndani ya Serikali wamekuwa wakiamua mambo lakini kwenye utekelezaji wake wanagawanyika.

source : Mwananchi Jumapili :
 

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,218
0
Kama ofisi ya bunge imebajeti hilo fungu na serikali Au hazina ikakubali kuna shida gani?
 

Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,125
0
Kwahiyo wakafanye burudani na wake za watu Igunga kama yeye?

Wafanye kwa Gharama zao Hakuna Posho ya Kupakatana, wamepewa Fedha za kwenda kutumikia Wananchi mkitaka kusaliti ndoa zenu nje ya Nchi tumieni Fedha zenu hakuna ataelalamika. Mtu anajaribiwa kupewa KUB (kIONGOZ WA UPINZANI bUNGENI) anashindwa kuwa Muadilifu akipewa u Mizengo Pinda si itakuwa Usaliti kama wa Yuda?
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
61,817
2,000
Wafanye kwa Gharama zao Hakuna Posho ya Kupakatana, wamepewa Fedha za kwenda kutumikia Wananchi mkitaka kusaliti ndoa zenu nje ya Nchi tumieni Fedha zenu hakuna ataelalamika. Mtu anajaribiwa kupewa KUB (kIONGOZ WA UPINZANI bUNGENI) anashindwa kuwa Muadilifu akipewa u Mizengo Pinda si itakuwa Usaliti kama wa Yuda?

Kweli kabisa, ukipewa ukuu afu ukamfunga babu Seya kwa sababu ya kitu K ni utumiaji mzuri wa madaraka.
 

naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,709
2,000
Mbowe sijui alimfanya nini huyu jamaa,maana yake dah kuanzia bungen hadi humu kwa siku JF anaanzisha thread tano kwa ID mbalimbali na vitu vyenyewe ni too personal nadhani hii ni zaidi ya siasa
 

Jambohili

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
262
195
Huyu jamaa mnafki yy anagawa hela kwa ajili ya kuua Chadema huku anazuia wenzake kwenda kucheza. kwanza ni muuaji huyu!
 

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,524
1,250
nawashahri vijana na wazee wa CHDEMA kubadilisha mbinu za ushindi. Tuanze kutongoza wake na watoto wa wana CCM na kuwarubuni kwa kuwa wanawake ndo wapiga kura 2015 tutapita kiulaini kabisa. Kila mwanaCDM mmoja ahakikishe anachuku wake za wanaccm watano ukizidisha na kura milioni mbili tulizopata 2010 tutakuwa tayari na kula zaidi ya milioni kumi. Hapo tutakuwa tumelamba dume
CC:Simiyu yet, Ucho 88 Ritz,Sumu,Faiza,Mzee mwenzangu W. malecela,MloweziChris Lukos n.k. Kaeni chonjo kazi inakuja..
 

Sawana

Senior Member
Dec 19, 2013
130
0
Ukijua maana ya budget utajua kuwa hii hoja ya mwigulu haina mshiko. Hii hela ilishawekwa kwenye budget na budget ikapitishwa kwa hiyo kwa muda huu ni ku-spend. Kusema kuwa spika asitoe hela ya michezo ni hoja iliyochelewa ulikuwa wapi wakati budget inapitishwa. Sometimes huwa hawasomi vitu na kuelewa vinapitishwa wakiwa wanasinzia wakati wa implementation ndo wanangamua makosa na kuanza kelele. Mfano mzuri ni kodi ya sim cards.
 

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
I guess this guyz(Mwigu) anaweza akapewa wizara,hasa ya mambo ya ndani,,,,na pia nadhan Januari anaweza pewa wizara kabisa,
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
nawashahri vijana na wazee wa CHDEMA kubadilisha mbinu za ushindi. Tuanze kutongoza wake na watoto wa wana CCM na kuwarubuni kwa kuwa wanawake ndo wapiga kura 2015 tutapita kiulaini kabisa. Kila mwanaCDM mmoja ahakikishe anachuku wake za wanaccm watano ukizidisha na kura milioni mbili tulizopata 2010 tutakuwa tayari na kula zaidi ya milioni kumi. Hapo tutakuwa tumelamba dume
CC:Simiyu yet, Ucho 88 Ritz,Sumu,Faiza,Mzee mwenzangu W. malecela,MloweziChris Lukos n.k. Kaeni chonjo kazi inakuja..

Wote wagonjwa, utaua chama baada ya miaka 4tu, wakumbushe pia kutumia CDM kulinda kura na afya
 

casampeda

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
2,800
1,500
Wanasema wameanza na mungu,lkn ukiwaangalia kwa undani wote Mboe na Slaa ,wanamatatizo na familia zao wamevunja amri ya 6,kama familia ya watu wasiozidi 7 inawashinda wataweza watu zaidi ya milioni 45!!??
 

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,280
2,000
Mizigo ni mizigo tuu..hivi usifasadi si sehemu ya kampeni ya kubana matumizi?
 

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,808
2,000
Arudishe Gharama alizotumia kwenda Marekani kustarehe na akina Stella na Julie
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom